Katika kipindi hiki muhimu kwa mustakabali wa taifa letu, sauti ya wananchi inazidi kuwa wazi na isiyoweza kupuuzwa: “No Reforms, No Election”. Hii si kauli ya jazba bali ni ujumbe wa kizalendo kutoka kwa Watanzania wanaotaka misingi imara ya demokrasia, uwazi wa uchaguzi, na uongozi wa haki.
Wananchi hawako tayari kushiriki tena katika mchakato wa uchaguzi unaoendeshwa bila uhalali, usawa na uangalizi huru. Wanahitaji mageuzi ya kweli katika mfumo wa uchaguzi, hasa kuhusu namna Tume ya Taifa ya Uchaguzi inavyoundwa, inavyofanya kazi na inavyowajibika.
Serikali isikose kusoma alama za nyakati. Siyo muda wa kubembeleza ukweli — wananchi wanahitaji mabadiliko ya msingi, na hawako tayari kurudi katika mizunguko ile ile ya uchaguzi wa mabavu, usio na uwazi wala uhalali.
Kila mkutano wa CHADEMA unaohudhuriwa na maelfu kwa maelfu ya Watanzania si mkutano wa kawaida. Ni ujumbe wa moja kwa moja kwa serikali kwamba watu hawa hawakubaliani na uendeshaji wa nchi kwa mazoea ya mabavu na udanganyifu wa kisiasa. Wingi wa watu wanaojitokeza kwenye mikutano hii ni ishara ya kutokuunga mkono mfumo wa sasa wa uchaguzi na ni salamu ya kumkataa wazi wazi mtu au taasisi yoyote inayotaka kuhalalisha udikteta kwa kivuli cha uchaguzi.
Endapo serikali italazimisha uchaguzi Oktoba 2025 bila kufanya mageuzi haya ya msingi, na kisha kujitangaza washindi bila ridhaa ya kweli ya wananchi, basi ni vyema ikajua kuwa sauti ya “No Reforms, No Election” haitakuwa imeishia hapo.
Chachu ya mabadiliko imeshaingia ndani ya watu. Ari ya kutaka mabadiliko ya kweli haiwezi kufutwa kwa propaganda wala mabavu. Badala yake, itaibuka kwa nguvu zaidi kama mwamko wa kudai mabadiliko makubwa zaidi ya mfumo mzima wa nchi — ikiwemo Katiba Mpya.
Serikali ijue wazi kuwa:
Wananchi wanaweza kuibua kauli mpya kama vile “No Reforms, No Participation” au “No Katiba Mpya, No Participation” kuonesha kutoshiriki kwao katika siasa, utawala au hata uchumi.
Upinzani unaweza kuongoza harakati halali za kiraia kwa kusisitiza wananchi wasishirikiane na serikali, ikiwemo wito wa kugoma kulipa kodi kama njia ya amani ya kupinga mfumo usio wa haki.
Kutakuwa na ugumu mkubwa wa utawala, kupungua kwa uhalali wa serikali, na kuporomoka kwa mshikamano wa kitaifa.
Katika hali kama hiyo:
1. Serikali itakosa ridhaa halali ya wengi, jambo linaloifanya kuwa serikali batili mbele ya macho ya wananchi.
2. Na kwa kuwa uhalali wa serikali hutokana na watu, basi serikali isiyokuwa na uhalali huo haina kinga ya kikatiba ya kuendelea kutawala.
3. Hali kama hiyo inaweza kufungua mlango wa mjadala mpana wa kitaifa kuhusu hatima ya utawala huo, na hata vyombo vya usalama vya nchi kama jeshi la wananchi vinaweza kujikuta katika nafasi ya kuamua kwa maslahi ya taifa, kutafuta njia ya kurejesha utawala halali na wa wananchi.
Hili si tishio bali ni taarifa ya mapema. Serikali isione maigizo yake ya kuendelea na mchakato wa uchaguzi yasiyo shirikishi kama jambo linaloleta afya ya kisiasa. Hali hiyo huongeza mgawanyiko, husababisha mparaganyiko, na mwishowe huharibu mshikamano wa kitaifa.
Hili ni onyo la tahadhari, Serikali yenye busara husikiliza kabla hali haijafikia pabaya. Wananchi wa Tanzania ni wavumilivu lakini sio wajinga. Wanaelewa haki zao, na sasa wameamua kuzisimamia.
Wananchi hawataki vurugu — wanataka HAKI. Lakini haki ikizuiwa kwa makusudi, huzaa mgogoro. Suluhisho la kisasa na la kizalendo ni moja tu: rejea meza ya maridhiano, fanya mageuzi ya kweli, jenga upya imani ya wananchi.
No Reforms, No Election ni mwito wa mabadiliko. Ukipuuzwa, utaibuka kuwa vuguvugu la kudai ujenzi mpya wa taifa — kupitia kauli kama “No Katiba Mpya, No Participation” na hata mgomo wa raia dhidi ya mfumo mzima wa utawala kandamizi, ikiwemo kutokulipa kodi au ushirikiano mwingine wowote na serikali.
Hili ni ombi la mwisho kabla hasira ya watu haijawa janga kwa taifa.