Tahadhari za corona zinapuuzwa

Tahadhari za corona zinapuuzwa

pilau

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
1,595
Reaction score
451
Katika hali isiyokuwa ya kawaida maeneo mengi ya jiji la Dar wakazi wake wameacha au kupunguza kuwa na tahadhari na ugonjwa huu .... Watu hawavai barakoa watu hawànawi kama ilivyokuwa siku chache gonjwa likipopamba moto.

Mwanzoni ilikuwa tahadhari ipo kila mahala na hata ndani ya mabasi ya daladala abiria walikuwa wanalazimishwa kuingia na barakoa na baadhi ya daladala waalikuwa wanatoa sanitizer.

TAHADHARI Serikali iangalie tena uwezekano wa kufanya ukaguzi ili hata kama gonjwa limepungua pasitokee mlipuko.
 
Watu washasherehekea kuisha kwa corona ninyi bado mnapiga mayowe ya corona
 
Hata ITV jana kwenye kipindi cha malumbano ya hoja hakuna aliyevaa kama ilivyokua kawaida yao.
 
Bia yetu
Kwani yaliyoandikwa ni uongo? Hatukusali kwa siku tatu? Dar ilikuwa na siku tatu za kusheherekea mwisho wa Corona, haha kuwa na lockdown down sasa la uongo hapo ni Lipi?
 
Hiyo habari imepikwa sana na zito kwa Lengo la kuwafurahisha Mabeberu
Kwani yaliyoandikwa ni ubongo? Hatukusali kwa siku tatu? Dar ilikuwa na siku tatu za kusheherekea mwisho wa Corona, haha kuwa na lockdown down sasa la uwongo hapo ni Lipi?
 
Mlioko mijini, huu ugonjwa umeisha au bado upo!
 
Ukivaa wewe barakoa inatosha sio lazima kila mtu avae sawa fata maisha yako
 
Rais wa nchi huwa ana nguvu na ushawishi sana akizungumza jambo lolote.

Na kwa bahati mbaya sana Rais Magufuli ametumia ushawishi wake kuleta mikanganyiko kwa makusudi kabisa.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida maeneo mengi ya jiji la Dar wakazi wake wameacha au kupunguza kuwa na tahadhari na ugonjwa huu .... Watu hawavai barakoa watu hawànawi kama ilivyokuwa siku chache gonjwa likipopamba moto

Mwanzoni ilikuwa tahadhari ipo kila mahala na hata ndani ya mabasi ya daladala abiria walikuwa wanalazimishwa kuingia na barakoa na baadhi ya daladala waalikuwa wanatoa sanitizer.

TAHADHARI Serikali iangalie tena uwezekano wa kufanya ukaguzi ili hata kama gonjwa limepungua pasitokee mlipuko
Unategemea nini kuhusu corona wakati viongozi wakubwa wanajitapa kwa kutovaa barakoa kisa wameishinda corona. Huu ugonjwa tunauchukulia kisiasa lakini virus havina siasa. Tumekuwa watu wa kulazimisha kila kitu na kutofuata utaalamu ni hatari sana siku hizi.
 
Asante Yesu kwa kutusikiliza na kujibu maombi yetu., kwa kutuondolea hili pepo corona.

Matambara ya mdomoni hayana uwezo wa kumlinda mtu na corona. Ni kutapatapa tu.



JESUS IS LORD!
 
Hakuna mtu atakaye chukua tahadhari ya kitu ambacho hakiogopi au kisichoweza kumdhuru.

Na hakuna atakaye ogopa kitu ambacho anaamini hakipo au kama kipo basi hakiwezi kumdhuru.
 
KORONA inabidi ichague kimoja kati ya mambo haya, IONDOKE AMA TUHESHIMIANE 👽👽
 
Back
Top Bottom