Tahadhari: Kwa watafuta ajira usijaribu kuomba wala kufanya kazi hospitali hizi jijini Mwanza

Mimi nilikua idara ya ukaguzi ndio maana ninajua A,B,C
 
Binafsi nimeeshatibiwa Uhuru hospital (na hawara yangu alitibiwa pale) sijapata shida yoyote matibabu yangu yalienda vizuri kabisa,nyie watafuta ajira mtajiju mkiondoka watakuja wengine watatupa huduma murua kabisa

Hapa Aljumaa mjini kati napo nilishatibiwa vizuri kabisa ,ila njaa zenu mnaojiita madokta ndo mnaponda ila wapo vijana wazalendo watatutibu acha kelele na njaa zako Mtoa mada boya wee
 
Hamna uzalendo mbele ya njaa, Mbunye na wazazi
 
Hamna uzalendo mbele ya njaa, Mbunye na wazazi
Kila mtu anapitia changamoto kwenye sehemu ya kutoa huduma kwa jamii,so jamaa anatakiwa ajue anatoa huduma kwa jamii so atulize matako,kama akiona usumbufu afungue hospital yake na si kuanza kuleta majungu huku mtandaoni na kuleta hofu kwa wananchi wanaopata huduma kwenye hospital hizo kwa njaa na umaskini wake
 
Kufa kibudu kwa uchumi wa Tanzania kumesababisha yote haya
 
Kuna uwezekano mkubwa kwamba hao wamiliki wanapambana na "mlima" wa marejesho.
 
Katika hizo hospital ulizotaja moja anamiliki yule mzee mmilikiwa wa shule ya sokoni na nyingine ni ile anayomiliki yule kijana mpenda sifa kibaraka wa Redio mawingu, asilimia 100 ni wababaishaji kweli kauli yao kubwa utasikia "Tutakukata mshahara wako"
 
Uko sahihi......
Wababaishaji mno,mamlaka nazo zipo tu.
 
Wewe usione dokta au nesi anakupa huduma nzuri ukafikiri mambo yako sawa,binadamu tuna matatizo mengi sana....mtu hajalipwa mshahara miezi miwili hawezi kufanya kazi kwa uweledi....watu wanaumia moyoni sema ndio basi hawana namna,hii ni hatari sana ndio ile unachomwa sindano ya uti wakati unaumwa maleria si busara kufurahia huu ujinga.
 
We unajua hela wanazoingiza huko kwenye hospitali ya private....faida wanapata kubwa sana...sema ni roho za kishetani za kutesa watu kwa kuwanyima haki zao....hakuna cha uchumi wala nini,wagonjwa wanaotibiwa hulipia pesa sasa hizo pesa zinaenda wapi?
 
Ukiona kila sehemu unayoenda inanuka kinyesi, basi jikague kwenye boxer inawezekana umejinyea bila taharifa. Ungekua na akili ungejiuliza kwa nn hospital zaidi ya 10 ziwe na shida inayofanana? Changamoto ni khali ya uchumi ni mbovu kwa wateja not managements.
Mimi nilikua idara ya ukaguzi ndio maana ninajua A,B,C
 
Na huto tuhospitali twa mwanza, wamiliki ni wale wale, ukikosana nao sehemu moja, ukienda kwingine hupati.., kwenye udahili unakutana na wale wale
 
Mkuu, Acha Uongo. Nimefanya Kazi na nina fanya kazi na Uhuru hospital kwa Miaka 5 sahizi. Sijawahi pata Shida ya Mshahara wala Mkataba. Hadi Tanzanite hospital imefunguliwa Bado nipo Na Uhuru Hospital na Tanzanite Hospital Sijapata Hizo Shida Ulizozisema Kwa Miaka 5 yote, Na Wala sijawahi kufikiria kuja Kuacha Kazi Uhuru Hospital Unless Nijiajiri.

Mwaka 2019, Nilienda Nje Ya Tanzania Kusoma, Uhuru hospital Waliendelea kunilipa Mshahara Bila Kuchelewa, Kwa Muda wote nilio Kuwa Nasoma, Na Bila Kunikata Hata Tsh.10, Hadi Nilipo Rudi 2020 nikaendelea nao na kazi.

Sahizi Tena Nimerudi Shule. Uhuru hospital Bado Wananilipa Mshahara Bila Shida Yoyote ile. So Acha Kuwadanganya Watu.

Changamoto niliyo Iona Kwa Miaka 5 yangu ya Kufanya Kazi Kwenye hii hospital Binafsi ni Bad Altitude za WAAJIRIWA. Waajiriwa Wengi Hawana Nidhamu Ya Kazi, Wanachukulia Taasisi Binafsi Hasa Hospital Kama Ni Sehemu Ya KIJIWE. Hii ndio Changamoto kubwa. Mfanyakazi hana Nidhamu ya Kazi, Hadhamini Ajira yake, Haheshimu Kituo Kilichompa Ajira wala Mwajiri wake. Unategema Mwajiri Akuheshimu na Wewe?

Tena Nyie Ndio mnao Wadanganya watu, Lakini Kwa Kijana Anayekua Kikazi, Uwezo binafsi uwezo wa kibiashara, Uhuru Hospital Ni sehemu sahihi ya Kufanya Kazi Kama Ukibahatika kupata Ajira. Nisehemu itakayo kupa nafasi ya kukua.

Mkuu Kudanganya watu na wewe ni Mtumishi wa Serikali Hizi Ndio Nidhamu Mbovu na mbaya Ambazo Wafanyakazi wengi wanazo.

Kifupi, UHURU HOSPITAL kama Huna NIDHAMU, Huna INTERGRITY basi Wewe hapakufai kufanya kazi.

Over
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…