Tafsiri Ya Mahakama Kuu Kenya Kutangaza Uchaguzi Mkuu Kenya Ni Batili..

Tafsiri Ya Mahakama Kuu Kenya Kutangaza Uchaguzi Mkuu Kenya Ni Batili..

Ndugu zangu,

Tafsiri yake; Kilichoangaliwa na Majaji si matokeo , bali mchakato wa uchaguzi. Kwamba mchakato ulikuwa batili. Na ilivyo, mchakato unaweza kuathiri matokeo.

Kenya imethibitisha kuwa Mahakama ni kimbilio la mnyonge na mwenye nguvu. Ndivyo inavyotakiwa iwe. Raila Odinga alionekana kichekesho na wale waliokuwa wakiamini kuwa Afrika mgombea aliye madarakani akishinda ni kujisumbua kwenda mahakamani. Hongera Sana Kenya kwa kuionyesha dunia kuwa Afrika uhuru wa Mahakama upo, na kwamba anayeshindwa uchaguzi kama anaona hakutendewa haki aende mahakamani, na si kuandamana na kufanya vurugu.

Maggid,

Iringa.
mkuu, huku kwetu bahati mbaya hatuna mahakama bali tuna genge la watu wanaitwa mahakimu wamekaa kwenye viti vya kuzunguka wakisubiri "maelekezo kutoka juu ".
 
Ukiona vyaelea ujue vimeundwa.
Tumeanza kujivunia Demokrasia ya jirani zetu wakenya lakini tunasahau hilo limetokana na UDHUBUTU WAO, UELEWA WAO, UTAYARI WAO, NIA YAO na MAAMUZI YAO YA KUDAI KATIBA MPYA.

Kilichotokea leo matunda ya zao la Katiba mpya ambayo kimsingi iliainisha vyema Mihimili ya utawala, kazi zake na mipaka ya kazi bila muingiliano wa aina yoyote ule.

Kuanzia kwenye upatikanaji wa viongozi wa mihili hii ya utawala rais ahusiki bali kunakuwepo na tume zinazosimamia upatikanaji wao na kwa maana hiyo wanakuwa huru katika utendaji wao.

Pale ambao kunakuwepo na the freedom of judiciary & its supremacy, the freedom of speech & expression etc etc basi ni rahisi kupata haki.

Kwetu Tanzani sidhani hata kama tunarusiwa kuhoji/kupinga matokea ya urais mahakamani ndio maana kwa vile tumenyimwa kuhoji/kupinga matokeo njia pekee inayobaki ya kudai haki huwa ni maandamano.

Swali la kujiuliza ni je kwa nini Mjadala kuhusu Katiba mpya ulizikwa? Na kwa nini awamu hii ya utawala ilitoa tamko kwamba Katiba mpya sio kipaumbele chao?
 
Mimi nilidhani raila kachaguliwa kuwa raisi
Kumbe ni uchaguzi kurudiwa ndani ya siku 60
Ngoja uje tutampiga mara mbili zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu,

Tafsiri yake; Kilichoangaliwa na Majaji si matokeo , bali mchakato wa uchaguzi. Kwamba mchakato ulikuwa batili. Na ilivyo, mchakato unaweza kuathiri matokeo.

Kenya imethibitisha kuwa Mahakama ni kimbilio la mnyonge na mwenye nguvu. Ndivyo inavyotakiwa iwe. Raila Odinga alionekana kichekesho na wale waliokuwa wakiamini kuwa Afrika mgombea aliye madarakani akishinda ni kujisumbua kwenda mahakamani. Hongera Sana Kenya kwa kuionyesha dunia kuwa Afrika uhuru wa Mahakama upo, na kwamba anayeshindwa uchaguzi kama anaona hakutendewa haki aende mahakamani, na si kuandamana na kufanya vurugu.

Maggid,

Iringa.
Acha kuchanganya mada hapa!
Unapozungumzia mahakama pia angalia katiba zinazoongoza nchi hizo!!

Tanzania katiba ni Rais na Rais ni katiba!! Kwa kifupi mahakama za Tanzania haziko huru kwani ni mali ya Rais!!

Kama tungepata katiba ya Warioba Tanzania ingekuwa na katiba bora kama Kenya!!

Kwa katiba tuliyonayo hoja yako ni mufilisi!!!
 
Suluhisho ni Katiba Mpya....na

Tume Huru ya Uchaguzi ....

Kilchotokea Kenya ni funzo pia kwa watawala wetu...

Angalia ule uhuni uliotokea Zanzibar...

Ni wakati sasa wa kudai Katiba Mpya + Tume Huru ya Uchaguzi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasubiri huo uchaguzi ujao utakposikia odinga ameshinda Tz tunajiandaa tu kupokea wakimbizi moshi na arusha

Sent using Jamii Forums mobile app

La hasha! Mambo yatakua kinyume na unayofikiria. Odinga akishinda kila Mkenya atakua na fursa ya kuhakiki umuhimu wake kwa ujenzi wa taifa bila maonevu wala ubaguzi. Sio ajabu Wakenya waliomo diaspora waanze kurudi,kinyume na kuwaona Wakenya wakimbizi Moshi/Arusha
 
Back
Top Bottom