TAHADHARI: Wahafidhina wapo toka zamani, Kisa cha Abneli mwana wa Neri na Generali Yoabu

Nadhani sasa unaweza kuona link iliyopo kati ya Uzi huu na Kisa hikiπŸ˜…πŸ˜…

Mfalme Daudi alikuwa na mapungufu mengi na ndio maana alikuwa ana hestate kumuonya hata kumwadhibu Yoabu.

Yoabu alijua siri nyingi za maovu ya daudi kwa kupitia hilo Daudi alikuwa dhaifu sana kwa Yoabu.

Yoabu alikuwa hasikilizi mtu yeyote ispokuwa Daudi tu na pengine anakengeuka.

Rais( Mfalme) kwa kawaida hawezi kuanzisha movement ya maridhiano then akatokea mtu mmoja kuyaharibu. Huo ndio Uhafidhina.

Maelewano ya Abneri na Daudi yalikuwa kitisho kwa Yoabu ndio maana alijihami.

Hii ndio maana ya "Tahadhari"
 
Kuna haja kuanzisha uzi kuhusu Daudi.

Huyu ana funzo kubwa sana kwetu;
1. Alikuwa mpiganaji hodari
2. Alikuwa msikivu...rejea kisa cha mke wa Nabali

3. Alikuwa na hofu ya Mungu..rejea alipopinduliwa na mwanae...kuna mtu alimzomea ...wasaidizi waliomba ruhusa ya Daudi wammalize yeye alisema...mwacheni huenda Mungu aliruhusu amzomee.

4. Kosa...kutamani mke wa mtu akioga

5. Kiburi...kuwahesabu Israel kwa kiburi akijua ni kosa.

6. Kisasi...alimkabidhi Sulemani watu kadhaa ahakikishe hawafi kwa amani isipokuwa anawamaliza.

.......DAUDI ANA MAMBO MENGI KUJIFUNZA...
 
Si "waparestina" ni "wa palestina" muandishi utakuwa wa kwetu kanda ya Ziwa si Bure,

Hongera kwa Makala yako
 
Mkuu umetoa mfano bora kabisa na ubarikiwe, ni kweli wako watu wasiotaka amani wala utangamano wala upendo na hao ndo wanamvuruga sana mama lakini Samia na Mbowe walianza na "MUNGU" watamaliza na "MUNGU".
CUF na NCCR walipoamua kufanya hayo mliwatukana sana. Ndio maana nasema chadema wengi akili hamna
 
Ndicho alichosema Mh Rais Samia.
Hao watu ndio husababisha hata mambo mabaya kutokea katika Nchi ! Wanaoitwa wahafidhina katika Nchi zilizoendelea hawako kama hawa wenzetu ambao wapo tayari kumterrorise either psychological au physically yeyote ambae watamuona haendani na fikra zao !!
 
Hoja namba
1. Alikuwa na nguvu za ajabu( alipewa na Mungu) alikuwa anaweza kuua wafilisti kwa mikono yake. Wakati anamuoa Mikali alipewa sharti la kuleta govi 100. Huu ulikuwa mtego wa Sauli ili akafie vitani.
2. Daudi alikuwa na ubabe fulani. Kisa cha kutaka kumuua Nabali ni kwa sababu Nabali alikataa kuporwa mali zake na wanajeshi wa Daudi. Ndipo mke wake Abigaili akamuomba msamaha. Baadae Nabali alifariki Daudi akamuoa mjane.

3. Alimkata Ayoub asimwue mwanaye Absalomu hata kama absalom alitaka kumpindua. Hii ni huruma ya kiwango kikubwa. Lakini mwanaye angemfanya nini?

Uhafidhina wa Yoabu ulianza zamani.

Yoabu anajifanya ana huruma kwenda kumchukua Absalome mafichoni na kutumia njama za mwanamke mmoja kumpa methali Daudi kana kwamba Yoabu anamuombea msamaha Absalom lakini njama za Yoabu ilikuwa kumsogeza karibu aweze kumdhuru.

Daudi alilia sana kifo cha mateso cha mwanaye Yoabu
 
 
Mkuu ujumbe wako ni mzuri Ila Kwa kuongezea tu hapo kwenye nukuu ya biblia kama ilivyoandikwa. Imeandikwa kwamba Yoabu alimwua Abneli Kwa akili ya damu ya Asaheli ndugu yake, ambaye aliuwawa na Abneli.
2 Sam 3;27
Ndio ujue kwamba mleta mada haelewi hata anachojaribu kutuelezea.

Hakuna relevance yeyote ile ya andiko na uhafidhina.
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Hiyo story ya bible umeichanganya changanya sana hadi imekosa ladha
 
Kumbe ndio bahati bukuku huyo? Maana zaman hakua mwarabu ivo mpaka nimemsahau asee!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…