Tahadhari: Utapeli wa Zimbabwe wa kubadili mtu aliyelala na mke wa mtu aonekane ana miguu ya ng'ombe na mkia, umefika Tanzania

Tahadhari: Utapeli wa Zimbabwe wa kubadili mtu aliyelala na mke wa mtu aonekane ana miguu ya ng'ombe na mkia, umefika Tanzania

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
903581fbfe04af0cb4fdabcff8a3cc07.png


Kinachofanyika ni kwamba mtu anafukiwa miguu kwenye shimo ama anaweza kuwa ni kilema hana miguu, wanaiweka miguu ya ng'ombe kwenye suruali halafu kwa namna wanayojua wenyewe inaunganishwa na na kiwili wili.

Kuhusu huo mkia unacheza cheza kila mara, kuna mota inafungwa ama kuna uzi umepita chini ya ardhi kuna watu wanachezesha

Watu wanaandaliwa waje kushika shika na kujifanya hawaamini wanachokiona na kutoa shuhuda za uongo, hii ndio inaitwa "biashara ni matangazo"

Baada ya hapo mganga feki ataonekana ni mtaalama sana, ataanza kutafutwa na wajinga na atapiga pesa za wajinga

Zimbabwe hii hapa



Wabongo nao hawaachwi, huyu jamaa sijui wamemtoa kijiwe gani na hizo rasta zake ajifanye alilala na mke wa mtu, video zake zimebamba sana kwenye magroup na watu wanadhani nikweli.

 
Mimi sikuziamini tangia mwanzo angalia movement ya mkia kwenye video zote mbili ,na matukio yote yametokea kwenye mazingira ya kufanana
 
Afu kwanini wote wanakuwa wamekaa sehemu yenye kichanga?

Ilitakiwa angalau awe kwenye floor ya tiles au kwenye kiti kabisa
Watamrekodi anavyokaa lakini hawawezi mrekodi akisimama ama kutembea
 
Wabongo kwa kukufanya wajuaji daaah. Eti Dunia hii kwa kumfanya Binadamu Mwenzako hivi🤣🤣🤣🤣🤣
 
Bora uyo actor wa zimbabwe alikuwa analia anaonesha uhalisia

Actor wa Tz (rasi) yeye alii anasikitika kwa kichwa tu, alafu mkia wake unacheza cheza sana kama kibendera
 
Back
Top Bottom