Doubleg Malafyale
JF-Expert Member
- Feb 17, 2017
- 2,733
- 3,561
Kumekuwa na jitihada nyingi wakati wa uchaguzi wanasiasa kutaka kuonesha walivyofanya maajabu, ubaya nipale yanapotengenezwa mambo kinguvu ili kusadifu matakwa ya wanasiasa.
Tunakumbuka 2013 matokeo ya K IV yalinogeshwa ili BRN (big results now) ionekane imeleta output kubwa enzi hiyo.
Hivi sasa niajabu kidogo jinsi shule za serikali nane zimeshika kumi bora matokeo KVI.
Shule za private zimewekeza mmmno natena kadhaa huchukua wanafunzi bora tupu na huwalipa walimu wake vizuri sana,zina vifaa bora kabisa vya kufundishia na kujifunzia sasa leo iweje wazidiwe na shule ambazo wanafunzi hawachujwi, chakula cha wanafunzi ni tabu, walimu hawalipwi vyema, mishahara haiongezeki, madaraja kupanda ni kwashida, wanaidai serikali malimbikizi ya mishahara muda mrefu bila kulipwa,wamepandishiwa kibabe makato ya heslb na wanalalamika awamu ya tano kutokuwajali kama ile ya nne na matatizo mengine mengi.
Bila hata ya utafiti ni dhahiri point tatu zinatafutwa kwabao la mkono nahii ni aibu kuu maana bila elimu bora taifa huishia kusinyaa hata lijengwejengwe vipi. Tunataka elimu bora isiyolongoshewa siasa za ubabe ubabe kulazimisha yasiyoyamkinika.
#ondoa magumashi kwenye elimu.
Hoja yako ni ipi? Hutaki shule za serikali zifanye vyema au? Kisa tu awali vzr,walimu wake hawajalipwa mishahara minono n.k ww unsona ndo kigezo cha kufeli? Zikifaulisha ni kosa?
Mbona zikifelisha mnapandisha uzi umu kuzilaumu kwann zinazidiwa,
Binadamu siku zote nj vigeugeu
Enzi zetu sisis tunasoma shule za serikali ndo zilikuwa ongoza si olevel wala advance na mtu ukisoma private unaonekana kilaza
Naona sasa upepo unabadilika iwe kama zamani wewe unataka shule za private ziendelee kufeli☺☺
Kama umesoma private na umefeli ni wewe mkuu wapo walio faulu