Tag wahenga wenzako

Tag wahenga wenzako

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] amezingua hyu muhenga VP wewe ushakula tupipi twamviringo tunamistari tumetobolewa kati!!utoke kwenu ukaoe[emoji12] [emoji12] [emoji12]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Shikamoo muhenga
 
UTAJUAJE KAMA WEWE NI MUHENGA?

1. Kama ulikata daftari mara mbili. Kipande kimoja ukaacha nyumbani na kingine ukaenda nacho shule. Wewe ni muhenga.
2. Kama ulitumia kipande cha kandambili kama ufutio.
3. Kama ulikanyagia kisigino ulipotoka kuoga ili usichafuke kwa kuwa hauna kandambili....Wewe ni muhenga.
4. Kama kwenu mlianika betri za national ili ziongezeke chaji kwenu..... Wewe ni muhenga.
7. Kama uliweka chumvi kwenye uji mweupe ndio ukanywa....Wewe ni muhenga
13.Kama ulivalishwa nepi na sio papmpers.....Wewe ni muhenga
19.Kama ulivaa kandambili mikononi wakati mnacheza mpira wa makaratasi "one touch".....Wewe ni muhenga
20.Kama uliweka kioo chini ya dawati ili uwachungulie wasichana...Wewe ni muhenga
23.Kama uliwahi kutengeneza magari ya waya,mabox na makopo yalioisha KIMBO Wewe ni muhenga
24.Kama uliwahi kucheza ule mchezo wa kifimbo cheza Wewe ni muhenga
27.Kama uliwahi kuvaa ndala za SKY WAY ,NODIN,UMOJA na viatu vya bora Wewe ni muhenga
29.Kama uliwahi kuogea sabuni ya komoa,komesha,mshindi,ilula Wewe ni muhenga
30.Kama uliwahi kutumia TANBOND,KIMBO,,,,Wewe ni muhenga
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Hebu watag wahenga wenzio uliocheza nao
Hizi zinanihusu kabisa Muhenga mm
 
Hahahaha kama uliangalia mechi za akina:
Ronaldo de lima
George weah
Taribo west
Patrick Mboma
Ndief wa cameroon
Nuno Gomez wa ureno
Luis Figo
David Beckham
Ulimboka Mwakingwe
Pawasa
Mohamed Mwameja
Mrisho Ngasa n.k

Na kusikiliza miziki ya kina:
Blue ya Mr blue
Leo Ay
Zeze TID
Fatma, Rah P,Sister P ,Joan, Razia kipozi n.k

Kama uliangalia pia maigizo ya
Mambo hayo
Kaole

Kama uliimba wimbo wa ccm kabla ya kumwamkia mwalimu anapoingia darasani nawe ni mhenga pia

Kipindi cha watoto cha Itv cha Eddy

Kama ulisikiliza mama na mwana , siku ya leo show , majira ,mazungumzo baada ya habari ,maigizo ya kina Jangala, mzee mundu ,mama hambiliki n.k

Kama umeshuhudia yote we ni mhenga daraja la kati
 
Wahenga tumekuja.

Kama umechezea tiara wewe ni mhenga.

Kama ulitoboa vikopo vya mafuta na kufunga Uzi ili kuongea kama simu. wewe ni mhenga

Kama ulimfunga kamba Komba mavi(mnambe) mguuni ili apae ukishikilia Ile kamba. Wewe ni Mhenga.

Kama ulitumia soksi za punda milia na mifuko ya spot. Wewe ni Mhenga.

Kama ulitumia kalamu ya Beifa, Bic, shangingi. Wewe ni Mhenga.

Kama ulipanda mabasi aina ya TATA. wewe ni Mhenga.

Kama ulibandika stika za wachezaji kwenye ukuta au daftari la shule. Wewe ni Mhenga.
hahahahaha hapo kwenye soksi za pundamilia nmevaa sana enzi hzo..
Na kuna nyngne zlikuwa na rangi nyekundu na nyeupe
 
Kama uliwahi kusafiri masafa marefu umevaa sare za shule ili usilipe nauli wewe ni muhenga
 
Kama ulisoma gazeti la Mfanyakazi, Moto moto, Dar leo, Alasiri, na kumekucha basi wewe ni muhenga
Mkuu Ahsante kwa KUMBUKIZI. Shukrani MHENGA Mwenzangu

Sent from my HTC Desire 820G PLUS dual sim using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom