Mkuu
Pasco,
Ufunuo au kupata insight kwa mkristo kupo kwenye Biblia na mtu hahitaji kufanya meditation ili aweze kufunuliwa, bali kwa kusikia Neno kwa usahihi, kulisoma na kwa kuomba ili Roho wa Mungu amwongoze katika kulielewa na kulitenda. Neno meditation kama lilivyotumika kwenye Biblia lina maana ya kutafakari kwa makini au kwa kina kuhusu jambo fulani "to think, conteplate, devise, ponder" sometimes to "sigh or murmur", Biblia haiwaambii watu wafanye practices kama alivyoonyesha
Mtambuzi.
Yesu hakufanya meditation (kwa jinsi mlivyoielezea) na wala hakuhitaji kwa sababu Yeye ni AllMighty: Omnipotence - All powerful, Omnipresence - He is not limited by time and space, He is everywhere at all times, Ominiscience - All Knowing.
Kwa mjibu wako au wengine meditation lengo lake ni kumpa mtu focus, insights na powers, Yesu ni Mungu na Nguvu, uwezo, mamlaka, insights zote zatoka kwake, na ni designer wa foci, sasa afanye meditation ili iweje? Ili nani ampe uwezo gani? He is infinite God.
Biblia inaposema mwanadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu unadhani maana yake ni kwamba anaweza kuwa na nguvu na uwezo kama Mungu? La hasha, nguvu za Mungu hata 1 over trillion mwanadamu hana. Mungu anaposema mwanadamu ameumbwa kwa mfano wake huhusianisha zaidi na mambo ya utakatifu - kwamba mwanadamu anaweza kuendelea kubadilika na kufanana naye kwa kuwa na utakatifu au ameumbwa na asili ya utakatifu kama alivyo Mungu na atakuwa mtakatifu kamili (kwa waliookoka) siku atakaponyakuliwa na kwenda mbinguni. Kwa habari ya nguvu Mungu amesema kila leo mwanadamu uwezo wake ni very limited.
Hauhitaji kufanya meditation kama ulivyoilezea ili kuijua kweli - Neno la Mungu ni kweli, and it's very apparent. Meditation ni imani, iwapo utaigeukia hiyo na kuacha imani ya Kikristo unamtumikia mungu mwingine na sio Mungu wa Biblia. Mtu anafunuliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu kupitia Neno la Mungu.
Na kuhusu habari ya kunena kwa lugha ni ishara ambazo zilifanywa wakati mitume wanasimika Neno la Mungu (wakati wanaweka msingi). Kwa sasa hizo huduma zimesitishwa, hazipo. Kunena kwa lugha sio kelele zisizokuwa na mpangilio wenye maana au kuongea lugha ambazo haziexist kama wafanyavyo watu siku hizi, bali ni mtu asiyejua lugha fulani kupata uwezo wa kuiongea kiufasaha na pia Biblia inasema katika kanisa wanaweza kunena wawili au watatu na lazima awepo mtu wa kutafsiri. Mfano mzuri ni siku ya Pentekoste, watu walinena kilugha kwa maana ya kuongea lugha ambayo hapo awali hawakuwahi kujifunza wala kuijua na watu wengine waliweza kusikia na kuelewa walichokuwa wakisema na kushangaa. Unakuta watu wanalia kanisa zima halafu milio kama ya wanyama na ndege huku hakuna mfasiri hata mmoja! Hiyo sio kunena kilugha ni drama/movie.
Mtu anapata Roho mtakatifu pale tu anapompokea Kristo. Wokovu, kupokea Roho mtakatifu, kusamehewa dhambi; vyote vinatokea concurrently.
Kuijua kweli ni kupitia Neno la Mungu na si vinginevyo. Na Neno la Mungu linasema ukiwa na Imani ndogo tu kama punje ya haradali unaweza hata kuhamisha mlima (hiyo nguvu umeiongelea)! Unaona kwamba haya mambo yanafanyika kwa imani. Sawa imani inaweza kuwa ni ya giza au mwanga kama ulivyosema.
Meditation ni "cult", ni kitu kinachooshiria imani nyingine, inahusisha alteration of mind na kucreate scenes ya mambo ambayo hayapo, badala ya kumfanya mtu ajitambue inamfanya awe convoluted kwa sababu anakuwa subjected to an environment where he/she does not fit naturally.
Meditation ni dini/imani
"Meditation has been practiced since antiquity as a component of numerous religious traditions and beliefs.[SUP]
[6][/SUP]" - wiki.
"The history of meditation is intimately bound up with the religious context within which it was practiced." - wiki
Kuna references nyingi including vitabu vinavyoelezea how meditation the way you have stipulated is a religion/belief system. Kama nilivyosema, meditation, scientology, wicca, spell, magic, witchcraft ni intermingled practices in the sense that they borrow from each other!
Labda
juve2012 na
2013 wana mchango wao kuhusu hili