DOKEZO Tahadhari: Mtu Anayejitambulisha Kama Afisa wa Ajira TAMISEMI anawatapeli wanaotafuta Ajira

DOKEZO Tahadhari: Mtu Anayejitambulisha Kama Afisa wa Ajira TAMISEMI anawatapeli wanaotafuta Ajira

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mmoja wa watu waliowahi kupigiwa simu na mtu anayejitambulisha kwa jina la Joseph Kichele, akidai anatokea Ofisi ya Ajira ya TAMISEMI jijini Dodoma. Kutokana na uzoefu wangu na taarifa nilizopata kutoka kwa wengine, naomba mamlaka husika zifuatilie suala hili kwa haraka ili kuwalinda wananchi.

Kwa mujibu wa maelezo yanayotolewa, mtu huyo amekuwa akiwasiliana na Makatibu wa Wilaya pamoja na Wahasibu, akidai kuwa kuna nafasi za wahasibu wa mikataba katika hospitali na vituo vya afya, na kwamba waombaji wanaweza kuajiriwa moja kwa moja katika wilaya husika.

Baada ya kupata taarifa binafsi za waombaji, huwapigia simu na kufanya mahojiano mafupi. Baadaye huwaeleza kuwa hawajakidhi baadhi ya vigezo vya ajira, lakini anaweza kuwasaidia kupata nafasi hizo endapo watatoa fedha.

Kwa nilivyoshuhudia, huanza kwa kudai kiasi cha Shilingi milioni 3. Ukimweleza kuwa huna uwezo wa kutoa kiasi hicho, hupunguza na kuomba kati ya Shilingi 500,000 hadi 800,000, huku akidai salio litalipwa baadaye ili kukamilisha mchakato wa ajira.

Inaelezwa kuwa tayari watu kadhaa wameathirika kwa utaratibu huo na kupoteza fedha wakiamini wanasaidiwa kupata ajira.

Namba inayotumiwa katika mawasiliano hayo ni: 0696 355 901

Iwapo taarifa hizi ni sahihi, tunaomba mamlaka husika, hususan President's Office – Regional Administration and Local Government (TAMISEMI) pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama, kufanya uchunguzi wa kina na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu yeyote anayewatumia wananchi kwa njia ya udanganyifu.

Pia, watafuta ajira wanapaswa kuwa waangalifu na kutambua kuwa ajira za serikali hutangazwa na kuendeshwa kupitia taratibu rasmi, na hakuna mtumishi wa umma anayepaswa kudai fedha ili kumpatia mtu ajira.
 
Back
Top Bottom