TAHADHARI kwa mnaotaka kuanzisha biashara nchini Tanzania kwa sasa!

Ungeongezea pia kwa kuwaonya wale wanaoenda kuchukua mkopo benki na kuweka dhamana nyumba... Wategemee kulala nje siku si nyingi...
 
Biashara mkuu hatuachi,, lazima tuendelee tu hata kama wakituua lazima tufanye, maana 2020 haiko mbali tushuhudie jamaa anavyorukaruka kichura chura!! Lazima betri zilegee safari hiyo!!
 
exactly.umepigilia yani
 
Usisahau na maduka ya dawa maana kuumwa kupo pale pale tena yawezekana awamu hii watu wakaumwa zaidi[emoji5][emoji5]
Duuuuu.......INAWEZA KUWA AWAMU YA KUUMWA....Mungu aepushie mbali kwa kweli
 
Mkuu nikwel anachoongea jamaa me mwenyewe ni mfanya Biashara nakuhakishia sasa hivi mauzo yamepungua kwa zaidi ya 60% mkuu
Achana na huyo inawezekana katika maisha yake hajawahi kufanya biashara halafu anaanza kupiga porojo


Watu wanashauriana yeye anakuja na bla bla zake

Mimi mwenyewe nilikuwa na mpango wa kuanzisha biashara lakini nimesita nafikiria kwa umakini
 
Zimbabwe yenyewe ambayo uchumi wake ushakufa lakini watu bado wanafanya biashara, sembuse nchi bikra kama bongo, miporojo kibao tena iliyojaa mihemko ya kibavicha
Uvivu unamsumbua, ukosefu wa ubunifu!
 
Zimbabwe yenyewe ambayo uchumi wake ushakufa lakini watu bado wanafanya biashara, sembuse nchi bikra kama bongo, miporojo kibao tena iliyojaa mihemko ya kibavicha
Ila kuheshimu mawazo yake ni vizuri pia,kumbuka ilala biashara nyingi zimekufa.
 
Ila kuheshimu mawazo yake ni vizuri pia,kumbuka ilala biashara nyingi zimekufa.
Pia,jana nimepita katikati ya mji wa Morogoro na kuuliza bidhaa moja maduka yote na sikupata,Mhindi mmoja akaniambia Biashara ni mbaya sana,haamini kama huyu Rais na mfumo wake vitadumu muda gani.Mimi mwenyewe nikamwambia usiseme makazini ni kwema,Kuna shida isiyo ya kawaida Rais ni kama anongoza wanyama Serengeti wanapohama kwenda Kenya.
 
Ila kuheshimu mawazo yake ni vizuri pia,kumbuka ilala biashara nyingi zimekufa.
Ila ILALA ni halmashauri zake zinaongozwa na upinzani kwanini wasiwawekee watu unafuu wa ushuru maana tunaaminishwa ndio wakombozi wa shida zote
 
Nlivoona heading nkajua kuna point ztaongelewa apa, wakati huu ndo ule mda watu wanasema matatizo ni mengi kwahio opportunities nazo ni nyingi, wakati unaendelea kuwaambia sio wakati mzuri wa kuanzisha biashara watu walishawaza jinsi ya kutengeneza ela nyingi sana tena naona saahv hadi betting wana branch karibia kila kona, CRDB waliotangaza hasara ndio kwanza wanaongeza matawi na kuajiri watu wengi zaidi, juzi apa mwananchi kama ulisoma kuna benki wametangaza faida ya mabilion inaonyesha jinsi gan hujawahi shika bishara yoyote, USISHAURI WATU UJINGA
 
Ushauri ni mzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…