Tahadhari kwa watanzania kuhusu kikundi cha Siib na viashiria vya utapeli

Tahadhari kwa watanzania kuhusu kikundi cha Siib na viashiria vya utapeli

Mudawote

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2013
Posts
11,612
Reaction score
16,189
Great Thinkers,

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na taarifa za kuwapo kwa kikundi kinachojiita SIIB kinachodai kuhusika na mradi wa Pi Network hapa Tanzania. Napenda kuwatahadharisha Watanzania wote—hasa wastaafu—kuwa makini sana, kwani kikundi hiki hakijasajiliwa kisheria hapa Tanzania na kinatoa dalili zote za kuwa ni matapeli wa kisasa.

Viashiria vya Utapeli wa SIIB:
  1. Ahadi za kuwajengea watu nyumba bila maelezo ya kina wala uthibitisho wa mchakato wa fedha.
  2. Kununulia watu magari kwa madai ya zawadi au fadhila kupitia ushiriki wao kwenye SIIB.
  3. Kudai kuwa kampuni yao imesajiliwa kimataifa, lakini bila kuonesha ushahidi wa usajili huo popote duniani.
  4. Kutoa fomu za kujisajili kwa wananchi, hasa wastaafu, kwa lengo la kuwalaghai wachangie fedha au kujiunga kwa matarajio ya faida zisizo halisi.
Wana SIIB wameanza kutumia jina la Pi Network, mradi halali wa kimataifa wa blockchain, kama kichaka cha utapeli wao. Pi Network yenyewe haijaanzisha kampuni yoyote rasmi inayoitwa SIIB hapa nchini Tanzania. Kwa hiyo matumizi ya jina la Pi ni ya kupotosha na ni mbinu ya kupata imani ya watu kwa hila.

Ujumbe kwa Wastaafu na Umma kwa Ujumla:

Wastaafu na wananchi kwa ujumla, tafadhali msikubali kushawishiwa kujiunga au kuchangia fedha kwenye SIIB. Hii ni njia ya wazi ya kuporwa akiba zenu na kulaghaiwa kupitia matumaini hewa.

Chukua Hatua:
  • Usikubali kutoa taarifa zako binafsi au za kifedha kwa kikundi hiki.
  • Ripoti kikundi hiki kwa mamlaka husika ikiwemo TAKUKURU, TCRA, na Jeshi la Polisi.
  • Uliza kabla ya kujiunga: je, kampuni hiyo imesajiliwa BRELA? Je, ina leseni ya kufanya shughuli zake kutoka mamlaka za Tanzania?
Hitimisho

Wakati tunasherehekea maendeleo ya teknolojia kama blockchain na miradi kama Pi Network, tusiruhusu matapeli kutumia maendeleo hayo kutuhadaa na kutuibia. SIIB si kampuni halali na si sehemu ya mradi wa Pi Network.

“Wizi wa kisaikolojia unafanyika pale ambapo matumaini huuzwa kwa maneno, na fedha hupokonywa kwa udanganyifu.”

TAHADHARINI. WAJIBIKA. KAA MACHO.

Great Thinkers, tuendelee kutoa elimu na kuwalinda wananchi dhidi ya huu utapeli wa kisasa.
 
Wabongo kwa dezo pamoja na onyo ila bado wapo watakaojiunga
 
waTz mpaka walizwe kwanza ndiyo akili zinakaa sawa,hata ukitoa tahadhari bado wataenda kutest,wabongo ni kama mbuzi,akikurupushwa akikimbia umbali fulani lazima arudi kuchungulia kinachomfukuza
 
Hamna KAZI ngumu Kama kumshauri mtu alie kwenye mchakato wa kutapeliwa😂
Hapo ni sawa uwashauri wafuasi na pale Kawe kwamba jamaa huyo anawapiga kamba katu kamwe hawatokuamini,
 
Hamna KAZI ngumu Kama kumshauri mtu alie kwenye mchakato wa kutapeliwa😂
Sawa na vibarua vya kumshauri Ke aliyempenda sana Me, mtu aliyeathirika kiakili kujichua au kubeti waachane na hizo ishu.............................!?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Back
Top Bottom