Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kila atakayejaribu kufanya hivyo lazima atakuja na ushuhuda wa ajabu wenye majonzi furaha au hata mshangaoDah kuna kitu nimeamini katika picha, nimerejea picha zangu za zamani toka utotoni ila nimejikuta nadondokwa na machozi.
Nilikuwa sijui picha zina maana gani ila sasa hv nadhani nitakuwa makini katika kuchunguza picha na maisha ya mbeleni.
Aisee kuna picha nilipiga na classmates wangu lakin kuna mmoja katangulia mbele za haki, sasa itabidi nikaingalie vizuri isije ikawa zamu yangu... inasikitisha...Kila atakayejaribu kufanya hivyo lazima atakuja na ushuhuda wa ajabu wenye majonzi furaha au hata mshangao
Hiyo ni hali ya kawaida ya maishaDah kuna kitu nimeamini katika picha, nimerejea picha zangu za zamani toka utotoni ila nimejikuta nadondokwa na machozi.
Nilikuwa sijui picha zina maana gani ila sasa hv nadhani nitakuwa makini katika kuchunguza picha na maisha ya mbeleni.
Kuna picha nilipiga na mtu wangu wa karibu ila kashatangulia mbele za haki lkn leo nimegundua kitu katika picha hizoHiyo ni hali ya kawaida ya maisha
ulitaka hizo picha ziwe sawa na leo?
hata ukipiga nyingine leo kesho itabadilika kulingana na maisha yanavyoenda
Mshana jr. Kali kuliko zote nimewahi ziona ni mtu kuibiwa kivuli chake, yani hata asimame juani hakionekani.Picha ni sehemu ya mwili wako iliyo nje yake wachawi na waganga huroga katika baadhi ya matukio kwa kutumia picha na kinacholeta uhai uhalisia na mawasiliano ya kiroho ni sura
BennyHabari kaka Mshana;
Hizo ni coincidence tu hazina uhusiano na nguvu wala miujiza yoyote kila jambo ni vile unavyolitazama mimi sikubaliani na wewe...
Kama picha ilipigwa zamani kivipi leo niione sawa wakati nyakati zinabadilika? ni lazima nione mabadiliko mengi tu kwa kua muda nao umepita ipo hivyo tu
Nikipiga picha leo na mbuzi wangu nyumbani baada ya miaka mitano yule mbuzi hatakuwepo labda amechinjwa au vyovyote na mimi pia nitakua pengine kama asili ya maisha ilivyo hakuna nguvu wala nini inayotumika hapa
Benny naamini kabisa hukuelewa kabisa nilichoandika,! Ni hivi sizungumzii picha yako na mtu fulani au kitu fulani nazungumzia picha za makundi na hicho unachoita coincidence
Kuna picha sipo nazo hapa lakini picha ya kwanza walipiga watu saba chini ya mtu watatu walikaa kushoto na wane walikaa kulia! Wale wane walikuja kufa kwa kufuatana kwa miezi minne mfululizo
Picha nyingine jamaa wakiwa sekondari siku ya mahafali walipiga picha ya kumbukumbu wanafunzi kama kumi hivi na mabinti wa shule ya jirani
Kwenye ile picha kuna kijana mmoja alikuwa kachuchumaa na binti mmoja halafu mwingine alikuwa kasimama pia na binti...baada ya miaka kupita kila mmoja bila kutegemea alimuoa binti aliyekuwa naye karibu na siku wanakutana kwenye kuangalia album mmoja ndio akakumbuka hilo tukio