Tafuta pesa, hakuna mwanamke wa mtu

Tafuta pesa, hakuna mwanamke wa mtu

Habari

Habari

Hapa tena na tena ndugu yangu kijana wenu nimekuja kwa unyenyekevu sana ndugu yenu.

Kwa ufupi ndugu yenu ninaomba msaada na nina matumaini nitafanikiwa kwa maana hapa JF kuna manguli wa kila namna ya wamejaaa tele.

Kijana mwenzenu nimezulumiwa haki yangu.

HISTORIA FUPI
Mwaka 2013 nilioa mwanamke wa Kitanga, nilibahatika kupata mtoto mmoja na uyo binti, mwaka 2015 nilibahatika kujenga nyumba.

Mwaka 2017 nilibahatika kununua gari lenye dhamani ya ML 9, wakati hayo yote nikiyafanya nilikuwa na mke wangu mpendwa tena alikuwa ananipenda kupitiliza

Mwaka 2018 niligundua mke wangu ana mahusiano na kijana wangu wa dukani, kiukweli iliniuma sana sana baada ya ushauri wa marafiki nikaamua nimuache hapo ndipo sheria ilipo chukua nafasi.

Ila sheria ilinisaliti na ndipo maisha yangu yakabadilika kabisa wakati nanunua kiwanja gari vyote niliandika kwa jina lake.

Na sasa mwanamke amebadilika na kusema vyote ni vyake na sheria imemuamini kwa maana majina yote ya kwenye hati ni majina yake.

Kiukweli inaniuma sana kwa sasa sina hata pesa ya kuendeleza kesi.

SASA BASI NAOMBA MSAADA WA NGUVU KWA MWENYE UWEZO

NATAFUTA MGANGA TENA MGANGA WA KWELI AMBAE ANAUWEZO WA HALI YA JUU NIWEZE KUTETA NAE KWA MAANA MWENZANGU YEYE ANATEMBEA KWA WAGANGA KILA SIKU

NAOMBA YOYOTE ANAE TAKA KUNISAIDIA AJE INBOX NAITAJI MGANGA NAITAJI MNGANGA

NISAIDIENI NDUNGU ZANGU.
FB_IMG_1732143510306.jpg
 
Kama unatumia akili vizuri ni rahisi sana hilo, Kama una tumia hisia itakuletea shida
 
Back
Top Bottom