Hute
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,537
- 6,472
kuna mtu mmoja hapa hapa Dar es saaam alioa kabisa, akazaa na mtoto mmoja na mwanamke asomfahamu...kuna siku moja yule mkewe akamwambia, leo nataka uwahi kurudi nyumbani mapema sana, kwasababu nataka kuja kulala kikwetu...jioni ilipofika, yule mwanamke akamwambia sasa ni muda wa mimi kulala kikwetu...mwanaume akawa anacheka tu akifikiri anamtania labda ni manjonjo ya mahaba...ebwanaeee, akastukia mwanamke ameaa kichwa chini miguu juuu inaeekea darini, ameshikilia vidole tu kwa chini na haanguki wala nini...bifu la kuchanganyikiwa na kuzirai lilipoisha, ndo ilikuwa mwisho wa ndoa hiyo na mwanzo wa kupotea/kuyeyuka kwa hilo jini mtu pamoja na mtoto wake ambaye lilimuua kwa kumchinja kabisa...akaondoka naye kwenda kuzimu...Majini pia yapo kwa ajili ya wanawake wapenda pesa na kujitongozesha kwa wanaume wazuri na wenye pesa,hivyo nanyi wanawake muwe makini.
pale magomeni kuna majini mengi sana, wanavaa ushungi mweusi ni wazuri sana, na wanavutia..wachawi wengi wa kiislam huwa wanayaoa, yanawajengea na nyumba, wanaishi nayo...shehe wa msikiti, au imam au mtu yeyote aliyebobea kwenye elimu ya kiisam, lazima aoe jini, achiia wake wengine wengi...hii kitu inajulikana kabisa...
