DOKEZO Tahadhari: Unakula kuku au vibudu?

DOKEZO Tahadhari: Unakula kuku au vibudu?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Ngoja niwasanue wananchi wenzangu

Siku hizi wilaya Bagamoyo (Mapinga, Kerege, Kiaraka), ambapo wengi wetu wafugaji wa kuku ndiyo tunafanyia ufugaji mkubwa)

Nimekuwa naona makundi ya wakina mama na vijana wamebeba ndoo alfajiri wakitokea mashambani kati ya saa 1 hadi 3 asubuhi au jioni kuanzia saa 12 hadi 2 usiku.

Mwanzo nilifikiri Wanaenda kununua maziwa katika nashamba ya watu kisha wanayaleta mjini kwa ajili ya biashara

HAPANA! zile ndoo zina kuku waliokufa mabandani sasa wanaletwa mjini kwa ajili ya biashara

Ni hivi, ukiwa mfugaji wa kuku wa nyama wengi (1000, 5000 hadi 10,000) ni kawaida sana kuingia bandani na kukuta kuku 5, 10 , 20, 30 hadi 50 wamekufa asubuhi au Jioni.

Sasa utaratibu ni kwamba vijana wa kazi hawaruhusiwi kuwatupa mpaka mimi mwenye banda au meneja aje awashuhudie, awahesabu na kisha asimamie zoezi la kuwafukia kuku waliokufa.

Sasa kumbe pale tunapofukia kuku waliokufa na ukiondoka tu, nyuma yake ndiyo wanaingia wale wamama wenye ndoo, wanauziwa wale kuku waliokufa Tsh 1,000 kwa kila kuku mmoja.

Wanawafukua kisha wanahesabiana na kuwanunua, wale wamama wenye ndoo wanawaleta mjini kwa matumizi ya kitoweo.

Wenyewe wanasema ukishaweka Kitunguu swaumu na tangawizi kujua kuku huyo alikuwa kibudu ni mpaka muuzaji akutonye la sivyo huwezi kujua.

Lakini pia bei yake lazima ushtuke, kuku nusu anauzwa Tsh 3,000, kuku rangi yake nyeusi akisha kaangwa, kuku kapakwa rangi za njano au nyekundu kupoteza ishara za kuonekana ni kibudu.

Mimi au wewe huenda tumeshakula Vibudu tukifikiri ni Kuku, tuongeze umakini katika kuchagua na Kununua Kuku.

20230904_002259.jpg
20230904_002256.jpg
 
Nunua kuku interchick kuepuka kula vibudu!
Pia ukienda sokoni kununua kuku hakikisha wanamchinja kuku ukiwa unamuona. Usikubali waende sehemu ambayo huoni. Wengi huwa wanabadilishiwa anachukuliwa kuku aliyekufa wana kata kichwa na kumyonyoa na kumkata vipande kuku aliyekufa alafu mzima wanabaki nae anarudishwa bandani .
 
bandiko hili liwe dokezo

Vyakula tunavyolishwa kwenye Baa, Hotelini, Migahawa nk
 
To yeye bado una yeya tu hutaki kulala, vipi kwa tugimbe kuna umeme hapo?🤣🤣🤣🤣
 
uzuri nilipo napochukuaga kuku madori, mfugaji namjua 🙌

Ila kuku madori ananoga akaangwe, achomwe, makange.

Wa kienyeji asipochemshwa ipasavyo, ule ugumu wake hapana jamani 😄 Atabaki kuwa favorite kwenye mchemsho
 
Back
Top Bottom