Tahadhari ya utapeli mpya Dar kwa sasa

kuna siku kiduchu wale washenzi wauza tyre used wakidai mpya kwa bei cheee waniunguze....yaani walinilenga vema na ilikuwa time za Christmas unajianda service gari tukale mbege....wakanitokea ghafla, full package brand new tyre...nne...bei ilikuwa nafuu ajabu...na zangu zilikuwa choka hatarii...kuwauliza mmepiga wapi...wakanambia wanafanya kwa godown ya mhindi....nikajiuliza hizi toka vingunguti mpaka sinza wamekosa mteja kweli hapo kati???... walikuwa wako na bodaboda mbili....nikazichukua tyre...nikawambie twendeni pale kwenye mpesa nkawalipe....kwa pembeni ya mpesa wanaziba pancha.....nkawaambia jamaa wa pancha naomba mniwekee tyre zangu mpya......kwani najua wale jamaa waliondoka saa ngapi....kuzifunua ni chakavu hatari......wamezipack vizuri ajabu....na wengi weshapigwa kihivyo...
 
Pole sana.
 
Utakuwa na nyota ya kutapeliwa, ila tahadhari muhimu...
 
[emoji23][emoji23] kama unatapeliwa nchini mwako tu na sehemu unatumia usafiri dakika 20.basi naomba usijisumbue kufanya manunuzi ya ya nchi za nje.

bahati nzuri harufu ya utapeli na kujua huyu scammer or legit ni ndogo sana.

*shtuka swala la bei
*shtuka biashara ambayo kila dakika inafanyiwa promo
*shtuka kwa kujaribu kuona ile page je comment mbona ni chache au kutolewa kabisa na like nyingi.
jaribu kucomment hata kumwambia "mtakuwa matapeli" baada ya dakika itafutwa.
*jaribu kuangalia ni mda gani yupo kwenye soko na hata ku google namba yake na jina ili kupata kama
ana tatizo lolote .

mengine sitakupa ujifunze vzuri ukiwa unatapeliwa
 
Utapeli wa mabenki

Hapa ninachojiuliza ni kuwa .....Nina pesa nying kwenye account .....na hyo ni siri yangu...( kama kawaida wabongo kuficha siri kuhusu pesa zangu)
Je siku nikifariki ......benk inapeleka WAP ....fedha zanguuuu
Wewe ndugu zako watakuwa na death certificate na pia watakuwa na kiongozi wa mirathim mtaenda Benki husika au hata mitandao ya simu mtaomba kuchukua pesa za marehemu.
 
Utapeli mwingine upo kwa mawakala wa Nmb Crdb mnapo fanya malipo hakikisha kiasi kwa kupatiwa risit ya mashine ya Bank husika now watu wanaibiwa sana
Mkuu kwani wewe hujaiunganisha account yako ya bank na SIM banking? Mimi kila nikitoa lazima nipokee ujumbe kwenye simu ukionesha kiasi nilichotoa
 
Hiyo ya kuuziwa simu, bado ni tatizo kwa watu wengi hadi Sasa. Kuna jamaa aliuziwa na uncle wake kabisaa akampa na uhakika lakn kumbe anko alimwibia mwanajeshi. Kilichofata ni majonzi kwa familia
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna wale wazee wa Michenzani Zenji, wapo insta wanauza vitu bei chee...

TV ya 65", unapata jamaa wanauza 1mil hivi halafu kitu LG au Samsung, hahaha na ukiwapigia mnaongea fresh kabisa, sasa tuma pesa uone vumbi kwenye maji [emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kna mdada aliliwa lak 5 nch 45, alilia huyo nusu awe chizi
 
Duuuh hatareeeh sana.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…