Tahadhali, wezi wamekuja na mbinu mpya kabisa

Tahadhali, wezi wamekuja na mbinu mpya kabisa

Uhuru24

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2015
Posts
4,112
Reaction score
4,361
Wezi/majambazi baada yakuona kuna shida kidogo kuingia ndani kutoka na milango yetu na madirisha kuwa imara wameamua kuja na mbinu mbadala kabisa, kiasi kwamba mbinu hii itawafanya kuwarahisishia jamaa kufanikiwa jambo lao.

Wanachokifanya hao wezi/majambazi ni kuruka ukuta kisha wakisha zama wanafungulia maji kutoka kwenye bomba, sasa ukistuka usingizini na kukuta maji yanamwagika ndipo utakapochukua maamuzi ya kufungua mlango na kwenda kufunga bomba, hapo ndipo mtakapoingia wote ndani.

#JAMBO LA KIZINGATIA.
Hakikisheni kwa umakini kabisa kwamba bomba la maji limefungwa, na pindi utakoposikia usiku maji yanamwagika ni bora ukaacha kabisa kutoka nje kwenda kufunga bomba, maaana uwamuzi utakao chukua kwenda kufunga bomba hapo mtaongozana na wazee wa kazi kuingia ndani.

Hii imetokea kwenye nyumba ya jirani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa taarifa but hii sio mpya maana ilishagunduika hakuna anaeitumia tena
 
Nyie wezi tuoneeni huruma wakati mwingine,yaani kweli uko ndani unasikia maji yanamwagika unayaacha kisa kuogopa wezi ! na kinachokuumiza zaidi una deni la kampuni ya maji umelimbikiza zaidi ya miezi miwili,kwakweli hayo maumivu ni makali sana,hapa ndipo unapokuta mwanaume wa shoka analia machozi bila kupigwa, na kutoka nje hawezi,maana anajua wazee wa kazi wanamsubiria ili wafanye yao....
 
Ukifungua wanakuteka,ila jamaa wanajiamini sana aisee hawaogopi kufa,hawajua ndani kabaki nani wanamiliki silaha gani?
 
Tafuta kufuli nzito ya bomba hapo umemaliza maana wakija kuanza kukata tu wanakushtua unapiga kelele


OVa
 
aa6baf73-084f-4e7b-a004-58029b83df94.jpg
320a5361-4518-4ba7-ac0c-489f33d92b49.jpg
a34f30bc-919d-4ea6-951c-cd8971223fbb.jpg
b1f9ac78-ca5e-47de-8052-083b1a833186.jpg
22412d6b-52c4-4bf8-92ce-944768ed1202.jpg



Hizi picha nmeona leo wanasema huko kinyerezi watu wameua mbwa wakaiba vifaa vya magari. Namna hii si mtu unarudi kupanda daladala usawa huu.
 
Sawa mkuu hiyo imetokea maeneo gani maana huku kwetu tunanunua maji kwenye mkoko10 ayo mabomba hatujawai kuyaona majumbani.
 
Back
Top Bottom