TAHADHARI: Wahafidhina wapo toka zamani, Kisa cha Abneli mwana wa Neri na Generali Yoabu

Mambo ya CCM watajua wenyewe maana wamelea kansa wenyewe na sasa kila dawa kwao wanaona ni adui. Labda unabii wa Nyerere wa upinzani wa kweli kutokea CCM utimie haraka ili tujenge Taifa lenye manufaa kwa wengi.
Asante Mtazamo.
 
Zipo lugha angetumia sio Uhafidhina, msingi wa chama chake ni uhafidhina ingawa sasa kimatendo ni tofauti. Uhafidhina ni itikadi sio tabia! Vitu kama unafiki ni tabia tu.

Mfano mzuri sisi Wakatoliki wapo wahafidhina wanaotaka tushike mapokeo tuliyoyapokea karne nyingi bila kubadilisha kitu! Wapo wanao challenge mabadiliko mfano namna ya ku handle mashoga kwenye huduma! Kuwa na mapadre wanawake n.k

Tofauti za kiitikadi ndio zinazoleta tofauti ya hivi vyama. Kuna watu ndani ya Chadema wanaamini hawawezi kwenda ikulu kwa maridhiano na CCM! Wanaamini hii ni mitego tu! Wapo waliolegea sababu ya ku suffocate na kibano cha JPM sasa hawaamini tena kama wanaweza kupambana na CCM bila maridhiano.

Muda ni mwalimu mzuri

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Sawa Mtazamo. Tabia inapokuwa inaungwa mkono na watu wengi na kuwa applied kwenye mfumo fulani wa maisha. Ni sawa kabisa ukiuita Uhafidhina.

Ofcourse uhafidhina sio jina baya maana ni itikadi lakini umepelekea matokeo hasi kwa mara nyingi unapotumika kwa dunia ya leo.

Mfano Ccm imekopi huo uhafidhina huko Urusi na China ambapo china yenyewe imeshaachana nao. Imebaki ni jina tu in Practicea haupo real.
 
Na ndivyo walivyo wahafidhina wa hapa Nchini !! Yaani exactly kama ulivyoeleza hapo juu ! Yaani hawaoni tatizo kumfanyia mtu ubaya wowote ule na wa namna yeyote ile mradi tu yule mtu ana mitizamo tofauti na wao !!
 
Wasilikilizwe matakwa yao kama yana vigezo kitaifa wasipuuzwe.
Midset yao huwa ni umimi umimi na kuona wengine hawastahili chochote kile bali wao ndio wenye hati miliki ya kila kitu !! Kwa kawaida huwa ni ngumu kwao kubadilika kwa hiari !!
 
Mkuu ujumbe wako ni mzuri Ila Kwa kuongezea tu hapo kwenye nukuu ya biblia kama ilivyoandikwa. Imeandikwa kwamba Yoabu alimwua Abneli Kwa ajili ya damu ya Asaheli ndugu yake, ambaye aliuwawa na Abneli.
2 Sam 3;27
 
Hiyo picha hapo chini ya dada shombeshombe inahusiana na huu uzi mkuu? Ni nan huyu shombeshombe?
 
Hao hawajaacha ila wameuboresha kimkakati lakini uyaonayo mbele ni kivuli tu. Mambo yao msimamo wao ni ule ule ila kwenye uchumi ndio wameboresha kwa kivuli cha majasusi. Mfano matajiri wengi wa hizi nchi ni majasusi na wana invest all over the world lakini wao ni vivuli tu.

Sisi tunatikisa misingi huku hatujajiandaa na matokeo yake. Huwezi kutabiri reactions za wananchi kama hujawaandaa na hawana habari na mnayofanya. Hata haya ya maridhiano picha kubwa ya wananchi unafikiri ni wao kutaka maridhiano sababu ya mambo ya utawala wa awamu ya tano? Wanaona ni mambo ya wakubwa tu waligusana kwenye maslahi yao na sasa wanajadiliana namna ya kula kwa urefu wa kamba.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ujumbe wako ni mzuri Ila Kwa kuongezea tu hapo kwenye nukuu ya biblia kama ilivyoandikwa. Imeandikwa kwamba Yoabu alimwua Abneli Kwa akili ya damu ya Asaheli ndugu yake, ambaye aliuwawa na Abneli.
2 Sam 3;27
Ni kweli labisa. Asaheli ndugu yake Yoabu aliuawawa wakiwa vitani.
Uhasama ulikuwa mkubwa na ndio maana palihitajika Maridhiano.

Lakimi Mhafidhina Yoabu hakukubali hilo. Roho ya kisasi ilimwandama.
 
Abneri na Yoabu ilikuwa kisasi sio ishu ya uhafidhina.
Abneri alimuua ndg yake na Yoabu hivyo ilikuwa ni nafasi pekee ya Yoabu kulipa kisasi kwa Abneri
 
Abneri ma Yoabu ilikuwa kisasi sio ishi ya uhafidhina.
Abneri alimuua ndh yake na Yoabu hivyo ilikuwa ni nafasi pekee ya Yoabu kulipa kisasi kwa Abneri
Sababu ya Abneri kumuua ASaheli ilikuwa migogoro ya muda mrefu.

Mtu haamki asubuhi tu na kumua mtu. Kambi mbili za Daudi na Sauli zilikuwa ktk uhasama mkubwa wa muda mrefu.

Lakini pamoja na maridhiano kufanyika siku hiyo hiyo Yoabu analipiza kisasi na kuharibu mipango yoote ya Daudi ya usuluhishi.
 
Hiyo picha hapo chini ya dada shombeshombe inahusiana na huu uzi mkuu? Ni nan huyu shombeshombe?
Unaongelea huyu anayeimba?

Kama ndivyo, huyo ni Mwimbaji wa Injili Bahati Bukuku.
Anaelezea namna ya kupambana na matatizo ya kijamii kwa kutumia busara badala ya nguvu nyingi.

Anasema usitumie nyundo kumuua Nzi aliyetua kichwani mwa mtu maana utaacha jeraha kubwa kwa mtu huyo.
 
Midset yao huwa ni umimi umimi na kuona wengine hawastahili chochote kile bali wao ndio wenye hati miliki ya kila kitu !! Kwa kawaida huwa ni ngumu kwao kubadilika kwa hiari !!
Ndicho alichosema Mh Rais Samia.
 
Kuna kosa la kiuongozi Daudi alifanya.
Hakuwahusisha watu muhimu kama Yoabu.
Yoabu alihatarisha sana uhai wake kwa ajili ya Daudi lakini Daudi hakukumbuka hayo.

Ni Yoabu ndiye aliyemuondolea Daudi aibu ya kumjaza mimba mke wa Uria ambaye Daudi aliagiza awekwe mstari wa mbele ili auawe na adui kupoteza ushahidi.

KUna funzo kubwa sana...kiongozi wa juu anapofanya mapatano au maridhiano ahakikishe ushiriki wa wasaidizi wake vinginevyo atasababisha migogoro kwenye uongozi wake.

Nina wasiwasi kama wana ccm muhimu wamehusishwa na kuridhia yanayoendelea ...muda utaongea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…