..Nashuudia kwamba huu Uislam wenu ni dini ya haki kabisa
Wanaotaka kuufahamu uislamu wasome vyanzo vya habari vya kiislamu sio vya wababaishaji wasiojuwa uislamu au wanapotosha makusudi,kila ibada inayofanyika ndani ya uislamu ina maelekezo yake,na faida zake,
1.Swala kwa waislamu,ni tendo la mazoezi kwa viungo kwa siku mara tano,maskini,tajiri,mfalme,rangi tofauti wote wanaswali pamoja na kugusana.,.(Yapo maelezo yake kwa urefu)
2. Kufunga ni tendo la Afya, Mtume Muhammad (S.A.W) asema Fungeni mpate Afya. (Yapo maelezo kwa urefu).
3. Kuhiji ni tendo la kukutana waislamu wa dunia nzima mwaka Mara moja,imejumuisha mazoezi,afya,semina,makongamano,kubadilishana mawazo, kusaidia maskini, kuangalia neema za uumbaji wa Allah,kwa kukutana watu,makabila,rangi tofauti,matajiri,maskini, Wenye
Vyeo,wasio na vyeo nk(Yapo maelezo kwa urefu).
4. Maziko ya kiislamu
a. Tajiri na maskini wanazikwa kisawasawa
b. Tajiri,maskini,mfalme wote wanazikwa na kuvalishwa sanda aina moja.
c. Wote wanazikwa kwenye kaburi na kuguswa na michanga bila kujali utajiri,rangi,cheo,umaskini wa maiti.