doctor mwanafunzi
Member
- Jun 16, 2024
- 45
- 56
Ndugu zangu nawashauri kuwa makini sana na kupenda kwenda hospitali kwanza kama unashida ya kiafya ambayo unahisi ukianzia duka la dawa hutopata matibabu sahihi. Hiyo picha ni picha ya majibu ya kipimo cha sphymomanometer kinachutumika kupima presha ya damu. Hapo kwenye picha chini ni majibu ya mtu fulani mzee( jina limefichwa kwa kuzingatia haki ya mgonjwa ya usiri wa majibu yake). Kabla hajaelekea hospitali alikuwa anajisikia vibaya na kuamua kwenda duka la dawa muhimu akiwa na dalili " X " ambazo moja kwa moja kama angeonana na mtaalamu wa afya basi alipaswa kumpima presha ya damu. Ila cha kusikitisha na kuumiza moyo muuza duka la dawa hilo alimpatia dawa hizo hapo kwenye picha kitaalamu zinaitwa prednisolone kwa kumshauri kuwa zitamsaidia. Dawa hizo zipo kwenye kundi la madawa ambayo hayahusiani kabisa na kutibu presha. Lakin bibi huyo ametumia dawa hzo kwa wiki nzima mpaka alipoamua kufika hospitali na kujieleza nakusema kuwa alipewa dawa hizo zimsaidie kwa tatizo lake hilo kitu ambacho ni uongo. Prednisolone ni dawa kutoka kundi la corticosteroids ambayo hutumika kama anti inflammatory au anti allergy. Bibi huyo alipimwa presha na kukutwa ipo juu kama inavyoonekana pichani. Nlijaribu kufatilia ni duka la dawa gani lakini kwa sababu ya bibi kutokuwa na kumbukumbu vizuri zoezi likawa gumu sana. Kwa sasa bibi huyo yupo kwenye matibabu ya awali ya presha ambayo ni kumpima presha katika nyakati tofauti tatu huku akiboresha mwenendo wa maisha ikiwemo kutotumia chumvi kwa wingi n.k kwanza kabla hajaanza dawa.
USHAURI KWA UMMA
Nenda hospitali kama unadalili ambazo zinaulazima kwenda hospitali au ulitumia dawa na haikukusaidia
USHAURI KWA SERIKALI
wataalamu wa dawa hasa kwenye maduka madogo madogo ya dawa wapewe semina mara kwa mara kila baada ya muda fulani maalumu kama ilivyo kwa madaktari ili kuepusha matibabu yasiyosahihi kwa wagonjwa
USHAURI KWA WATOA DAWA ( PHARMACEUTICAL TECHNICHIANS)
nivyema kumshauri mtu akamwone daktari kwanza kama dalili alizokueleza huzielewielewi kuliko kujali tu uingize fedha.