Tahadhari ya Baa la njaa duniani yatolewa, mtu mmoja hufariki kila baada ya Sekunde 4

Tahadhari ya Baa la njaa duniani yatolewa, mtu mmoja hufariki kila baada ya Sekunde 4

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Katika barua ya wazi kwa viongozi wanaokutana katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jijini NewYork, Mashirika 238 kutoka Nchi 75, yakiwemo #Oxfam, #SaveTheChildren na #PlanInternational yameelezea hali ya wasiwasi ongezeko la viwango vya njaa

Barua hiyo imebainisha kuwa Mtu mmoja anakadiriwa kufariki dunia kila baada ya sekunde nne kutokana na njaa hivyo mataifa hayo yamehimiza hatua ya kimataifa kuchukuliwa ili kumaliza janga kubwa la njaa ulimwenguni

Aidha, taarifa imeeleza kuwa watu Milioni 345 wanakabiliwa na njaa kali kwa sasa, hiyo ikiwa mara mbili ya hali ilivyokuwa mwaka 2019

Chanzo: DW Swahili
 
Hii siyo habari kwetu, huku tuna njaa miaka yote, tunaishi Kwa kudra za Mungu tu.
 
Sayari ipi hiyo watu wanakufa kila baada ya sekunde 4.?
 
Back
Top Bottom