Tahadhari na ushauri

Tahadhari na ushauri

Joined
Jun 16, 2024
Posts
45
Reaction score
56
Ndugu zangu nawashauri kuwa makini sana na kupenda kwenda hospitali kwanza kama unashida ya kiafya ambayo unahisi ukianzia duka la dawa hutopata matibabu sahihi. Hiyo picha ni picha ya majibu ya kipimo cha sphymomanometer kinachutumika kupima presha ya damu. Hapo kwenye picha chini ni majibu ya mtu fulani mzee( jina limefichwa kwa kuzingatia haki ya mgonjwa ya usiri wa majibu yake). Kabla hajaelekea hospitali alikuwa anajisikia vibaya na kuamua kwenda duka la dawa muhimu akiwa na dalili " X " ambazo moja kwa moja kama angeonana na mtaalamu wa afya basi alipaswa kumpima presha ya damu. Ila cha kusikitisha na kuumiza moyo muuza duka la dawa hilo alimpatia dawa hizo hapo kwenye picha kitaalamu zinaitwa prednisolone kwa kumshauri kuwa zitamsaidia. Dawa hizo zipo kwenye kundi la madawa ambayo hayahusiani kabisa na kutibu presha. Lakin bibi huyo ametumia dawa hzo kwa wiki nzima mpaka alipoamua kufika hospitali na kujieleza nakusema kuwa alipewa dawa hizo zimsaidie kwa tatizo lake hilo kitu ambacho ni uongo. Prednisolone ni dawa kutoka kundi la corticosteroids ambayo hutumika kama anti inflammatory au anti allergy. Bibi huyo alipimwa presha na kukutwa ipo juu kama inavyoonekana pichani. Nlijaribu kufatilia ni duka la dawa gani lakini kwa sababu ya bibi kutokuwa na kumbukumbu vizuri zoezi likawa gumu sana. Kwa sasa bibi huyo yupo kwenye matibabu ya awali ya presha ambayo ni kumpima presha katika nyakati tofauti tatu huku akiboresha mwenendo wa maisha ikiwemo kutotumia chumvi kwa wingi n.k kwanza kabla hajaanza dawa.

USHAURI KWA UMMA
Nenda hospitali kama unadalili ambazo zinaulazima kwenda hospitali au ulitumia dawa na haikukusaidia

USHAURI KWA SERIKALI
wataalamu wa dawa hasa kwenye maduka madogo madogo ya dawa wapewe semina mara kwa mara kila baada ya muda fulani maalumu kama ilivyo kwa madaktari ili kuepusha matibabu yasiyosahihi kwa wagonjwa

USHAURI KWA WATOA DAWA ( PHARMACEUTICAL TECHNICHIANS)
nivyema kumshauri mtu akamwone daktari kwanza kama dalili alizokueleza huzielewielewi kuliko kujali tu uingize fedha.
 
Attachments

  • 20250122_090642.jpg
    20250122_090642.jpg
    295.3 KB · Views: 2
Unaandika utafikiria umeshaithirika na overdose tayari ya dawa ulizopewa
🤣🤣
 
Mnafikiri watu hawapendi kwenda hospitalini.
Unakuta mtu anajibiwa hovyo
huduma zinachukua muda mrefu
halafu wahudumu wanafanya kazi like they don't care!
ile dhana ya udaktari kuwa wito imegeuka imekuwa fito!, hivyo nikucharaza tu..
pia serikali ijali watu wake kwenye maswala ya afya angalau gharama zipunguzwe!.
 
Watanzania sio kama hatutaki kwenda hospital tatizo zile foleni ndio zinatoa mzuka. Yaani nafika hospital asubuhi natoka jioni utasema na mimi mfanyakazi wa hio hospital🤣🤣

Halafu kuna madaktari wana matusi na misonyo kama ndio dozi ya kwanza maninazao😂
 
Ndugu zangu nawashauri kuwa makini sana na kupenda kwenda hospitali kwanza kama unashida ya kiafya ambayo unahisi ukianzia duka la dawa hutopata matibabu sahihi. Hiyo picha ni picha ya majibu ya kipimo cha sphymomanometer kinachutumika kupima presha ya damu. Hapo kwenye picha chini ni majibu ya mtu fulani mzee jina limefichwa kwa kuzingatia haki ya mgonjwa ya usiri wa majibu yake. Kabla ahajelekea hospitali alikuwa anajisikia vibaya na kuamua kwenda duka la dawa muhimu akiwa na dalili " X " ambazo moja kwa moja kama angeonana na mtaalamu wa afya basi alipaswa kumpima presha ya damu. Ila cha kusikitisha na kuumiza moyo muuza duka la dawa hilo alimpatia dawa hizo hapo kwenye picha kitaalamu zinaitwa prednisolone kwa kumshauri kuwa zitamsaidia zipo kwenye kundi la madawa ambayo hayahusiani kabisa na kutibu presha. Lakin bibi huyo ametumia dawa hzo kwa wiki nzima mpaka alipoamua kufika hospitali na kujieleza nakusema kuwa alipewa dawa hizo zimsaidie kwa tatizo lake hilo kitu ambacho ni uongo. Prednisolone ni dawa kutoka kundi la corticosteroids ambayo hutumika kama anti inflammatory au anti allergy. Bibi huyo alipimwa presha na kukutwa ipo juu kama inavyoonekana pichani. Nlijaribu kufatilia ni duka la dawa gani lakini kwa sababu ya bibi kutokuwa na kumbukumbu vizuri zoezi likawa gumu sana. Kwa sasa bibi huyo yupo kwenye matibabu ya awali ya presha ambayo ni kumpima presha katika nyakati tofauti tatu huku akiboresha mwenendo wa maisha ikiwemo kutotumia chumvi kwa wingi n.k kwanza kabla hajaanza dawa.

USHAURI KWA UMMA
Nenda hospitali kama unadalili ambazo zinaulazima kwenda hospitali au ulitumia dawa na haikukusaidia

USHAURI KWA SERIKALI
wataalamu wa dawa hasa kwenye maduka madogo madogo ya dawa wapewe semina mara kwa mara kila baada ya muda fulani maalumu kama ilivyo kwa madaktari ili kuepusha matibabu yasiyosahihi kwa wagonjwa

USHAURI KWA WATOA DAWA ( PHARMACEUTICAL TECHNICHIANS)
nivyema kumshauri mtu akamwone daktari kwanza kama dalili alizokueleza huzielewielewi kuliko kujali tu uingize fedha.
Kimsingi Hospitali nyingi sana za Tanzania hazina mvuto, customer care ni mbaya sana. Hazivutii kamwe.
 
niko na pharmacy yangu moja io,,hata niumwe vipi pale hua nauhakika napona,,niliumwa nkazunguka hospital kunipiga hela na sikupona nilikuja kuponea kwenye io pharmacy kwa dawa ya 1300 tu.
 
Kuna saa hospital panachosha unajieleza weeee dokta anaandika vipimo malaria,choo ndogo na kubwa amemaliza. Ukisema unaumwa na kifua na ngozi hivi vile anakwambia aah nimeshaandika vipimo subiri majibu. Majibu yakija paap panado mseto , azuma
 
niko na pharmacy yangu moja io,,hata niumwe vipi pale hua nauhakika napona,,niliumwa nkazunguka hospital kunipiga hela na sikupona nilikuja kuponea kwenye io pharmacy kwa dawa ya 1300 tu.
Mh bei za azuma izo [emoji1]
 
Mnafikiri watu hawapendi kwenda hospitalini.
Unakuta mtu anajibiwa hovyo
huduma zinachukua muda mrefu
halafu wahudumu wanafanya kazi like they don't care!
ile dhana ya udaktari kuwa wito imegeuka imekuwa fito!, hivyo nikucharaza tu..
pia serikali ijali watu wake kwenye maswala ya afya angalau gharama zipunguzwe!.
Lakini hospitali zipo nyingi tu zenye huduma bora na zinazohudumia kwa uharaka kama hujaridhika na kituo fulani nivyema ukajaribu kituo kingine
 
Ndugu zangu nawashauri kuwa makini sana na kupenda kwenda hospitali kwanza kama unashida ya kiafya ambayo unahisi ukianzia duka la dawa hutopata matibabu sahihi. Hiyo picha ni picha ya majibu ya kipimo cha sphymomanometer kinachutumika kupima presha ya damu. Hapo kwenye picha chini ni majibu ya mtu fulani mzee( jina limefichwa kwa kuzingatia haki ya mgonjwa ya usiri wa majibu yake). Kabla hajaelekea hospitali alikuwa anajisikia vibaya na kuamua kwenda duka la dawa muhimu akiwa na dalili " X " ambazo moja kwa moja kama angeonana na mtaalamu wa afya basi alipaswa kumpima presha ya damu. Ila cha kusikitisha na kuumiza moyo muuza duka la dawa hilo alimpatia dawa hizo hapo kwenye picha kitaalamu zinaitwa prednisolone kwa kumshauri kuwa zitamsaidia. Dawa hizo zipo kwenye kundi la madawa ambayo hayahusiani kabisa na kutibu presha. Lakin bibi huyo ametumia dawa hzo kwa wiki nzima mpaka alipoamua kufika hospitali na kujieleza nakusema kuwa alipewa dawa hizo zimsaidie kwa tatizo lake hilo kitu ambacho ni uongo. Prednisolone ni dawa kutoka kundi la corticosteroids ambayo hutumika kama anti inflammatory au anti allergy. Bibi huyo alipimwa presha na kukutwa ipo juu kama inavyoonekana pichani. Nlijaribu kufatilia ni duka la dawa gani lakini kwa sababu ya bibi kutokuwa na kumbukumbu vizuri zoezi likawa gumu sana. Kwa sasa bibi huyo yupo kwenye matibabu ya awali ya presha ambayo ni kumpima presha katika nyakati tofauti tatu huku akiboresha mwenendo wa maisha ikiwemo kutotumia chumvi kwa wingi n.k kwanza kabla hajaanza dawa.

USHAURI KWA UMMA
Nenda hospitali kama unadalili ambazo zinaulazima kwenda hospitali au ulitumia dawa na haikukusaidia

USHAURI KWA SERIKALI
wataalamu wa dawa hasa kwenye maduka madogo madogo ya dawa wapewe semina mara kwa mara kila baada ya muda fulani maalumu kama ilivyo kwa madaktari ili kuepusha matibabu yasiyosahihi kwa wagonjwa

USHAURI KWA WATOA DAWA ( PHARMACEUTICAL TECHNICHIANS)
nivyema kumshauri mtu akamwone daktari kwanza kama dalili alizokueleza huzielewielewi kuliko kujali tu uingize fedha.
Wahudumu wa pharmacy siku hizi wamekuwa Madaktari.
 
Back
Top Bottom