Huu wimbo mzito na mzuri sana, nimeusikiliza na nimeupenda sana kuanzia mashairi, beats, mpoto mwenyewe na banana na huyo farida kwa mbali.
Maana yake ziko nyingi yategemeana na unataka uutafsiri kufit tukio gani, kwa uelewa wangu nafikiri muimbaji alihamasiwa na mambo ya siasa hapa tanzania.
Sizonji ni Magufuli na nyumba ni ikulu (serikali na taifa kwa ujumla) na na watu kupita madirishani na kuacha mlango ni watu kutokufuata sheria, taratibu na kanuni. Kwa ufupi nyumba imekuwa shamba la bibi pia wenyeji hawafaidiki isipokuwa wachache na wajanja. Kazi hamna hivyo vijana wanaishia kuilaumu serikali.
Ile picha ya ukutani ya original yaweza kuwa ni ya Mkwere ambaye aliandaa mtu possibly Baba mdogo, ila bahati "mbaya" kaja mtu tofauti, usiyempenda kaja! Sasa kuna watu wanafiki huko jikoni au idarani na vitengo nyeti wanaanza kujipendekeza na kumsoma Magufuli yuko vipi kwa huo wali wa nazi au mafuta.
Wimbo una mengi sana. Ni suala la kuangalia tukio na kuuvalisha uhusika.