Tafsiri ya Sizonje - Wimbo wa Mrisho Mpoto

Tafsiri ya Sizonje - Wimbo wa Mrisho Mpoto

Wachangiaji mmenisaidia sana at least nimeanza kuuelewa huu wimbo. Ama kweli penye wengi kuna mengi. Ngoja niendelee kuusikiliza tena.
Ila neno "sizonje" ni la kilugha ama ni kiswahili fasaha??
Mwenyewe anasema hilo neno sio kiswahili wala sio lugha yoyote ile ya kibantu ni la kubuni tu yeye mwenyewe
 
napita tu,maana inabidi kufikiri kwa kina kabla ya kutoa uchambuzi
 
Ndio jina la wimbo wake mpya Mrisho Mpoto alieyeshirikiana na Banana Zoro. Nimeusikiliza kwa makini lakini bado sijajua maana halisi ya huu wimbo.

Huwa napenda sana nyimbo zake Mpoto, kwani zinakuwa na ujumbe mzito ndani yake ambao huufanya ubongo ufikiri, achilia mbali mtindo au staili yake anayoitumia kuwaburudisha hadhira yake..


========

Baadhi ya maoni kutoka kwa wachangiaji wakijaribu kuufafanua;

Sio soda tu..Ukitaka na vingine utapewa...Fanya msaada basi[/QUO

Sizonje ni mjomba aliyopo sasa
Nyumba-Tanzania
Makaburi-mambo yaliyopita kama escro,meremeta,rushwa tpa
Wanapita madirishani-sheria zipo ila watu hawazifatwi
Jikoni-chama alichotoka sizonje
huna haja kwenda-sio lazima uwe mwenyekiti wa chama faster faster
Harufu ya uzazi haishi mpaka mtoto akuwe-huwezi kutatua maswala ya rushwa kwa muda mfupi
 
Naona vijana wa Mulugo hawauelewa.
 
Naona vijana wa Mulugo hawauelewa.

Mie na elimu yangu ya La Saba 'B' nilichoelewa;

"Tulikaa barazani, tukasikia kelele, kelele toka ndani mtu anaruka dirishani..."

Huyu aliyeruka dirishani nahisi ni miongoni mwa wale waliohama chama tawala kwenda upinzani...
Kama siye ALIYEKATWA, basi atakuwa ni yule ALIYEJIONDOA mwenyewe..
 
Sizonje....hiki chumba usiingie...nitakwambia kwanini....kuna sauti inajirudia mara kwa mara....zamani palikuwa na picha mbili kuubwa mlangoni...moja ni picha na nyingine ni mchoro wa ile picha ya kwanza.
Hii kiboko
 
Naona vijana wa Mulugo hawauelewa.

Ndo maana thread imeanzishwa ili tujuzane kwa kuwa wimbo una sura ya picha ambayo kila mtu anaweza kuitafsiri kwa uelewa wake hivyo,kinachotafutwa ni maana sahihi aliyoilenga muandishi..

sehemu sahihi ambayo kila mtu anaielewa kiurahisi ni sizonje (magufuli) ambaye ni mgeni na anakaribishwa katika nyumba (serikali kuu) asiokuwa na ufahamu nayo vyema hivyo,anapewa maelekezo na mtunzi wa wimbo kwa maana anao uelewa mkubwa wa nyumba hiyo.sasa tupatie maana ya wimbo kwa uelewa wako
 
Sizonje....hiki chumba usiingie...nitakwambia kwanini....kuna sauti inajirudia mara kwa mara....zamani palikuwa na picha mbili kuubwa mlangoni...moja ni picha na nyingine ni mchoro wa ile picha ya kwanza.
Hii kiboko
Jamaa inaonekana alshawah kuish kabla ya kuzaliwa
 
Huu wimbo una maana zaidi ya moja, kwa ufupi kazungumzia maisha ya mtanzania yanavyoongozwa na serikali pasipokufuata sheria.
 
Huu wimbo mzito na mzuri sana, nimeusikiliza na nimeupenda sana kuanzia mashairi, beats, mpoto mwenyewe na banana na huyo farida kwa mbali.
Maana yake ziko nyingi yategemeana na unataka uutafsiri kufit tukio gani, kwa uelewa wangu nafikiri muimbaji alihamasiwa na mambo ya siasa hapa tanzania.
Sizonji ni Magufuli na nyumba ni ikulu (serikali na taifa kwa ujumla) na na watu kupita madirishani na kuacha mlango ni watu kutokufuata sheria, taratibu na kanuni. Kwa ufupi nyumba imekuwa shamba la bibi pia wenyeji hawafaidiki isipokuwa wachache na wajanja. Kazi hamna hivyo vijana wanaishia kuilaumu serikali.
Ile picha ya ukutani ya original yaweza kuwa ni ya Mkwere ambaye aliandaa mtu possibly Baba mdogo, ila bahati "mbaya" kaja mtu tofauti, usiyempenda kaja! Sasa kuna watu wanafiki huko jikoni au idarani na vitengo nyeti wanaanza kujipendekeza na kumsoma Magufuli yuko vipi kwa huo wali wa nazi au mafuta.
Wimbo una mengi sana. Ni suala la kuangalia tukio na kuuvalisha uhusika.
 
Habari za siku Mingi..? Wadau wa Jf...Siku nyingi sijaingia toka..Uchaguzi...Anyway tuyaache hayo..Tufanye kazi...
Wimbo wa Sozanje wa Mrisho Mpoto..Umebeba Ujumbe mzito ambao uko kwenye FUMBO...akionyesha Ujuzi wa hali ya juu ktk Usanii katika Kutumia KISWAHILI CHA MAFUMBO TATA....Nina idea kwa mbali MPOTO...Anatueleza nini hapa...ila bado niko Gizani...
Nawasilisha Wadau kwenu ...Na nyinyi mlieleze fumbo hili la Wimbo SOZANJE..by MRISHO MPO T O...
 
Nimeusikiliza zaidi ya Mara 5 ila sijauulewa huyu mpoto sio mtanzania
Mkuu huu wimbo mm nausikiliza kila siku asubh lakin sielewagi huyu jamaa anamaanisha nn. Nilihisi km weng wanavyohisi kwmb Magufuli anahusika. Lakin bado napata shida sana huyu jamaa katisha
 
Back
Top Bottom