Tahadhari kwa wanaotaka kuingia kwenye biashara ya kilimo

Huyo mpuuzi tumsamehe bure. Pengine anasumbuliwa na stress.. Si unajua tena maisha sa hivi ni vurugu tupu😀
Maisha vurugu kwako sio kwangu, mimi kwangu mstari.
 
Unashukuru kupata taarifa kutoka kwa mkulima alieshindwa ? huyo hakuwa mkulima, alijaribu kilimo kwamaana alisikia kuwa kilimo kina lipa akaona tofauti akapanic. hakufanya research kabla ya kilimo, aliingia kichwa kichwa kwa kutumia kilimo kwanza ( kilimo cha kizamani). Alafu unadai kakupa ushauri mzuri.
 
hapo umenena kiukweli. YATOSHA
 

Mtu mwenye akili utoa ushauri, unapoteza muda kuponda lakini utoi ushauri. Mimi ni kweli nilikurupuka ndio maana nikaandika kuwa watu wawe na taadhari, maana kuna vijana wengi wanaingia kwenye kilimo kwa kukurupuka. Nashindwa kuelewa point zako ni zipi?, au unaamini watu wote wako aware kama ulivyo wewe?.
 

Haya maelezo ndio ulitakiwa uyatoe mwanzoni mkuu, hapakua na haja ya kutumia lugha kali kiasi kile, hata hivyo nafikiri Nkobe ametolea mfano huo kuonyesha kwamba watu wengi wanafanya hivyo na ni kweli wengi wanaofanya kilimo hawafanyi kilimokama biashara kama ambavyo umeelezea vizuri suala la umuhimu wa utafiti.

Unaona sasa mtu akisoma bandiko la mwanzo akichanganya na nyongeza yako anapata kitu kamili? Ni kujifunza kuvumiliana tu mkuu. Ahsante kwa mchango wako!
 
Last edited by a moderator:
Hata hivyo kuna kujifunza kwa njia mbili, ya kwanza ni kuangalia wengine wamekosea wapi kisha wewe ukafanya tofauti na kujihadhari usikosee. Njia ya pili ni wewe mwenyewe kukosea na kujifunza kutokana na makosa yako! Cha msingi kama maelezo yatasaidia wengi sioni kama kuna tatizo!
 

We jamaa unaonekana ama hujawahi kulima ama huna uzoefu wa kutosha wa kilimo...ama unalima kama hobi tu.

Sioni sehemu uliyotoa maboresho.Unakazana mtoa mada kashindwa sasa wewe uliyefanikiwa boresha uzi watu wajifunze..Unaweka neno Research kujifanya unajua sana...Hata ufanye research ya aina gani bado kilimo cha bongo kina changamoto nyingi mpya zinazoibuka kila siku.Mfano mimi nililima sehemu mwaka huo wadudu wakaingia sikuvuna kitu.

Umejaa majivuno kujifanya unalima kisasa huku huweki chochote cha kujifunza kwa wengine.Eti research si tungekusikia Unamuuzia Mahindi Bakhressa..
 

Mkuu umetimiza Wajibu wako wa kushauri..wenye kusoma wamekuelewa..Kilimo kina changamoto mpya zinaibuka kila siku ni jukumu kuyasema ili wanaoingia wajue...
 
Thanks Samaritan
 
Last edited by a moderator:
Nchi hii hakuna mkulima au wakulima watakaoweza kujaza vihenge vyake.
OOOhh kilimo chanza ,sijui nini nini
Mahindi,ngano akiacha ku import.
Taznania tutakufa njaa,bei vitu vitaenda juu.
 
Tatizo lako kubwa ni hukufanya utafiti, changamoto ulizotaja ni za kawaida sana ambazo kama ungefanya critical analyzation usinge fail
 
Gunia la mahindi mikoa ya kusini halijawah kushuka chini ya elfu tisini
Ukitaka kikulipe fanya tofauti na wenzio, hasa ni lazima umwagilie. Mikoa ya kusini ina mvua ya kutosha, uwezekano wa kuvuna ni mkubwa, tatizo la kule gunia la Mahindi linaweza kushuka hadi elfu 15 maana kila anaelima anapata. Ukiweza kuleta Dar sawa
 
Mtu ambae hajawahi kulima na anahamasisha kulima kupitia mtandao utamjua tu, Tusi ulilomtukana mwenzio likurudie. Mimi nimelima zaidi ya miaka 30 na nimelima kilimo cha kila namna cha kutumia mvua cha kumwagilia kwa matone na kawaida.
Biashara ya kilimo ina changamoto lukuki. Unaweza kuwa na maji ukachambuliwa na magonjwa ambayo si rahisi kuyatibu. Unawaeza ukavuna kwa wingi ukapambana na changamoto ya soko ambayo ni kubwa kuliko changamoto zote kwenye nchi kama yetu hii ambayo Serikali ndiyo ina kauli wapi uuze mazao yako na si mkulima mwenyewe. Pia unazungumzia kumwagilia mazao je unajua kweli gharama za kukuwezesha kumwagilia mazao kweli?! unahitaji water source ambayo ni ya kuaminika, mashine za kusukuma maji na mafuta ya kupamp kila siku kwa siku si chini ya 100 na kuendelea kutokana na aina ya zao na hali ya hewa, matanki ya kutunza maji na pia infrastructure ya umwagiliaji matone ndo ghali sana, kwa uchache hapo mtu anahitaji si chini ya milion thelethini kwa miundo mbinu tu ya umwagiliaji. Ndugu yangu ngoja niachie hapo na kama una busara umwombe radhi mwenzio, Mara nyingi sisi wakulima halisi huwa tunapenda kuwahamasisha wengine waingie kwenye kilimo ili waonje joto ya jiwe. Nampongeza sana mleta mada aliyoandika ndo halisi kabisa, ukiingia kwenye kilimo usiende kichwa kichwa utakufa siku si zako.
 
kwel kabisa, yaani jamaa ni mpumbavu plus
 
Huyu jamaa amekula maharage ya wapi aisee!!
Hasira zako unakuja kumalizia huku .Hii mada ni nzuri tu inaonyesha changamoto katika sekta ya kilimo na jinsi ya kukabiliana nazo sasa wewe unakuja kutukana huku na kumlaumu mleta mada kama wewe ni mjuzi zaidi si ungefungua UZI wako uelimishe watu kuhusu kilimo unasubir watu wafungue uzi uje uwatukane na kuwaponda sii vizuri kabisa alafu pili pili usio ila inakuwashia nini.
 
Gunia la mahindi mikoa ya kusini halijawah kushuka chini ya elfu tisini
Acha matani mkuu , mimi ninavyoandika niko Sumbawanga na mwaka huu tumeuza gunia sh 12, 000 mpaka elfu 9,000 kwa sasa ndo bei imepanda na haijazidi 45,000 kwa bei ya reja reja, Ninalima pia mikoa ya Dodoma kanda ya ziwa na Morogoro. Kwa taarifa yako ni kanda ya ziwa pekee ambapo bei ya mahindi imefika 75,000 na hiyo ni bei ya rejareja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…