TAHADHARI: Watanzania waliobado na utu wema na mioyo ya kujali, huku mitaani tuwe makini tusije kuponza wenzetu

TAHADHARI: Watanzania waliobado na utu wema na mioyo ya kujali, huku mitaani tuwe makini tusije kuponza wenzetu

Mimi namuelekeza mtu njia km amepotea ila simuelekezi nyumbani kwa mtu maana sijui anaenda kumfanya nini huyo mtu na ana nia gani na huyo mtu, nimejifunza nasikia jamaa watatu wakajifanya mafundi wa TANESCO wakamwambia afungue mlango wana mazungumzo na yeye wakiwa wamevaa km watu kutoka TANESCO then alipofungua tu wakaja jamaa wanne wakiwa na mitutu ya bunduki na kumdavila kisha kutokomea nae kusikojulikana
Hapa ukiwa kama wewe unafanyaje mkuu na unaona kabisa TANESCO hawa hapa vipi ufungui mlango
 
Hii ni tabia sugu Kwa watanzania wengi ,mtu anaulizwa ulizwa na mtu humjui au awe anamjua anamwagika tu kma sifa.

Mimi niliwahi kuhamia sehemu Moja mpya nkakonect kidgo na coworker wangu akapajua kwangu sijakaa wiki staff nzima wakawanapajua
kuja kufwatilia kumbe ni yule coworker nlie mwelekeza Tena mwanaume,sema sikuchukua round nkahama asee tuache kusambaza taarifa za watu hovyo hovyo na kujifanya kujuana Juana
Mkuu naomba niuulize kidogo mtu anakuja kuniulizia mtu namjua kabisa na Nyumba naona Ile pale na jirani yangu kabisa vipi hapo nasema simjui mtu huyo, mkuu Kuna vitu basi tu Kuna mazingira basi tu
 
Baada ya pilika pilika za kutafuta ugali, jioni hii Nimekaa-zangu nje ya nyumba napata upepo wa el Nino. Anapita njiani mtu mzima ila simfahamu kabisa maeneo ya mtaa wetu, kisha ghafla anajongea karibu yangu na kuniuliza unamfahamu Pendo.

Mimi: pendo wa wapi

yeye: anakaa mitaa hii, kama unamfahamu au anapafahamu anapokaa nielekeze ninashida nae.

Mimi: kufupisha mambo namjibu simfahamu na ni-mgeni eneo hili.

Akaondoka ila mbele kidogo kama hatua tano ivi akamsisha mmama fulani njiani na kuanza kumuulizia pendo kama anamfahamu na anapafahamu anapoishi amuelekeze. Bahati nzuri huyo mmama akawa anamfahamu pendo na anapoishi akawa anapafahamu, akamuelekeza huyo mbaba stanger tena kwa kumuonesha mpaka mlango wa geti la nyumba (nyumba ilikuwa inaonekana haikuwa mbali).

Cha ajabu ni kwamba huyo mbaba hakuelekea kule uelekeo wa nyumba aliko elekezwa, badala yake alirudia uelekeo alikotokeo, ndio kitu kimenishanganza sana.

Nikamfuata yule mmama nikamuonya awe makini na kutoa taarifa za watu kwa wageni asiowajua.

Simba bingwa CAF
Arsenali bingwa UEFA
Mungu ibariki Tanzania
Hapo chini kwenye mabingwa watarajiwa tupo pamoja sana!
 
Nchi zilizostarabika hata namba ya mtu huwezi kugawa kwa mtu mwingine mpaka upate ridhaa kutoka kwa mhusika.
 
Mkuu naomba niuulize kidogo mtu anakuja kuniulizia mtu namjua kabisa na Nyumba naona Ile pale na jirani yangu kabisa vipi hapo nasema simjui mtu huyo, mkuu Kuna vitu basi tu Kuna mazingira basi tu
Kutokutoa location ya mtu Kwa mtu yeyote Kuna faida nyingi kuliko hasra ,jibu tu simjui au sijui kwake ova
 
Mkuu naomba niuulize kidogo mtu anakuja kuniulizia mtu namjua kabisa na Nyumba naona Ile pale na jirani yangu kabisa vipi hapo nasema simjui mtu huyo, mkuu Kuna vitu basi tu Kuna mazingira basi tu
Inshu rahisi unamuelekeza tu alipo mwenyeketi au kiongozi wa serikali ya mtaa, ndiko atapata details zote anazohitaji. Hiyo ni kwa usalama wako wewe mwenyewe na muhusika. Tofauti na hapo kama mtafutaji ana nia mbaya na anaetafutwa hujioni wewe ndio utakuwa shahidi wa kuanzia.
 
Mimi namuelekeza mtu njia km amepotea ila simuelekezi nyumbani kwa mtu maana sijui anaenda kumfanya nini huyo mtu na ana nia gani na huyo mtu, nimejifunza nasikia jamaa watatu wakajifanya mafundi wa TANESCO wakamwambia afungue mlango wana mazungumzo na yeye wakiwa wamevaa km watu kutoka TANESCO then alipofungua tu wakaja jamaa wanne wakiwa na mitutu ya bunduki na kumdavila kisha kutokomea nae kusikojulikana
Habari ndugu wadau.

Pole kwa changamoto, kama unachokisema kiko hivo, mfanyakazi wa TANESCO utambulisho wake ni kitambulisho cha kazi na wala haitakiwi kuwa maneno au mavazi. Hivyo kwa mtu yeyote mwenye mashaka anatakiwa kuuliza kitambulisho chake cha kazi na wala siyo mavazi maana kitambulisho kinakua na majina yake halisi, jina la taasisi na saini ya mkuu wa taasisi.

Aidha kwa mazingira ambayo yanakua na utata zaidi ni vizuri kushirikisha ofisi ya serikali ya mtaa au kitongoji kulingana na eneo ulilopo.
Hii inahusisha pia watu wanaoweza kujiita TANESCO na kuja kufanya uhalifu kwa jina la taasisi, ukizingatia muongozo huu itapunguza hatari au hujuma ambayo inaweza kufanyika kwenye miundombinu au changamoto kama uliyotueleza.

Asanteni kwa ushirikiano wenu.^HN
 
Back
Top Bottom