TAHAJUDI (Meditation): Mbinu, faida, aina na mambo ya kuzingatia

TAHAJUDI (Meditation): Mbinu, faida, aina na mambo ya kuzingatia

Before you join the party...Fahamu kuwa ''meditation" is a Cult. pia na zaidi ya yote ni Anti-God. kama unaamini uwepo wa mungu ipo siku utaacha dini yako.
fanya utafiti binafsi.
Hapana not Anti-God but true God, ni journey ya kudiscover our true self, its a spiritual path. Kwa wakristo hata Jesus alikua akipractice meditation that's why alikua akienda sehem tulivu mlimani
 
Kijana unaelewa kusoma? Mimi siongeleai "meditation"naongelea Tahajjud.

Wewe baki na "mefitation" yako, wacha mimi nibaki na Tahajjud yangu. Tatizo lako nini?
Sina tatizo na wewe ila hili ni jukwaa la kijamii sio jukwaa la mtu na Mpnz wake chumbani , ukisema neno lako humu umeshaweka uhalali wa kila mtu kutoa mawazo yake ata kma yapo tofauti na mtizamo wako, bila kuvunja sheria za hi forum.
 
Wewe base upendapo nami na base nipendavyo. Unataka mimi niwe kama wewe? Mimi ni Muislam na Uislam umekamilika hauhiytaji msaada wa wamufundisho ya dini yeyote ile ya kuabudu binaadam.
Sina tatzo na uislamu,unataka kujumuuisha dini kubwa hivyo natatizo lako la kiakil? Uislamu umekamilika bila hata wewe kudhibitisha .
 
Sina tatzo na uislamu,unataka kujumuuisha dini kubwa hivyo natatizo lako la kiakil? Uislamu umekamilika bila hata wewe kudhibitisha .
Safi sana.++
Salat Tahajjud unaifaham?
 
Meditation (uliyoilezea wewe) ina mchanganyiko wa vitu ambavyo vingine vinaweza kukubalika kwa imani ya kikristo, mfano to calm yourself, think deeply, sit in a quite place to read a Bible or pray, kutenga muda kila siku kumeditate with the God our Father. Katika ukristo kwa kifupi meditation ni kutenga muda katika hali ya utulivu "quite time" kwa nia ya kucommunicate na Mungu kupitia maandiko, maombi au tafakari ya aina yoyote kuhusu Mungu au Neno lake. Hii ndio meditation inayoelezewa kwenye Biblia.

Lakini meditation unayoielezea Wewe na Mtambuzi inaembrace na kuborrow a lot from paganism, in that sense the whole thing ni paganism, kwa sababu Neno la Mungu halitaki mchanganyiko.

CC Pasco
Wewe jamaa una uwezo mdogo sana.
 
Machale..... ndio maana naona wanaofanya meditation kama wanga.
Kuna jamaa yangu Rodrick Ntepa aliniambia kaanzisha dini yake inaitwa WANAZARAYO. Na yeye ndiye Mungu wa dini hiyo. Akanifundisha ku meditate. Tulimeditate kwa masaa matatu none stop. Yeye akaniambia alishawahi kumeditate hadi akawa kama mfu. Na siku hiyo alikuwa ameenda kwenye mbingu ya saba ambako anakaa Mungu wa Wakristo.
Noma sana
 
Machale..... ndio maana naona wanaofanya meditation kama wanga.
Kuna jamaa yangu Rodrick Ntepa aliniambia kaanzisha dini yake inaitwa WANAZARAYO. Na yeye ndiye Mungu wa dini hiyo. Akanifundisha ku meditate. Tulimeditate kwa masaa matatu none stop. Yeye akaniambia alishawahi kumeditate hadi akawa kama mfu. Na siku hiyo alikuwa ameenda kwenye mbingu ya saba ambako anakaa Mungu wa Wakristo.
Chai...
 
■ BASIC PRINCIPLES OF AWAKENING. (Kanuni kuu za kuamka)

Inafurahisha kuona watu wengi wanaachana na zama za zamani (Pisces ages) zama za kuamini na kuingia katika zama mpya, zama za kuelewa zama za mmwagiko wa maji (aquarius Ages)

Kwa kuwa bado kuna athari za mfumo wa zamani kwenye mfumo mpya, watu wengi hata wakisoma mafundisho yenye nia ya kuleta utambuzi na mwamko wa kiroho, mafundisho hayo hugeuka kifungo, kufuri na minyororo kwa wengi wanaoitafuta nuru kwa sababu ya kutozingatia baadhi ya mambo muhimu.

Ndio maana nashauri usomapo mafundisho haya, uyasome ukiwa katika mazingira safi, usiwe na stress na usisome kama gazeti bila kutafakari kilichoandikwa. Usomapo uwe katika hali ya utulivu wa akili ili kuepuka kufungwa na maandiko usomayo.

Vitendo(mazoezi) vingi vinavyoleta uamsho wa kiroho uhitaji kuituliza akili ili kukuletea uamsho(enlightenment), mfano wa vitendo hivyo ni Meditation, astral projection, kufungua jicho la tatu, kubalance chakras n.k vitendo.

Zifuatazo ni PRINCIPLE/kanuni chache za kuzingatia ili uweze kuitawala Akili yako na kuzuia mawazo yako, mbinu hizi pia zitakusaidia kuvuka vikwazo vya meditation na mazoezi mengine ya kiroho.

[emoji746]Ukitaka kufanikiwa katika jambo lolote la kiroho, kwanza kabisa usijiwekee matarajio yoyote baada ya kujifunza, kujiwekea matarajio ni moja ya kifungo kikubwa kitakacho kuzuia kufanikiwa. Mambo ya kiroho yapo zaidi ya kikomo cha akili, huwezi ku-experience mambo ya kiroho kwa akili ya kawaida, ni tabia ya akili kufikilia yaliyopita na yajao. Kitu muhimu ni kuwa wakati uliopo (NOW).

[emoji746]Tangu tukiwa watoto tumefundishwa kufanya vitu kwa kufikiria na kwa umakini mkubwa ili tuweze kufanikiwa kuvipata, lakini mafunzo hayo hayafanyi kazi kwenye maswala ya kiroho. Kwenye mambo ya kiroho hutakiwi kuongeza umakini, hutakiwi kujilazimisha ili uliyojifunza kipate kuonekana.

Usianze kutathimini kinachotokea, usichanganue chochote, usipige hesabu saivi nimefikia hatua ipi ukiwa katika zoezi la kiroho bali uwe na ufahamu wa kinachoendelea (just Be Aware).

Kwanza yakupasa kusahau kila kitu. Inshort akili yako haitakiwi kufanya kitu chochote (bali uwe na ufahamu-just be aware). Pale utakapothubutu kuongeza umakini,kuchanganya au kujilazimisha kuituliza akili hutafanikiwa, sababu bado utakua unatumia akili yako kuituliza akili.

Acha vitu vitokee vyenyewe, acha vitu vijidhihirishe vyenyewe kisha uende navyo kama vinavyoenda
...Just be aware, and everything will happen...

[emoji746]Kupatwa na picha za kufikirika (imaginations) ni kitu cha kawaida kutokea Katika mazoezi mengi ya kiroho i.e kufungua jicho la tatu. Lakini wewe uwapo katika mazoezi ya kiroho Kamwe usijaribu wala kuthubutu kuvuta picha, kuruhusu maono au ku-imagine kitu chochote, narudia tena usithubutu, ukifanya hivyo utakua unatumia akili yako.

Remember: akili haiwezi kukuelezea kile kilichopo baada ya ukomo wa akili, ni ufahamu wako pekee ndio huweza. Ufahamu (consciousness) huanza kuonekana pale akili ikinyamazishwa.

Siku ukipatwa na maono,taswira au imaginations zilizotokana na ufahamu wako pekee bila ya uwepo wa akili, utashindwa kutofautisha na maono yako ambayo huwa unayatengeneza kwa akili yako.

Kumbuka mawazo(thoughts) ni sehemu ndogo sana ya Ufahamu, mawazo ni sehemu ya akili. Akili(Mind) na Ufahamu(consciousness) ni vitu viwili tofauti kabisa. Akili haiwezi kuwepo bila ya ufahamu, ila ufahamu unaweza kuwepo bila ya Akili.


Unachotakiwa kufanya ni kufanya zoezi, halafu uache mambo yaje yenyewe bila kuyalazimisha, just be aware

[emoji746]Trust your process, Trust your Experience.
Jiamini katika kila ufanyacho, amini unachokipata au kukipitia kuwa ni sahihi hata kama haiendi sawa kama ilivyoandikwa kwenye kitabu au kama guru (mwalimu) wako alivyokufindisha.

Si mnatambua kuwa mwalimu mkuu wa safari ya kiroho ni wewe mwenyewe.
Badala ya kufanya kama buddha , imekupasa kuwa buddha, uamke.

Maana yake kila hali utakayoipitia itakua ni kweli sababu wewe mwenyewe ndiye buddha na huna haja ya kujali chochote
...when there is nothing tobelieve, there is nothing to doubt either...

[emoji746] PRACTICE, PRACTICE, PRACTICE .
Anza kufanyia mazoezi baada ya kujifunza, ukisema utajifunza kesho maana yake hutafanyia mazoezi kamwe.

"...In terms of self-transformation, tomorrow means never..."

Unaweza ukawa bize sana kiasi cha kuona hutoweza kufanya mazoezi mbali mbali, ubize wako au maisha yako binafsi yasiwe kikwazo katika kuamka kiroho.

Watu wengi walioamka walikutana na vikwazo vingi vya kuwazuia kufanya mazoezi, lakini kutokuacha kwao (supernatural persistence) ndiko kulikowaletea uamsho(ENLIGHTENMENT)

Mazoezi ya kutuliza akili hayahitaji uache shughuli zako za kila siku, bali inatakiwa uendelee na shughuli zako ukiwa na ufahamu ,fanya shughuli zako ukiwa katika hali ya sasa(NOW).

[emoji746] Kuithibiti akili(mind controlling) ni kiini kikuu cha meditation, huwezi pata matokeo ya meditation ikiwa utashindwa kusimamisha mtiririko wa mawazo. Haya ni maandalizi ya awali ya namna ya kudhibiti Akili.


■ MIND CONTROL (SEHEMU YA PILI)
[emoji2936] NA Olyme Songo III

Maisha yamekua fumbo pale utakapojiuliza baadhi ya maswali mbali mbali kuhusu wewe, haswa utakapo jiuliza "mimi ni nani ?", Nimetokea wapi ?, nipo hapa kwa kusudi gani ? Na pale akili yako ikianza kupata majibu baadhi ndipo utajiuliza ni nani chanzo cha haya yote.

Ukiwa mtu wa dini huwezi kufika hata hatua ya kujiuliza maswali hayo sababu imani haitaki maswali, hata ukiuliza mnapewa majibu yasiyo na fact yoyote ila yatazidi kukufanya uendelee kuamini.

Kwa wengi maisha yanaonekana ni fumbo lakini kiuhalisia sio fumbo kwa maana tafsiri ya maisha hutokana na Intelijensia(/intelligence) yako, uwezo na upeo wako wa kuelewa.

Sababu inayofanya maisha kuwa fumbo ni kwa sababu baadhi ya vitu muhimu havipo wazi kwako na vitu visivyo halisi vimefanyika halisi kwako. Uwezo wa kuelewa kuhusu maisha hutofautinana kwa mtu mmoja hadi mwingine kutokana namna gani mtu huyo amefanikiwa kuyajua yale aliyofichwa na kutambua yote yasio halisi.

Wengi wetu humu, tunamjua adui wa nje, tunajua Mfumo maisha usio halisi(Matrix) ndio unaofanya hali inakua hivyo, mfumo fake unaongozwa na watu wachache ambao wanacontrol nyanja zote muhimu, nao wameishika dunia.

kizazi cha reptilia ndio kinadidimiza safari yako ya utambuzi kwa mbinu za hali ya juu (tricknology) kwa kutumia mbinu zinazowawezesha kuikamata akili yako.

Lakini yupo adui mwingine aliye ndani yako mwenyewe ambaye ametengenezwa na huyo adui wa nje unayemjua(reptilia bloodline).

Kwa kutumia tricknology watawala wa dunia hii wamefanikiwa kuigeuza akili yako kuwa adui yako na kukusababishia uharibifu , ingawa akili ikitumiwa kwa usahihi ni kitu kizuri mno sana.

Kwa maana akili ni kakitu kadogo sana katika ufahamu/intelijensia kanakotusaidia kutufanya tusiwe kama wanyama, maana bila ya akili nasi tungekua ng'ombe kama ng'ombe wengine.

Amin amin nakuambia, akili (mind) yako ni moja ya adui yako mkubwa katika safari yako , na ndio maana adui wa nje hufanya kila kitu ili kudhibiti utendaji kazi wa akili(Mind) yako.

Kwenye maandiko ya wanubia ya holy tablets wa viumbe jamii ya satanist ndio viumbe wabaya wanaotafuta control minds(akili) wakishirikiana na wa luciferians ambao ucontrol energy(nishati) na hao ndio wanaohusika na udanganyifu.

Umefanyika mtumwa wa akili yako mwenyewe, tena usipotaka kuamka, utakua mtumwa wa kifungo cha maisha, mpaka unapokufa. Badala ya kuiongoza akili yako, akili ndo inakuongoza wewe.

Muda wote akili (mind) hukupigia kelele na kushindwa kuisikia ujumbe kutoka utu wako wa ndani ulio uhalisia wako. Muda wote akili inawaza, inawaza hili haijamaliza hili inawaza jambo lingine.

Najua umeshawahi kumwona kichaa, kichaa muda wote huongea kwa sauti maneno mengi bila kuongeleshwa na mtu au kumwambia mtu. Kusema kweli hivyo ndivyo na sisi tulivyo isipokuwa sisi hatuyaongei kwa mdomo yakasikika.

Sauti usikiazo kutoka kwa kichaa hayo ndiyo mawazo yake yatokayo katika akili(mind).
Akili hutuwezesha kufikiri,kuwaza lakini ubongo ndio unaowezesha majukumu yote ya akili
Mawazo yetu hutoa maoni, kasoro, kommenti, hukumu, ufanano, sometimes hupenda au kuchukia n.k.

Na wakati mwingine mawazo huja katika mfumo wa picha, yaani "imagination" lakini cha ajabu mawazo hayo huwa hayahusiani na muda au mazingira uliyopo, bali kila kitu unachowaza hutokana na wakati uliopita.

Hata kama mawazo yako yatahusiana na kinachoendelea muda huo ni lazima yatatafsiri kinachoendelea kutokana na mambo kadhaa yaliyopita.

Unaweza ukawa unakula na ukasema chakula ni kitamu, lakini tafsiri ya utamu inatokana na ladha mbali mbali za hapo awali. In short mind haijawahi kukaa katika hali iliyopo(present moment)

Kwa wanaofanya meditation nadhani tunaelewana, dakika chache za mwanzo mawazo hukatiza sana katika ufahamu wako, na lengo kuu la meditation ni kukuwezesha kutuliza mawazo yote ambayo ni kelele kwenye utu wako wa ndani (higher self), na kuacha ukimya.

Na pale unapokuwa umetuliza akili yako kuwa kimya unakua umejiunganisha na uhalisia wako, utu wako, present only neither past nor future
Hapo unakua haubughudhiwi na FUTURE(wakati ujao) wala PAST (wakati wako uliopita) maana yake unakuwa katika PRESENT (wakati uliopo).

Ukiichunguza akili(mind) yako, utagundua muda wote hukuletea mawazo yanayohusu wakati uliopita au wakati ujao. Mara mpenzi wangu kaniacha mara nitajenga nyumba, mala baadae nitakula nini, yaani ni kelele mwanzo mwisho.

Naam hiyo ndio kazi ya akili(mind), akili hupenda kufikiri.
Kamwe huwezi kujiunganisha na utu wako wa ndani au kui experience hali iliyopo(NOW/PRESENT) kama utakua unatumia akili.

Kufikiri/akili sio sawa na ufahamu(consciousness) au fikra haiendani na ufahamu, fikra haziwezi kuwepo bila ya ufahamu, ila ufahamu unaweza kuwepo bila ya kufikiri(/akili)

Hata ukiwa unafikiri na kutafakari ili kutatua tatizo unaweza kujihisi unatumia akili kutatua matatizo yako, my brothers and sisters you are completely wrong, Akili hupenda kufikiri, kuwaza na kuwazua yaani ni kama vile mbwa apendavyo kutafuna mifupa.

Na kamwe ufanyavyo hivyo hautumii akili, bali akili ndiyo hukutumia wewe, yes it uses you, sababu umefanyika mtumwa wa akili yako mwenyewe, mfano rahisi ni mtu aliye athirika na pornography, yaani huyo akili inamtumia nje nje bila kificho naye kwa utiifu humtumikia master wake.

Bila akili unapoteza utambulisho wako(identity) sababu akili ndio iliyokupa utambulisho, na utambulisho huo ni fake sio halisi(delusions-maluweluwe) utambulisho wako halisi utautambua pale utakapoizuia akili iache kufikiri.

Na ndio maana wataalamu husema kiwango cha juu cha meditation ni kutofikiri kuhusu chochote.

"The highest level of meditation is to think nothing"

Akili hupenda kufikiri kuhusu yaliyopita na yajayo, na ukiona inakuwia vigumu kuzuia kuwaza yaliyopita au yajayo, hapo sasa ndo unielewe nilivyosema kuwa " huwa hautumii akili bali akili ndo huwa inakutumia wewe", Unajua kwa nini?

Kwasababu identify yako, utambulisho wako uliupata baada ya kuiruhusu akili yako ikutumie kwa sababu wewe u mtumwa wa akili yako, nayo akili, ikakuambia wewe ni mariamu, wewe ni masikini, wewe ni mrembo, wewe unapendwa sana n.k kwa sababu yenyewe imefanyika bwana wako(slave master)

Lazima uone kama haiwezekani kukaa bila kufikiri chochote, sasa ukiizuia akili yako wewe utakuwa nani? maana yake utakuwa si chochote, ukuu wako, cheo, title yako hapo mtaani na identify zako zote ulizopewa na akili zitapotea.

Je ukiizuia akili wewe utabakia nani? (Without mind, who are you?) Bado akili itapenda kuwaza yajayo ili kujihakikishia maisha ndani yako.

Amini amini nakuambia, ukizuia mawazo yako (-ya nyuma na yajayo-) hapo ndipo mwanzo wa kujitambua wewe ni nani, Na hiyo ndio huitwa ENLIGHTENMENT na wanadini ya kibudha.

Na ndo maana Wabudha husema kwamba, "kuangaziwa ni mwisho wa masumbuko yote."

"Enlightenment is the end of all suffering"

Kwa sababu mateso na masumbuko yote yanatokana na Mawazo yetu,fake identity tulizopewa na akii zetu.
Maisha sio fumbo hata kidogo, watu wanaoshindwa kuishi PRESENT, kamwe hawajawahi kupata furaha ya kweli, amani ya kweli, upendo wa kweli.

Yaani wamejawa na maumivu kila sehemu, pain every where, ndoa hazina raha, ndoa hazina upendo. Hata kile mnachoita upendo sio upendo huo ni delusion, baada ya muda (euphoria period) penzi linakufa,

Why?

Upendo, furaha, amani vyote vipo ndani yako mwenyewe, tatizo lenu mko bize kutafuta upendo kwenye mahusiano, furaha kwenye mali na pesa na kamwe hamjawahi kuupata huo upendo,furaha na amani yaani pain everywhere.

■ MIND CONTROL (Sehemu ya Tatu)
[emoji2936] NA Olyme Songo III

Kabla hujataka kuithibiti/control akili yako ni lazima kwanza uijue kisha uzaliwe ufahamu mpya juu ya namna ya kuithibiti akili ili kuepukana na utawala wa MATRIX ambao hutumia akili,mind control kama nyenzo kuu ya utawala.

LET'S BEGIN...
Utakuwa umepiga hatua kubwa kama tayari umeanza kutambua kuwa akili ina asilimia ndogo sana kuweza kukueleza wewe ni nani?

Pia kama utakua unatambua utambulisho wako halisi sio huu utokanao na akili, bali utambulisho wako halisi (-ambao ndio uhalisia wako-) unatokana na sehemu kubwa ya ufahamu(intelijensia) isiyo na kikomo /utu wako wa ndani (inner being)/ higherself.

Sasa tunaendelea kuipambanua AKILI katika vipande vidogo ili kila mtu aweze kujua akili ifanyavyo kazi,sifa na tabia zake.
Ukiijua namna akili ifanyavyo kazi, MEDITATION haitakuwa kikwazo tena kwenye maisha yako.

Watu wengi wanatamani kujifunza zaidi kuhusu meditation, nipo pamoja nanyi mpaka mwisho, na tukimaliza kujifunza kuhusu Akili, nitakushirikisheni vitu vichache kuhusu meditation ( Meditation Hints) nawe utainuka na kusimama tena, kisha kusonga mbele katika safari yako ya maisha yako.

Katika sehemu iliyopita tumeona kazi kuu ya Akili ni kukupa mawazo yasiyoisha, kwa kupendelea zaidi kuwaza kuhusu wakati uliopita, PAST na wakati ujao, FUTURE na kushindwa kabisa kutulia kwenye wakati uliopo, PRESENT.
Lakin leo tutatazama zaidi kuhusu HISIA ambazo ni sehemu mojawapo ya utendaji kazi wa akili.

Mawazo yanauwezo wa kuleta athari katika mwili wako(-body biochemistry-), yanaweza kuwa ni mawazo ya muda mfupi au muda mrefu juu ya jambo fulani, sasa mwili unapoathiriwa na mawazo kitu kipya huzaliwa na kitu hicho sio kingine bali ni HISIA, EMOTIONS. Na wataalamu wengine husema hisia huibuka pale akili na mwili vinapokutana.

"Emotions arises at the place where mind and body meet"

Baadhi ya utendaji kazi wa akili usioweza kuutambua (unconcious mind activities) hujidhihirisha katika mwili kama Hisia. Hapo unaweza ukawa unawaza kitu fulani bila hata ya wewe kutambua kuwa unawaza nini, hapo ni akili inachakata mambo bila wewe kutambua moja kwa moja.

Unaweza kupatwa na mawazo baada ya kutishwa juu ya kitu fulani na ukanyong'onyea kimwili na kisaikolojia, hiyoo ni HOFU. Au unaweza kushambuliwa kifikra, kimaneno au vitendo nawe ukipatwa na hisia fulani za kutaka kupambana na shambulizi, hizo ni HASIRA

Ukijitathimini au kujichunguza pale upatapo Hisia either hisia za hasira, hofu, chuki, raha n.k utagundua hisia sio chochote bali ni nishati au nguvu fulani inakuwa inatiririka katika mwili wako.

Na huo ndio udhihirisho wa akili katika mwili wako/Reflection of mind in body/body's reaction to Mind = EMOTIONS yaani HISIA, E-MOTION ambayo ni sawa na "Energy in Motion", ikiwa na maana nishati(nguvu) katika mwendo.

Jijengee tabia ya kujichunguza akili yako pale ukumbanapo na hali tofauti tofauti za maisha, utagundua mengi kuhusu wewe.

Sasa vuta pumzi kubwa ndani kisha nisikilize vizuri. Jamii inayotuzunguka, elimu na Matrix kiujumla vimetufundisha kwamba kuna hisia hasi na hisia chanya kama upendo, furaha n.k
Lakin kiuhalisia hisia zote, chanya na hasi zinatokana na utendaji kazi wa akili.

Lakini furaha, upendo, amani ya kweli sio hisia chanya na wala, hazitokani na akili bali hutokana na utu wako wa ndani unaopatikana baada ya kunyamazisha kelele za akili na kuwa katika wakati timilifu uliopo ambapo unakuwa haufikiri chochote bali unakua umeunganisha na utu wako, inner being ambao ndio utambulisho wako halisi.

Na wengi wetu tunapambana kutafuta hisia chanya tukidhani ni kitu kizuri kumbe bado ni akili yako inaendelea kukutumia na kukutawala.

Upendo, furaha ya kweli hutoka ndani yako mwenyewe kamwe haiwezi kukupa maumivu ila hisia zote, ziwe mbaya au nzuri, iwe ni upendo fake, amani fake itokanayo na akili huleta MAUMIVU/PAIN.

Huwezi kupata upendo, amani furaha ya kweli kama haujaweza kuicontrol akili yako. Amani ya kweli sio hisia, amani ya kweli haiwezi kukupa maumivu, amani ya kweli inapatikana baada ya kuvuka kikomo cha akili.

Wewe mwenyewe unaweza kuwa shahidi, kuna nyakati/moments huwa zinatokea mara moja moja sana, accidentally ambapo unaweza kupatwa na furaha au amani au upendo kutoka ndani yako na ukabakia umeduwaa kwa sekunde chache kisha furaha/amani/upendo wako wa kweli unatoweka baada ya akili kuendeleza kazi yake ya upigaji kelele kwa kukupa mawazo yasiyokwisha.

Hisia ni sehemu mojawapo ya utendaji kazi wa akili ya uwili uwili, dualistic mind, inamfumo wa kinyume/opposite, kwenye hisia nzuri basi kuna hisia yake mbaya. Na matrix imewaaminisheni kwamba raha ( pleasure) ndiyo furaha, kiuhalisia huitwa furaha kimakosa.

Siku zote FURAHA inatoka ndani yako lakini RAHA inatokana na vitu nje yako(either mpenzi, chakula kizuri, mandhari nzuri). Kitu kinachokupa raha, furaha, amani leo pia kinaweza kukupa maumivu kesho ndo maana ukiwa mbali na mpenzi, au mpenzi akikuacha lazima upate maumivu. Furaha, amani, upendo wa kweli sio hisia bali hutoka ndani yako mwenyewe na sio nje yako.

Sometimes akili hupingana na hisia, unajua ni kwa nini? Ni kwasababu akili hukupa mawazo kutokana na mazingira yanayokuzunguka(ie break up, kulipa kodi, msiba n.k) na pale mawazo hayo(ambayo ni matokeo ya utendaji kazi wa akili) yakijidhihirisha katika mwili, hukupa kitu kipya ambacho ni hisia. Hivyo mawazo na hisia ni vitu viwili vinavyotokana na utendaji kazi wa akili.

Ila wahenga husema pale hisia na akili vinapopingana ni vema kufuata hisia zako sababu mara nyingi mawazo yatakua ni uongo na hisia zitakua ni kweli. Na huo ukweli sio ukweli halisi sababu bado unatokana na akili.

Siku zote mawazo na hisia hutegemeana ili kuendelea kuishi, ili kuendelea kukutawala.
Akili hukupa mawazo, mawazo huzalisha hisia, na kadri hisia zinavyozidi ndivyo mawazo huzidi sababu mawazo hulishwa na hisia. Hapo hutokea mzunguko usio kwisha, vicious circle builds up.

Akili, mawazo na hisia vina endelea kukutumia, kukupa maumivu yasio na mwisho. Maumivu hayakwepeki kama utambulisho wako unatokana na akili, na akili kamwe haiwezi kukupa suluhisho la maumivu uyapatayo sababu kazi mojawapo ya akili ni kupambana kuondoa hisia za maumivu.

Ni sawa na kumpa askari kazi ya kupambana na uhalifu ilihali yeye pia anahusika kwenye huo uhalifu au ananufaika na huo uhalifu. Mbaya zaidi kadri akili inavyopambana kuondoa maumivu ndivyo maumivu uongezeka.

"The harder the mind struggles to get rid of pain, the greater the pain"

Suluhisho pekee la kuondokana na masumbuko ya mawazo, hisia, na maumivu ni kuinyamazisha akili yako, ili kujiunganisha na utu wako wa ndani, au kujiunganisha na uwepo wa sasa.

■ 3.MIND CONTROL- MEDITATION ESSENCE (Sehemu ya Nne)
(Uthibiti wa akili - kiini cha tahajudi)
[emoji2936] Serpent Brotherhood is Watching [emoji2539]

Kujifunza zaidi kuhusu akili hakukufanyi uangaziwe (enlightened) bali hukufanya kuwa mwanasaikolojia mzuri.

Katika sehemu zilizopita tumejifunza zaidi kuhusu namna ambavyo akili hututawala na kututumia kwa manufaa yake na wanaoithibiti (Reptilians), tuliona akili hutumia MAWAZO(THOUGHTS ) NA HISIA(EMOTIONS) ili kukupa utambulisho usio halisi unaokuzuia kuutambua uhalisia wako (your Being) na matokeo yake unafanyika mtumwa wa mitetemo ya chini ya ulimwengu wa 3D ili hali kuna uhalisia halisi pale utakapoithibiti akili na kuyazima mawazo yako na kuingia katika hali ya ufahamu isiyo na kufikiri (state of No mind).

Kwenye mwili wa binadamu, ubongo ni kiungo tata (complex organi) kukielewa, vivyo hivyo, akili nayo ni tata kuielewa. Kuwa na maarifa mengi zaidi kuhusu utendaji kazi wa akili ni jambo jema sababu litakufanya uwe mwanasaikolojia mzuri, lakini halitakusaidia kuidhibiti akili yako au kuyazuia mawazo yako ili uweze Kuamka/kufikia kiwango cha juu cha meditation na kui-experience/kuipitia hali ya sasa(power of Now).

Leo tutaangazia mbinu mbili za uthibiti akili, lakini Kabla hujaanza kufanyia mazoezi mbinu hizo haitakiwi uweke matarajio yoyote, tena ufanyapo usifikiri chochote kile kwa umakini, usilazimishe kupata matokeo uliyojifunza, usifanye tathmini wala mchanganuo wa kinachoendelea, usitengeneze taswira/imaginations zozote, yakupasa usahau kila kitu ulichowahi kujifunza kuhusu uthibiti wa akili ili uweze kufanya zoezi kwa ufanisi ukiwa na ufahamu wa sasa hivi.

Ukweli ni kwamba, kitu kiletacho kuzaliwa upya kiroho (uamsho-enlightment) sio kile unachokiamini au kukipokea kama Ukweli, bali uamsho wa kiroho hutokana na kile unachokipitia(experience) kwa wakati huo, hivyo basi, Acha vitu vitokee vyenyewe, acha vitu vijidhihirishe vyenyewe kisha uende navyo kama vinavyoenda, kuwa na ufahamu na kila kitu kinachotokea, jiamini kuwa matokeo uyapatayo ni bora na wala hamna ulipokosea hata kama haiendi kama ilivyoelezwa au kufundishwa, kwa sababu mwalimu mkuu katika safari yako ya kiroho ni wewe mwenyewe, na uamsho wa kiroho hutokana na kile unachokipitia(experience) wewe kwa wakati huo na sio ulichosoma au kusimuliwa na Guru, Mwalimu, Buddha, Muhammad au Yesu.

Usifuate matakwa ya Mungu, Kuwa Mungu. Kama ulikua hujui mungu ni cheo tu kama vyeo vingine, na ile nguvu kuu ya asili iliyo chanzo cha vyote imepewa cheo cha mungu na watu wa dini, lakini wamekuja kuharibu baada ya kuwasilisha sifa kuu ya nguvu kuu ya asili kwa mtu wa kufikirika aliye mfano wa mwanadamu, mwenye ndevu nyingi akaaye mbinguni.

Yote kwa yote mambo ya Ngoswe tunamwachia Ngoswe, mambo ya dini tunawaachia wanadini. That's why sometimes I used to call myself GOD OF QUANTUM, GOD OF STORIES, sio kwa sababu nina EGO, No!! ONLY BECAUSE EYE CAN SEE.

"Spiritual regeneration comes from what you experience and not what you believe."

LET'S US BEGIN.

I: WATCHING THE THINKER.

Kama umeshawahi kumuona kichaa anayejiongelesha maneno mengi bila kusemeshwa na mtu basi utaenda kunielewa vema kabisa. Katika maneno mengi atoayo kichaa, kuna maneno yanayonesha hofu, kuchukizwa, kupendezwa, maoni, malalamiko n.k, na mara nyingi maneno atoayo huwa hayahusiani na wakati uliopo, bali wakati uliopita, na wakati ujao.

Na hata maneno atoayo yakihusiana na wakati uliopo ni lazima yatakua yanatafsiri wakati uliopo kutokana na nyakati zijazo au zilizopita. Sasa hayo maneno atoayo ndiyo mawazo yake, na mawazo (thoughts) hayo hutokana na akili iliyotengenezwa tangu utoto (conditioned mind).

Sasa nini tofauti ya kichaa anayeongea bila kuongeleshwa na wewe? wewe hauongei mawazo yako kwa sauti, lakini kichaa huongea mawazo yake kwa sauti, sababu kichaa haoni tofauti ya kisicho halisi na kilicho halisi, that's why huwasilisha mawazo yake kwa sauti tofauti na wewe ambaye huyaacha mawazo yako kichwani mwako, mawazo yako yanakuwa kama sauti zinazosikika katika kichwa chako, kichwani mwako kunakuwa na mazungumzo yasiyokwishwa.

Hivyo ndivyo akili hukutawala, hivyo ndivyo akili hukupigia kelele.Lakini usije ukajaribu kwenda hospital ukajieleza eti unasikia sauti kichwani mwako, my friend punde si punde utajikuta upo Mirembe [emoji541].

[emoji1630] HOW TO STOP MONKEY MIND[emoji205]. ( Namna ya kusimamisha akili iliyo kama nyani.)

Si unajua namna nyani anavyoruka-ruka kwenye miti, hawezi kutulia kwenye tawi moja, hivyo ndivyo ilivyo akili iliyo kama nyani, haijamaliza kuwaza hili linakuja wazo lingine,nalo halijaisha linakuja lingine tena na tena na tena[emoji3536].

Suluhisho la kusimamisha mawazo ni kumtazama anayewaza (Watching the Thinker). Anza kuzisikiliza hizo sauti kichwani mwako kadri uwezavyo, kadri unavyopata nafasi. Na hiyo ndiyo maana ya kumtazama anayewaza.

Kitendo cha kusikiliza sauti (kumtazama anayewaza) baada ya sekunde chache utapata utambuzi kuwa kuna SAUTI afu kuna MIMI ninaisikiliza sauti, ukishajihisi kuwa upo kusikiliza sauti hapo utakua umejipata, umepata uhalisia wako au utu wako (inner being).

Utambuzi wa utu wako unatoka sehemu ya mbali ya ufahamu iliyo kikomo cha akili yako, Utambuzi huo hautokani na akili yako bali UFAHAMU, tena ufahamu ukiwa umejitenga na akili.

Si mnakumbuka nilisema mawazo(mind) ni kitu kidogo sana katika ufahamu(consciousness), Ufahamu hauna kikomo kama ilivyo 9 ether. Kwenye masomo yahusuyo nishati, nilishawahi kutoa point isemayo "9 ether is consciousness".

Ukiwa unasikiliza sauti hizo yakupasa usimame kama mtazamaji tu, usitoe hukumu,usipendezwe wala kupendezwa na sauti/wazo lolote either liwe baya au zuri. Kitendo cha kuanza kutoa maoni au kujudge kutakuvuta tena na kuruhusu akili kukuvamia tena kwa mlango wa nyuma.

Pale unapoyasikiliza mawazo yako unakuwa na ufahamu wa mawazo yako na ufahamu wa utu wako, yaani ufahamu wa wewe halisi usiye na utambulisho utokanao na dunia bali na ufahamu mkuu(super conciousness).

Kumtazama anayewaza/kusikiliza mawazo yako kunayafanya mawazo kupoteza nguvu zake na baadae kutokomea na kubakia katika hali ya kutokuwa na fikra(thoughts/mawazo)/NO MIND.

Ukiwa katika hali ya "NO MIND" (kutokuwa na fikra) unakuwa na utambuzi na ufahamu wa yote yanayoendelea lakini unakua haufikirii kitu chochote, na hicho ndio kiini cha Meditation.

Hali hiyo pia hutambulika kama "KUPITIA WAKATI WA SASA" (EXPERIENCING NOW) - Hapo unakua hauwazi yaliyopita wala yajayo, bali unakua katika wakati wa SASA (NOW).

"Experiencing NOW means: Being Alert and Aware but not Thinking"

Japokuwa mwanzoni utaweza kusimamisha mawazo(thoughts) kwa sekunde chache, kadri unavyofanya mazoezi ndivyo muda wa kupitia "hali ya sasa" uongezeka.

Unavyokuwa katika hali ya sasa, unakua umejiunganisha na utu wako wa ndani, ni sawa na kujiunganisha na mungu.
Hata Mtakatifu Pio wa Pietrelcina aliamini sana Tahajudi katika ukristo na alipata kusema:

"Kwa kusoma vitabu, mtu anamtafuta Mungu; kwa kutafakari(kufanya meditation) mtu anampata Mungu"

Na hiyo ndio ile hali ya juu ya meditation inavyokuwa, unakuwa huwazi past wala future, unakuwa katika hali ya sasa (Now).

Na baada ya kupitia hali ya sasa (NOW) utajikuta amani na furaha ya kweli inaongezeka, hiyo ni Amani na Furaha isiyotegemea vitu vya nje bali ni amani na furaha kutoka ndani na hiyo ndiyo nguvu ya sasa(POWER OF NOW) kama ilivyoelezewa na Eckhart Tolle katika kitabu chake cha "THE POWER OF NOW".

Kama umeelewa namna ya kujiunganisha na hali ya sasa, naamini utaenda kufanikiwa katika vitendo vyako vya meditation, kwasababu ile hali ya utambuzi (-wa utu wako wa ndani uliotofauti na utambuzi wa akili-) unayoipata unavyomtazama anayewaza/kusikiliza sauti yako/"WATCHING THE THINKER" ndio mwanzo wa hali utakayoipata katika Meditation, Na ndiyo maana wataalamu husema,

"Meditation is simple, but simple does not mean easy."

Karudie kusoma kanuni kuu za kuamka kiroho (BASIC PRINCIPLES OF AWAKENING) kama ulivyojifunza katika sehemu iliyopita. Maneno haya yakiwa ni mbegu iliyoangukia katika udongo mzuri wenye rutuba, Trust me, nawe utapata kumwona Mungu ndani mwako uso kwa uso. Lakini kama yameangukia kwenye miamba, njiani na kwenye miiba, keep waiting for a miracle [emoji23].

II: DIRECTING THE FOCUS OF YOUR ATTENTION INTO THE NOW. (weka focus ya umakini wako katika wakati wa sasa)

Copied Article: Olyme Songo III [emoji244]SERPENT BROTHERHOOD
JAMES LORDY KASHIRINA MINISTRY [emoji2398]All rights reserved.
 
Back
Top Bottom