DOKEZO Tahadhari: Unakula kuku au vibudu?

DOKEZO Tahadhari: Unakula kuku au vibudu?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Unakuta mama mtaani anauza supu ya kuku bei poa unashangaa nyama kubwa inauzwa mia mbili, kumbe ni kibudu
Ndiyo maana Dar huwezi kusikia mtu kafa njaa japo ina wakazi wengi mno na hawalimi. Hili ni suala la kuku tu. Njia za kuingiza fedha kiharamu ni nyingi, na vyakula haramu ni vingi. Ukiamua kufuatilia kila aina ya chakula basi unaweza kuhama jiji.
 
Humu wengi mtasema silibluku wa kisasa ila nafsi zenu zinawasuta😂😂 mimi nisichokula mjini ji miguu utumbo maini firigisi kutokana na dawa wanazokuziwa ila nyama hata ianze kuoza nakula. vitu vimekarangizwa vinaladha niviache haiwezekani. Alishakufa nguruwe wangu bandani doctor kuja ananiambia ni mambo ya sumu kuvu kwenye pumba mimi sikuuliza mara mbili nikapita na mapaja mbavu na mgongo nilizika vitu baadhi ila aliliwa kama kawaida. Mjini ukichagua sana unakutana na za uso
 
Watu wanalishwa sana vibudu kwakweli.

Miaka ya nyuma kidogo, kuna jirani yetu kuku wake walikufa kama wawili hivi, sasa hakuwafukia aliwatupa tu jalalani, kuna teja mmoja alipita akawaona, akasema: yaani nyinyi mnatupa hela!, akawaokota wale kuku na kuondokanao.

Hivyo bila shaka walienda kulishwa watu wale kuku.
 
Ngoja niwasanue wananchi wenzangu

Siku hizi wilaya Bagamoyo (Mapinga, Kerege, Kiaraka), ambapo wengi wetu wafugaji wa kuku ndiyo tunafanyia ufugaji mkubwa)

Nimekuwa naona makundi ya wakina mama na vijana wamebeba ndoo alfajiri wakitokea mashambani kati ya saa 1 hadi 3 asubuhi au jioni kuanzia saa 12 hadi 2 usiku.

Mwanzo nilifikiri Wanaenda kununua maziwa katika nashamba ya watu kisha wanayaleta mjini kwa ajili ya biashara

HAPANA! zile ndoo zina kuku waliokufa mabandani sasa wanaletwa mjini kwa ajili ya biashara

Ni hivi.., ukiwa mfugaji wa kuku wa nyama wengi (1000, 5000 hadi 10,000) ni kawaida sana kuingia bandani na kukuta kuku 5, 10 , 20, 30 hadi 50 wamekufa asubuhi au Jioni

Sasa utaratibu ni kwamba vijana wa kazi hawaruhusiwi kuwatupa mpaka mimi mwenye banda au meneja aje awashuhudie, awahesabu na kisha asimamie zoezi la kuwafukia kuku waliokufa

Sasa kumbe pale tunapofukia kuku waliokufa na ukiondoka tu, nyuma yake ndiyo wanaingia wale wamama wenye ndoo, wanauziwa wale kuku waliokufa Tsh 1,000 kwa kila kuku mmoja

Wanawafukua kisha wanahesabiana na kuwanunua, wale wamama wenye ndoo wanawaleta mjini kwa matumizi ya kitoweo

Wenyewe wanasema ukishaweka Kitunguu swaumu na tangawizi kujua kuku huyo alikuwa kibudu ni mpaka muuzaji akutonye la sivyo huwezi kujua

Lakini pia bei yake lazima ushtuke, kuku nusu anauzwa Tsh 3,000, kuku rangi yake nyeusi akisha kaangwa, kuku kapakwa rangi za njano au nyekundu kupoteza ishara za kuonekana ni kibudu.

Mimi au wewe huenda tumeshakula Vibudu tukifikiri ni Kuku,Tuongeze umakini katika kuchagua na Kununua Kuku.
Sikupingi,, nakumbuka kuna kijana alifumwa anaokota kuku maeneo ya darajani pale karibu na kituo cha jangwani cha mwendo kasi njia ya kuelekea posta kutokea magomeni mataa... Alikuwa anaokota kuku waliokufa na walikuwa wengi sana... SAsa sijui waliletwa na maji ya mtoni au walitupwa tu.... Na alivyo onwa aliacha ndoo alikimbia huyo..... Watu walijiuliza sana...... Ila wanadamu Wana roho mbaya sana.... Wanaangalia faida kubwa sio usalama wa mwengine
 
Ndiyo maana Dar huwezi kusikia mtu kafa njaa japo ina wakazi wengi mno na hawalimi. Hili ni suala la kuku tu. Njia za kuingiza fedha kiharamu ni nyingi, na vyakula haramu ni vingi. Ukiamua kufuatilia kila aina ya chakula basi unaweza kuhama jiji.
Pale Pugu mnadani kuna ng'ombe huja, wengine hufa kwa uchovu wa safari. Kuna watu hupewa kazi ya kwenda kufukia mizoga hiyo kwenye ule msitu kuelekea Kisarawe. Hawa jamaa hawatimizi jukumu lao la kufukia mizoga inakuwa ni fursa kwao kuchuna na kukatakata nyama na kuingia nazo mitaani kutafuta masoko. Watu wanakula mizoga kama hawana akili nzuri. Hii tabia ya kula mizoga nimeiona sehemu nyingi, hata sehemu za wafugaji mifugo ikifa na kutelekezwa na wafugaji waswahili huchangamkia nyama zake bila kujali huo mfugo umekufa kwa ugonjwa gani. Kuna mwingine mpika supu ya mbuzi anazuga kuweka kichwa na miguu ya mbuzi kumbe sufuriani kachemsha nyama ya mbwa, ukila unajisikia kiu balaa kumbe umekula mbwa.
 
Humu wengi mtasema silibluku wa kisasa ila nafsi zenu zinawasuta[emoji23][emoji23] mimi nisichokula mjini ji miguu utumbo maini firigisi kutokana na dawa wanazokuziwa ila nyama hata ianze kuoza nakula. vitu vimekarangizwa vinaladha niviache haiwezekani. Alishakufa nguruwe wangu bandani doctor kuja ananiambia ni mambo ya sumu kuvu kwenye pumba mimi sikuuliza mara mbili nikapita na mapaja mbavu na mgongo nilizika vitu baadhi ila aliliwa kama kawaida. Mjini ukichagua sana unakutana na za uso
[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji1544][emoji1550][emoji23]
20230904_081638.jpg
 
Kuna kitu kinaitwa "road trip" kila Jumamosi mimi na familia hatukai mjini au nyumbani!! Tunakwenda trip ya mahali tusipopajua hapa DSM!!

Katika hizo safari ndiko tunanunua mahitaji ya wiki!! Mfano hao kuku "kyenyeji pyua" mbuzi, tunakutana na magulio tunanunua mali za shamba kibao!! Huu mkaa mnanunua mjini 80k hadi 100k hapo Kilimani 10k tu!! Maliasili hawajawahi kukamata gari yangu wao wanadili na malori tu!!

Samaki, tunakwenda huko Nyamisati na maeneo ya Mchungu huko unakamata fish wa mwezi mzima kwa 30k tu!!

Hayo mabroiler mnakula sababu hamtembei!! Watoto pia wanajifunza mengi sana matembezini huko
 
Naonaga hata ng'ombe akifa anapakizwa kwenye guta wanamfunika sijui wanapeleka kuzika wapi[emoji1]
Kuna ngombe wangu alikuwa anaumwa kaugua kama muda 2a mwezi hivi, sindano za haja. Zile dawa anazochomwa zina maelekezo.kama kula nyama iliwe baada ya siku kadhaa.
Sasa kimbunga siku amekufa, nikatafuta vijana wachimbe shimo wazike.
Aisee vijana walisema unazikaje Mboga, nikasema mimi siwezi kula ila nachoomba tulinde afya ya jamii. Wakasemq tuachie sisi hili swala. Walimchukua wakaenda kugawana huko
 
Huyo aliyeumwa kwa muda mrefu kidogo Afadhali kuliko yule anayejidondokea tu, ANTRAX! inaua fasta fasta, unavimba kichwa baada ya siku 2 niagie!
 
Ngoja niwasanue wananchi wenzangu

Siku hizi wilaya Bagamoyo (Mapinga, Kerege, Kiaraka), ambapo wengi wetu wafugaji wa kuku ndiyo tunafanyia ufugaji mkubwa)

Nimekuwa naona makundi ya wakina mama na vijana wamebeba ndoo alfajiri wakitokea mashambani kati ya saa 1 hadi 3 asubuhi au jioni kuanzia saa 12 hadi 2 usiku.

Mwanzo nilifikiri Wanaenda kununua maziwa katika nashamba ya watu kisha wanayaleta mjini kwa ajili ya biashara

HAPANA! zile ndoo zina kuku waliokufa mabandani sasa wanaletwa mjini kwa ajili ya biashara

Ni hivi, ukiwa mfugaji wa kuku wa nyama wengi (1000, 5000 hadi 10,000) ni kawaida sana kuingia bandani na kukuta kuku 5, 10 , 20, 30 hadi 50 wamekufa asubuhi au Jioni.

Sasa utaratibu ni kwamba vijana wa kazi hawaruhusiwi kuwatupa mpaka mimi mwenye banda au meneja aje awashuhudie, awahesabu na kisha asimamie zoezi la kuwafukia kuku waliokufa.

Sasa kumbe pale tunapofukia kuku waliokufa na ukiondoka tu, nyuma yake ndiyo wanaingia wale wamama wenye ndoo, wanauziwa wale kuku waliokufa Tsh 1,000 kwa kila kuku mmoja.

Wanawafukua kisha wanahesabiana na kuwanunua, wale wamama wenye ndoo wanawaleta mjini kwa matumizi ya kitoweo.

Wenyewe wanasema ukishaweka Kitunguu swaumu na tangawizi kujua kuku huyo alikuwa kibudu ni mpaka muuzaji akutonye la sivyo huwezi kujua.

Lakini pia bei yake lazima ushtuke, kuku nusu anauzwa Tsh 3,000, kuku rangi yake nyeusi akisha kaangwa, kuku kapakwa rangi za njano au nyekundu kupoteza ishara za kuonekana ni kibudu.

Mimi au wewe huenda tumeshakula Vibudu tukifikiri ni Kuku, tuongeze umakini katika kuchagua na Kununua Kuku.
 
Attachments

  • B5881D0E-5B76-4BD1-811F-28E1D1257670.jpeg
    B5881D0E-5B76-4BD1-811F-28E1D1257670.jpeg
    49.8 KB · Views: 3
Back
Top Bottom