Mpuuzi huyu Mwabukusi ana akili zile zile za chuki zetu za kiafrika, kudhani kuwa matatizo yetu chanzo chake ni watu tunaoweza kuwanyooshea vidole.
China wapo bilioni 1.4 wao ndio walitakiwa wawe wa kwanza kunyooshea vidole wachache wanaodhani wanawasaliti lakini ni kinyume chake kwa sababu elimu wanayoitoa ni ile ya udadisi tangu wakiwa watoto.
Wanamuandaa kila mchina aweze kuishi mahali popote pale mbali na China. Sisi watanzania kwa kupewa elimu za kuja kuajiriwa baadae tunajikuta tunahangaika pale ajira rasmi zinapokuwa chache, matatizo yetu mengi huanzia hapo.
Sasa huyu mpuuzi mwanasheria kaingia katika mtego ule ule wa kunyooshea kidole tabaka la viongozi, hakuna duniani nchi isiyo na tabaka la wachache wenye kuongoza hiyo ndio hulka ya kibinadamu imejaa ubinafsi mwingi.
Hao DP wapo katika mataifa mengi tu na ni kwa sababu ya uwezo wao wa kazi ndio maana wanakubaliwa, anataka watoke hapo TPA anayo 'know how' yenye kuweza kutupatia mapato na ufanisi wa kazi kulinganisha na hao DPW?.