Tahadhari: Wizi wa vifaa ndani ya magari hospitali ya KCMC balaa

Tahadhari: Wizi wa vifaa ndani ya magari hospitali ya KCMC balaa

Fred Mwakitundu

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
227
Reaction score
382
Ni tahadhari tu kwa wale mnaotumia magari binafsi kwenda kuwaona wagonjwa ama kwa shughuli nyingine katika Hospital ya Rufaa ya Kanda ya KCMC mjini Moshi kwamba muwe makini sana kuna mtandao mkubwa wa vijana wanaotumia funguo bandia kufungua milango ya magari na kuiba vitu vilivyomo ndani ya gari na kufunga vizuri na kisha kuondoka pasipo kutiwa nguvuni.

Hiki kimekuwa kilio cha siku nyingi kwa watu wenye magari kiasi cha kupaona KCMC kama si mahala salama kwa usalama wa mali zao na kinachoshangaza zaidi eneo lote la maegesho wanapoegesha watu kunamulikwa na camera za usalama lakini wizi ndo kwanza unashika kasi

Hivi karibuni kinara wa mtandao huo alitiwa nguvuni tena kwa juhudi binafsi ya mtu aliyeibiwa vitu vyake ndani ya gari baada ya kuanzisha uchunguzi usio rasmi kwa kufuatilia nyendo za kijana huyo mdogomdogo na siku ya siku akambamba akiiba vitu ndani ya gari ya mtu mwingine na kuziarifu mamlaka za KCMC na hatimaye kumtia nguvuni

Kijana huyo alishitakiwa mahakamani na kutiwa hatiani na hadi sasa bado anatumikia kifungo chake lakini huku nyuma ameacha mizizi inayoendelea kutambaa bila kukatwa

Hii ni taarifa ya awali taarifa kamili ni hapo baadae

Wenye magari mkae chonjo, kama una kitu cha thamani ndani ya gari usikiache unaweza ukalia pasipo kuchapwa makola
 
Vijana wa Kichagga wanajiandaa Krismas 2022, ndicho mlichochagua kutafuta pessa kwa njia yoyote ngoja mpigwe tuuu
 
Hivi machalii mna shida gani lakini, pigeni kazi halali bhanaa.....
 
Kamateni mmoja muue. Watajifunza.

Screenshot_20211122-100534_WhatsApp.jpg
 
Kuna mwizi anaitwa kokomit alikamatwa na sasa yupo ndani anatumiķia kifungo cha miezi 6 gerezani
 
Dawa ni kuwakea na misosi minono yenye sumu wakifungua kuangalia ndani wanaona minyama ya kuku iliyochomwa.
Wakila tu kaishia habari zao
 
Kuna mwizi anaitwa kokomit alikamatwa na sasa yupo ndani anatumiķia kifungo cha miezi 6 gerezani
Kokomiti kabobea kwenye hiyo sekta,alijichanganya kwenye gari ya jirani yake Dr Rambau.
 
Back
Top Bottom