Mkuu private nyingi kwanini hamtoi mkataba wa ajira?
Huwa mnafanya hivyo kwa lengo lakuwatumikisha watu bila ujira!
Umetumia nguvu nyingi kutetea kwa sababu wewe una share hivyo pesa unapata chapu sio?
Kwa vijana mnao wajiri hamuwalipi au mnawalipa kidogo kidogo alfu maneno ya tuvumiliane yanakuwa mengi.
Maoni yangu
Kunifanyisha kazi mwisho wasiku unaleta janjajanja usitegemee heshima itafata mkondo..ukicheza nakuzaba vibao[emoji23][emoji23]
Mkuu, Kwanza Kabisa Mtu yeyote Yule Anaye Ajiriwa Anajua Wajibu na Haki Yake zake, ndio maana Serikali Ilitoa, Sheria za Ajira na Mahusiano Kazini, Ikaweza na Haki na Wajibu wa Muajiriwa na Muajiri. Kukiwa na Kipengele cha Umuhimu wa mkataba Wa kazi. Kama Umeenda kuomba Kazi ukaanza Kufanya Bila Mkataba au kuomba Mkataba Unataka Kusema Muajiri ndio Ana shida?, wewe Hadi unaanza Kazi Hujui Umuhimu Wa Mkataba? Na Kwanini Ukubali kuanza kufanya Kazi Bila Mkataba?, Japo sio Kwamba Private zote hazitoi mikataba Hapana, Private nyingi sanaa Zinatoa Mikataba.
Na Wajibu wako Ni Mmoja Tuu, Kabla Hujaanza Kazi kaa chini Na Muajiri msign Mkataba. Ukianza kazi Bila Mkataba Hayo ni Mahusiano Yako na Maelewano yako kati ya Wewe Na Muajiri wako, Na Chochote kikitokea usitafute wa kumtupia Lawama Kwasababu ulikuwa unajua Haki zako na Wajibu Wako.
Ukisema Private Masilahi ni Madogo, Umekubaliana Nini Na Muajiri Wako, Makubaliano Yenu mmeyaweka kwenye Maandishi? Usipo fanya hivi kwasababu ya Uhitaji wa kazi au umekaa sana nyumbani au soko la Ajira ni Gumu Unajitafutia matatizo wewe na Sio Muajiri. Hii ni Muhimu sanaaa Watu wanao hangaika na Ajira kuelewa badala ya kuja kumtupia mtu lawama.
Lakini, Kazini Tunaendeshwa sanaaa Na Mahusiano. Ndio maana Serikali Ileta Kipengere cha Mahusiano Kazini, Ni kipengele muhimu sanaaa kinaenda zaidi ya Mikataba… Mfano Sheria Ya Ajira kazini inatambua Ili upate ruhusa ya Kwenda Msibani ni Lazima Aliye fariki awe mmoja ya wale walio tajwa kwenye Mkataba naamanisha Neutral Family, Lakini Mtu unafiwa na Mjomba Wa Mama Yako Sijui, Kwakutambua Umuhimu wa Mahusiano kazini Muajiri anakupa Ruhusa ya wewe kwenda Kuhudhuria mazishi, Japo Mkataba na Sheria Hazimlazimishi kufanya hivyo. Hivi Vitu ni lazima Waajiriwa Waelewee badala ya kwenda Kuwatupia Lawama Waajiri kama Mleta mada Alivyofanya.
Sheria zipo Wazi, Usipolipwa kwa muda gani unaenda CMA kufungua Mashtaka. Lakini Mahusiano Bado yanaenda Nje ya Mkataba. Kuna Kipindi muajiri Hupitia Changamoto za Kifedha, Anawasiliana Na Wafanyakzi kuwa Mshahara utachelewa Kwa Sababu 1,2,3 Wewe kama Muajiriwa Uta Reason Je Hizi sababu nazopewa ni Kweli au hazina Mashiko. Utafanya maamuzi. Lakini isiwe wewe Hutimizi Wajibu wako Lakini unataka Muajiri Akutimizie wajibu wake, Hapana. Bado serikali ilienda mbali Ikaleta Haki na Wajibu wafanyakazi na Muajiri, Kwamba Kila Haki ina Wajibu na Kila Wajibu una Haki.
Kuendelea Kuvilalamikia Hivi Vituo Kwenye JF haiwezi kuwa suruhu kama Wanaoajiriwa hawata elewa Haya. Nenda Mahakamani Kesi za madai na zingine zote huanzia Kwenye Mazungumzo mahakama hutoa muda wa nyie kujadiliana na kuona kama kuna umuhimu wa Kuendelea na Kesi au ifutwe, kesi nyingi zinaishia kwenye mazungumzo na Maelewano kwasababu kuna mtu hakuwa anatambua wajibu na haki zake.
Mleta Maada Amekuja na Mlengo wa Kusema vituo Ambavyo yeye havipendi na hana Ukweli Wa anayo yasema. Hivyo vituo alivyo vitaja Naona watu wakifanya kazi na kufurahia, Na Kuna Vitu hajavitaja watu wanalalamika Vile vile lakini Ukweli wake ni Upi?
Masuala Ya Ajira huwezi Kumuamlia mtu au kumsemea. Kuna waalimu wangapi wanaidai Serikali? Wafanyakazi Wangapi Wanaidai Serikali? Ulisha sikia mtu anasema Usiombe ajira serikalini kwasababu hawalipi?