Tahadhari: Barabara ya Morogoro kwenda Dar es Salaam haipitiki kutokana na msongamano wa magari kuanzia Kibaha hadi Chalinze

Tahadhari: Barabara ya Morogoro kwenda Dar es Salaam haipitiki kutokana na msongamano wa magari kuanzia Kibaha hadi Chalinze

BVR 2015

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
344
Reaction score
713
Wasafiri ambao wanaenda mkoani kupitia barabara ya Morogoro kuanzia Kibaha hadi Chalinze kwa jioni ya leo haipitiki kutotokana na foleni iliyosababishwa na ujenzi unaoendelea katika mlima wa Mlandizi.

Matokeo ya kufunga barabara upande mmoja umesababisha mwingiliano wa magari na kufunga njia moja iliyobaki. Kuanzia saa 9 na nusu nimetoka Dar kwenda Dodoma tumenasa kwenye foleni hapa Ruvu darajani saa 2.55 hakuna dalili za gari kutembea.

Nawashauri wasafiri wenzangu wapite Bagamoyo road
 
Ndio maana hata kama naenda Moro nazunguka Bagamoyo! Hio njia haina guarantee!
umenipa bonge la idea bora kuzunguka bagamoyo huku mlandizi michosho sana yani hata safari ya kawaida gari inaanza kwenda kufunguka kuanzia chalinze kwenda kule
 
Mkuu uko sahihi kabisa. Hali ni mbaya sana. Mimi pia nimeshakaa hapa zaidi ya masaa manne.

Tatizo mkandarasi anayejenga hicho kipande anaonekana kuwa na speed ndogo bila shaka kutokana na vifaa duni.

Barabara muhimu kama hii wapewe wakandarasi wakubwa kazi wanafanya usiku mkubwa na kwa haraka bila kusababisha bugdha kama hii.
 
Poleni..badala ya njia kupanuliwa tutaziba viraka wee mpaka mkombozi mwengine aje.
 
Leo Kama unatoka Dar kwenda Chalinze kupitia Kibaha kula kabisa, uwezekano wa kulala njiani ni mkubwa Sana.
Nimetoka Mbezi Luis saa kumi na nusu, Hadi Sasa bado sijaiona kongowe.
Mlioko mbele yangu, hii foleni imesababishwa na nini?
 
Back
Top Bottom