DOKEZO Tahadhari: Unakula kuku au vibudu?

DOKEZO Tahadhari: Unakula kuku au vibudu?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Pia ukienda sokoni kununua kuku hakikisha wanamchinja kuku ukiwa unamuona. Usikubali waende sehemu ambayo huoni. Wengi huwa wanabadilishiwa anachukuliwa kuku aliyekufa wana kata kichwa na kumyonyoa na kumkata vipande kuku aliyekufa alafu mzima wanabaki nae anarudishwa bandani .
Kaka pale Loriondo kwenye Mabanda ya Kuku ndo ninaponunua kitoweo.... nikishanunua namwachia Jamaa akachnje... anamtia kwenye Maji Moto... ananletea tayari vipande vipande.....km nao wana uhuni huu... kaka nimeshalishwa sana vibudu.... ntaanza kuwachunguza kaka...
 
uzuri nilipo napochukuaga kuku madori, mfugaji namjua 🙌

Ila kuku madori ananoga akaangwe, achomwe, makange.

Wa kienyeji asipochemshwa ipasavyo, ule ugumu wake hapana jamani 😄 Atabaki kuwa favorite kwenye mchemsho
Haya maneno utayasikia kwa wanaume na wanawake wa Dar es salaam pekee, huwezi kusikia raia wa mikoani eti analalamikia ugumu wa nyama ya kuku wa kienyeji.

Watu wa DAR ni sawa kabisa na kuku Broilera 🤣🤣🤣🤣 wacha walane tuu.
 
20230903_075534.jpg
 
Kaka pale Loriondo kwenye Mabanda ya Kuku ndo ninaponunua kitoweo.... nikishanunua namwachia Jamaa akachnje... anamtia kwenye Maji Moto... ananletea tayari vipande vipande.....km nao wana uhuni huu... kaka nimeshalishwa sana vibudu.... ntaanza kuwachunguza kaka...
Brother binadamu hawaaminiki lazima usimamie mwanzo mwisho japo sidhabi kama pale kuna huu uhuni wa kubadilishiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naonaga hata ng'ombe akifa anapakizwa kwenye guta wanamfunika sijui wanapeleka kuzika wapi😄
Ng'ombe wengi hufia njiani wakati wanasafirishwa kutoka mkoani kuja Dar

Na hao ng'ombe wanakuwa washanunuliwa tangu shambani so mnunuzi hawezi kukubali apate hasara.

Ng'ombe waliofia njiani wanachinjwa huko huko na nyama yake sometimes inauzwa kwa bei ile ile.
 
Haya maneno utayasikia kwa wanaume na wanawake wa Dar es salaam pekee, huwezi kusikia raia wa mikoani eti analalamikia ugumu wa nyama ya kuku wa kienyeji.

Watu wa DAR ni sawa kabisa na kuku Broilera 🤣🤣🤣🤣 wacha walane tuu.
Mkuu wakulane kivipi😂😂
 
Ng'ombe wengi hufia njiani wakati wanasafirishwa kutoka mkoani kuja Dar

Na hao ng'ombe wanakuwa washanunuliwa tangu shambani so mnunuzi hawezi kukubali apate hasara.

Ng'ombe waliofia njiani wanachinjwa huko huko na nyama yake sometimes inauzwa kwa bei ile ile.
Kweli mkuu ng'ombe za kisasa zinafia bandani wanapeleka buchani!!

2016 nilinunua nyama, aisee familia nzima kuharisha,kusinzia, homa!! Nikawaza huenda ng'ombe alikuwa kibudu au alikuwa mgonjwa kapigwa sindano sana 😳😳

Nilihisi nyama kimeo coz vile nainunua machale kun'desa hivi😂😂
 
Hii issue inazunguka kwenye magroup ya WhatsApp kwa zaidi ya wiki sasa,kama kawaida yako umekimbilia kuileta huku,ni jambo jema ila ungeweka credit pia kuliko kujifanya kua eti wewe ndio umeshuhudia hilo zoezi.
 
Africa maisha yetu ni rehema zake Mungu na wema wake ndio unatupa uhai kila siku aijuae yeye.

Hakika mkuu, mfano: nyanya zinapigwa sumu kali, kesho mteja kapatikana sokoni - nyumbani!! Wengine hawaoshi vizuri wala hawamenyi ni mchuzi au kachumbari mezani😳
 
Tuishi tu ila haya mambo ni mtihani kuna siku utachoka utasema leo familia wacha tutoke huko mnakoenda inakuwaje na nyama pendwa kuku.
 
Ndo maana kuku la kisasa siyali
Ngoja niwasanue wananchi wenzangu

Siku hizi wilaya Bagamoyo (Mapinga, Kerege, Kiaraka), ambapo wengi wetu wafugaji wa kuku ndiyo tunafanyia ufugaji mkubwa)

Nimekuwa naona makundi ya wakina mama na vijana wamebeba ndoo alfajiri wakitokea mashambani kati ya saa 1 hadi 3 asubuhi au jioni kuanzia saa 12 hadi 2 usiku.

Mwanzo nilifikiri Wanaenda kununua maziwa katika nashamba ya watu kisha wanayaleta mjini kwa ajili ya biashara

HAPANA! zile ndoo zina kuku waliokufa mabandani sasa wanaletwa mjini kwa ajili ya biashara

Ni hivi, ukiwa mfugaji wa kuku wa nyama wengi (1000, 5000 hadi 10,000) ni kawaida sana kuingia bandani na kukuta kuku 5, 10 , 20, 30 hadi 50 wamekufa asubuhi au Jioni.

Sasa utaratibu ni kwamba vijana wa kazi hawaruhusiwi kuwatupa mpaka mimi mwenye banda au meneja aje awashuhudie, awahesabu na kisha asimamie zoezi la kuwafukia kuku waliokufa.

Sasa kumbe pale tunapofukia kuku waliokufa na ukiondoka tu, nyuma yake ndiyo wanaingia wale wamama wenye ndoo, wanauziwa wale kuku waliokufa Tsh 1,000 kwa kila kuku mmoja.

Wanawafukua kisha wanahesabiana na kuwanunua, wale wamama wenye ndoo wanawaleta mjini kwa matumizi ya kitoweo.

Wenyewe wanasema ukishaweka Kitunguu swaumu na tangawizi kujua kuku huyo alikuwa kibudu ni mpaka muuzaji akutonye la sivyo huwezi kujua.

Lakini pia bei yake lazima ushtuke, kuku nusu anauzwa Tsh 3,000, kuku rangi yake nyeusi akisha kaangwa, kuku kapakwa rangi za njano au nyekundu kupoteza ishara za kuonekana ni kibudu.

Mimi au wewe huenda tumeshakula Vibudu tukifikiri ni Kuku, tuongeze umakini katika kuchagua na Kununua Kuku.
 
Back
Top Bottom