TAHADHARI: Mboga za majani wanazokula wakazi wa Dar ni sumu tupu

TAHADHARI: Mboga za majani wanazokula wakazi wa Dar ni sumu tupu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Nimeileta hii mada huku kwa makusudi kwakuwa inahusika na mapishi lakini vile vile na afya zetu kwakuwa mapishi na afya haviachani

Sehemu kubwa ya mboga za Darisalama zinatoka mabonde ya Mto Msimbazi, Mandela road bonde lililoko kituo cha garage, Jangwani, Kigogo sambusa na maeneo ya Tandale na kwingineko
maji yanayopita kwenye mabonde haya ni machafu, yenye kemikali toka viwandani, yenye vinyesi toka vyooni nk ndio hayo hayo yanayonyweshea mbogamboga hizi tangu kuchipua hadi kukomaa.

Kwa vyovyote vile, maji haya yakipimwa ni wazi yatakutwa na kiwango kikubwa cha sumu mbalimbali zinazosababisha magonjwa kansa na ngozi.

Uchafu tunaoutupa kwenye mito ipitayo kwenye haya mabonde kama betri za simu na magari material za friji mbovu, computer mbovu nk nk vyote hivi vimebeba kemikali zenye sumu kali.

Tusipochukua tahadhari tutaishia kuongeza vyumba pale Ocean road kwenye ile hospital ya kansa
 
Hata tunaokaa nje kdogo ya mji habari ni ile ile,zinaoteshwa na madawa mengi ,Kwetu tunanunua mafungu 3 dailyy..Acha tu yani,
 
Kwa kweli hali hii ni balaa. Wizara na wanaharakati wanaohusika na mazingira wanatakiwa kulivalia njuga suala la kunajisi vianzio vya maji jijini Dar.
 
Kuna mboga nyingine zinatoka kando ya mto kimara mbezi. Pengine hizo zinaweza kuwa salama kidogo. Tatizo ni kuwa sijasikia chombo husika kikifanyia uchunguzi mboga zinazouzwa katika masoko ya Dsm.
 
Nimeileta hii mada huku kwa makusudi kwakuwa inahusika na mapishi lakini vile vile na afya zetu kwakuwa mapishi na afya haviachani

Sehemu kubwa ya mboga za Darisalama zinatoka mabonde ya mto msimbazi ,Mandela road bonde lililoko kituo cha garage ,jangwani kigogo sambusa na maeneo ya Tandale na kwingineko
maji yanayopita kwenye mabonde haya ni machafu ,yenye kemikali toka viwandani ,yenye vinyesi toka vyooni nk ndio hayo hayo yanayonyweshea mbogamboga hizi tangu kuchipua hadi kukomaa
kwa vyovyote vile maji haya yakipimwa ni wazi yatakutwa na kiwango kikubwa cha sumu mbali mbali zinazosababisha magonjwa kansa na ngozi
uchafu tunaoutupa kwenye mito ipitayo kwenye haya mabonde kama betri za z simu na magari material za friji mbovu computer mbovu nk nk vyote hivi vimebeba kemikali zenye sumu kali
Tusipochukua tahadhari tutaishia kuongeza vyumba pale Ocean road kwenye ile hospital ya kansa
Ahsante sana bossman kwa hii taarifa. Itabidi niwe naagizia mboga kutoka Bagamoyo sasa
 
Unanikumbusha za pale changombe, jamaa wanachota maji machafu toka ule mtaro wa maji machafu ya kiwanda cha serengeti
 
Umesema kweli Mkuu, Dar es salaam kwa chakula suala la usafi ni zero, kuanzia feri, mabucha yote masoko ya nafaka, ndizi na matunda etc. Hatuugui kwa neema za mungu.

Hatuna mabwana afya, tulionao ni zaidi ya waganga njaa na waumuni wakubwa wa Tumbo Street.
 
Kuna mtafiti mmoja wa Chemistry (Dr Kishimba, University of Dar Salaam); mnamo miaka ya 1990 alifanya utafiti na kuandika ripoti kuwa Mto Msimbazi una sumu nyingi ikiwemo heavy metals, na hivyo mradi wa CCM wa SUKITA uliokuwa unatumia maji ya mto Msimbazi wa kufuga samaki, kulima mchicha, kufuga nguruwe nk ni batili kwani unahatarisha afya za walaji. Alipata msuko suko, na sijui ile ripoti iliishia wapi. Kwa hiyo mtoa mada anachokisema kinafahamika tangu miaka ya 1990, Majanga!!!
 
Mleta uxi yuko sahihi kuna studu nyingine imefanyika kama miaka 2 iliyopita na Dr. RIZIKI SHEMDOE wa Chuo kikuu cha Ardhi kiukweli hali ni mbaya sana kwa walaji wa mbogamboga hapa Dar.
 
Hivyo ule utamaduni wa kupanda mboga zako uwani au nje ya nyumba umeishia wapi? Manake mie nakumbuka wakati tunakua tulikua tunanunua mboga mara chache saaana. Tulikua tumepanda matembele, mboga za maboga, kisamvu nk. Lakini nyumba za siku hizi hata vimche vichache vya mboga hamna, ni mismenti kila mahali. Yaani naitamani ile hali ya zamani. Ndio maana watu utakuta wanakula mboga za majani nk, lakini bado wanakufa na kansa. Yaani siku hizi kila nyumba kuna mtu ambaye ana kansa au kafa na kansa unamjua. tubadilike jamani, tujali afya zetu.
 
pale n balaa, tena maj yananuka
v baya na bado wanachota

hayo maji yatokayo serengeti hamlewi kweli??
utakuta mtu anakula mchicha afu analewa.
 
mkuu hii habari ya mboga za majani inatisha..

kuna wengine wanalimia bonde fulani hapa la garage kama ukiwa unaelekea ubungo kabla hujafikia kituo cha external..

hilo bonde ni zuri sana kwa kilimo, hiyo haipingiki... ardhi yake ni nzuri sana, ina utambarare na ina rutuba nyingi tu kwa shughuli za kilimo..

tatizo lake linakuja sasa kwenye shughuli nzima za umwagiliaji.. wakulima wanatumia maji machafu sana yanayotokea kwenye ule mto ulioko kando kando mwa bonde..

maji yake yamechafuliwa sana na wenyeji wanaozunguka mto kwa kuelekezea vyoo vyao na kutapishia vinyesi humo mtoni!
hivyo mtambue kuwa mnakula end products za watu...

kuna kiwanda cha sabuni kiko karibu sana na hilo bonde, hapo tu kituo cha garage, basi hao mabomba ya maji machafu nayo yameelekezewa humo.. mboga ziko full kemikali!

mto ule hautoki karibu...wenyeji wa mitaa yote ya mto unakoanzia kumbukeni nao wana uchafuzi wao ikiwemo kufulia nguo mtoni, kuoga, wengine wanaosha pikipiki zao, magari nk..

mwisho wa siku.. mboga za majani zinakuzwa kwa hayo maji! life expectancy lazima ishuke tu kwa lazima!

kuna mazungumzo mafupi tu nilishafanya na hawa wakulima na wenyeji wa eneo hili

wenyeji wanadai kuwa wao huwa hawatumii mboga za bonde hili... kitu ambacho sikuamini sana, lakini kwa vile niko kwenye utafiti, inabidi ukubali ili upate data...

wakulima wanadai kwamba hawana jinsi, wafanye nini wakati hiyo ndiyo ajira yao? serikali haiwajali, maji ni machafu ndio, kwa hiyo waende wapi ili kujiokoa na ukosefu wa ajira?

wafanyabiashara nao hawakukosa lao la kusema... wao wanadai kuwa wenyeji hawanunui hizo mboga za bonde hilo! hivyo wao huzisafirisha na kwenda kuziuzia mbali kabisa na mitaa hiyo!
lakini tatizo halijamalizwa bado kwa sababu, ukiuza mbali, na yule wa mbali akaja kuuza kwako for the same product, bado hamjaua kitu...!

poor city planning ndio tatizo kuu la dar es salaam...!

kwa tatizo la mboga kama hili, bidhaa zingeweza kutoka hata miko ya karibu...!
 
nimeupenda uchambuzi wako kwa njia hii JF is very construstive
 
Back
Top Bottom