Tahadhari kwa wapenzi wa supu ya pweza

Tahadhari kwa wapenzi wa supu ya pweza

Asante kwa kutupa mbinu ya kibiashara tuliokuwa hatujui...

Kuanzia sasa hapa gengeni kwangu hata mchemsho wa maharage natupia kitu cha viagra...

Nani kasema maharage hayaongezi nguvu za kiume....shabashhhh!!!!
Sio mbinu hii ni kumaliza nguvu za kiume za vijana wengi
 
Chunga Sana
Mkuu
Kwanza hongera kwa utafiti huu .
Dunia ina mambo ya ajabu sana.

Sasa ninachojiuliza ni hivi " hii thread ni ya 2015" ila hadi mwaka May, 2016 nilikuja Tanzania bado nilikuta hiyo ndiyo supu kila kijana hadi baadhi ya wanawake wanapendelea sasa hawasomi humu JF platform nyuzi kama hizi!?

Au ndiyo sikio la kufa hali sikii dawa!?.


Tusisahau hili

We need an immediate justice for our daughter Akwilina A. B.

R.I.P Binti yetu Akwilina A. B
Ndoto zako zimezimwa ghafula kama mshumaa uzimwavyo.

Daima tutakukumbuka. Kristo Yesu akuangazie mwangaza wake wa milele. Amina.
 
Hivi karibuni niliamua kufanya biashara ya Pweza hivyo nikaona ni vyema nifanye utafiti wa kina kabla ya kuanza,hii ni biashara nzuri hapa Dar es salaam na mtaji wake sio mkubwa pia inatoa fursa kwa vijana wetu.

Kilichonishtua ni kuwa daktari mmoja alinieleza kuwa Pweza huongeza protein muhimu mwilini na hawana uhusiano na kuongeza Nguvu za kiume wala si kichocheo cha body metabolism.

Hapo nikapata shauku ni kwa nini wateja wa hii kitu hupata Nguvu za ziada za mambo ya kikubwa pindi tu walapo hao pweza au kunywa mchuzi wake?

Jibu lilinistua sana maana hata mie ni mpenzi wa hawa Pweza na hata supu yake. Kumbe wauzaji huwa wananunua dawa ya kuongeza nguvu za kiume Viagra aina ya Sildenafil na kuchemshia Pweza kabla ya kuwakaanga.

Nikafanya uchunguzi kwa vijana kama wanne wanaofanya wanaofanya hii biashara maaeneo ya Ferry na Kariakoo wakathibitisha kuchanganya na Viagra.

Sikuishia hapo nikaenda kwenye Pharmacy moja na kudadisi ambapo Mfamisia mmama mtu mzima alibainisha kuwa ni kweli ana wateja wengi sana wa Viagra hio ambayo ni mahususi kwa kuchanganya na Chakula au Kinywaji.

Aisee nimekoma kula Pweza wa magengeni na sikuwa na hamu ya hio biashara nono. Nawashauri wapenzi wa Sea Foods hasa Pweza wanunue moja kwa moja Sokoni Ferry na waandae nyumbani vinginevyo with time Nguvu za kiume zitaathirika kwa kutumia Viagra bila kujua.

Nafunguka funguka.
Mtoa mada katika utafiti wako huo nimeona una mapungufu mengi sana na kuonekana kama ni uzushi ama ni tafiti yenye hila ya kuharibia watu biashara zao hapa mjini na si kwa ajili ya kusaidia afya ya jamii.
Maswali muhimu:
Je biashara hiyo imeibuka ghafla sana baada ya ujio wa viagra miaka ya 2000 na kabla yake haikuwepo?
Ni wazee wangapi wateja wa hiyo kitu waliokuwa wakitumia tangu enzi kabla ya ujio wa viagra na kuonesha utofauti wa miaka ile na sasa, uliowahoji na kulinganisha majibu yao?
Je ni madaktari wangapi , zaidi ya huyo mmoja uliyesema,uliowahoji ili kuweka majibu yao kwenye mizania iliyosahihi?
Je ni watumiaji wangapi wa viagra uliowahoji ili wakupe nguvu waipatayo kwa vidonge tofauti na mchuzi ama minofu ya huyo samaki nk nk, ili mwisho wa siku uje na conclusion iliyojazwa nyama.
Hili la kukurupuka na utafiti wa kukopi majibu kutoka katika chanzo kimoja, ni uzembe ambao siku moja waweza kukuzalishia migogoro isiyo ya lazima katika jamii.
 
Kama ni kweli basi Dar wataathirika zaidi maana ndio watumiaji wakubwa wa hicho kitoweo
 
Back
Top Bottom