sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Kinachofanyika ni kwamba mtu anafukiwa miguu kwenye shimo ama anaweza kuwa ni kilema hana miguu, wanaiweka miguu ya ng'ombe kwenye suruali halafu kwa namna wanayojua wenyewe inaunganishwa na na kiwili wili.
Kuhusu huo mkia unacheza cheza kila mara, kuna mota inafungwa ama kuna uzi umepita chini ya ardhi kuna watu wanachezesha
Watu wanaandaliwa waje kushika shika na kujifanya hawaamini wanachokiona na kutoa shuhuda za uongo, hii ndio inaitwa "biashara ni matangazo"
Baada ya hapo mganga feki ataonekana ni mtaalama sana, ataanza kutafutwa na wajinga na atapiga pesa za wajinga
Zimbabwe hii hapa
Wabongo nao hawaachwi, huyu jamaa sijui wamemtoa kijiwe gani na hizo rasta zake ajifanye alilala na mke wa mtu, video zake zimebamba sana kwenye magroup na watu wanadhani nikweli.