Tahadhari Kubwa: Morogoro, madaraja na mafuriko-nchi kukatika mawasiliano!

Tahadhari Kubwa: Morogoro, madaraja na mafuriko-nchi kukatika mawasiliano!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
18,653
Reaction score
31,010

(Mafuriko daraja la Dumila mwaka jana-mwaka huu kuna uwezekano kutokea tena mafuriko)

Mkoa wa Morogoro umabahatika kupitiwa na barabara karibu zote zinazoingia Jiji la Dar es salaam.
Barbara hizi zinavuka mito mingi inayoingia Bahari ya Hindi.
Sasa hivi tunaona sarakasi za kukatika madaraja kwa mfano Kiyegea hivi karibuni, na Dumila mwaka mmoja uliopita.

Wizara ya Ujenzi haiwezi kubea lawam kwa kukatika hii miundombinu adhimu lakini vile vile serikali kupitia wizara nyingine ikemee kwa nguvu zote matumizi mabaya ya ardhi ikiwemo kulima kwenye milima na kando ya mito.

Udongo unaoingia mtoni katika madaraja unasababisha maji kujaa hivyo kubebea matuta ya barabara.
Hicho ndicho kilichotokea Kiyegea na kabla ya mwisho wa mvua ndicho kitatokea pale Dumila.

Tukilima kwenye slope kali za milima na kwenye kingo za mito matokeo yake tunayaona live.
Hii ni hatari kubwa kwa mawasiliano ya nchi.
 
Badara ya kugombana na mvua anagombana na watendaji...kasikiaga korona kakimbilia Dodoma, watu wengine shida tupure

Don't make a promise you can't fulfill...
 
Kama hili nalo wahandisi wa TANROADS wana kosa gani hapo? Bwana mkubwa atandelea kuwa tumbua?

Kumbe kosa wala sio lao. Kosa ni design factor iliyo tumika. Jamaa alie fanya design hakuangalia return period ya juu ya discharge. Kakaa ofisini kaweka mchoro kawapa wakandarasi. Sasa mvua zimekuja kubwa kuliko design ya daraja lazima kuwe na shida. Huwezi kuyazuia maji maana yata tafuta njia ya kutoka.

Si bure hata hivi sasa utakuta watu wa hali ya hewa hawaja chukua discharge inayo pita kwenye mito hivi sasa kwa ajili ya future references..
 
Kama hili nalo wahandisi wa TANROADS wana kosa gani hapo? Bwana mkubwa atandelea kuwa tumbua?
Kumbe kosa wala sio lao. Kosa ni design factor iliyo tumika. Jamaa alie fanya design hakuangalia return period ya juu ya discharge. Kakaa ofisini kaweka mchoro kawapa wakandarasi. Sasa mvua zimekuja kubwa kuliko design ya daraja lazima kuwe na shida. Huwezi kuyazuia maji maana yata tafuta njia ya kutoka.
Si bure hata hivi sasa utajuta watu wa hali ya hewa hawaja chukua discharge inayo pita kwenye mito hivi sasa kwa ajili ya future references..

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni kweli mkuu lakini nafikiri tatizo kubwa zaidi ni hili la kilimo kwenye miinuko mikali ya milima hasa Gairo na Turiani..
Cheko hiyo clip na utona maji ya mto ni kahawia na yamejaa udongo wenye tope.
Hapo ndo madaraja yatafeli
 
Kwa hivyo unashauri hao wakulima wakalime wapi au waache kulima serikali itawapelekea chakula

Sent using Jamii Forums mobile app
Jati_Luwih.jpg

Ni suala la ukulima bora tu na inaitwa terrace farming.
Kwa wenzetu kama Vietnam, ni wakulima wazuri sana kwenye slopes.
Vipindi vya ukulima boora wala hatuvisikii siku hizi.
 
Jana nimeumia sana wahandisi kupumzishwa kazi na karipio la mkuu kwa Waziri na Watendaji Tanroad. Ushauri wangu wataalam wote nchi nzima kagueni madaraja nchi nzima, yenye kasomo wekeni stop order yasitumike. Kwa maandishi maamlaka husika.
Majanga ya asili yapo hata mataifa makubwa.

Ijulikane tu kuwa kama fedha hakuna, uhandisi ni bure!!
 
Back
Top Bottom