Taasisi ya Haki za Binadamu, Tanzania Human Rights-Foundation (TAHURI) imetoa tamko la kuwataka Watanzania kuungana pamoja katika vita dhidi ya Shirika la Afya Duniani, WHO na Rais Magufuli huku likiwataka wananchi kumuunga mkono Rais wao.
Akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo Bollen Ngetti amesema;
"Tunaweza kutofautiana katika mambo mengi ya kiitikadi, kimtazamo na maono lakini katika mambo ya msingi kwa nchi kama hili la chanjo ni sharti tuungane kuwa kitu kimoja".
Aidha, Ngetti ambaye ni mwandishi wa habari nchini amesema Watanzania wasikimbilie tu athari za kiafya kwa chanjo hiyo na badala yake waangalie athari za kiuchumi.
"Tutambue kuwa dunia iko katika vitu kubwa ya kiuchumi. Kama Tahuri hatutajikita sana katika athari za kiafya za chanjo hiyo lakini tufikirie ni fedha kiasi gani chanjo hiyo itaswaga?"
"Ikumbukwe kwamba, kwa mujibu wa WHO ili nchi za ki-Afrika kupata chanjo kutoka makampuni yaliyojiorodhesha kwenye mkataba wa COVAX ambayo ni BioNTech na Moderna itazigharimu kiasi cha Dola za Marekani kati ya 7-11 kwa chanjo moja".
Ngetti ameendelea kusema, "kwa Tanzania pekee kama Rais Magufuli ataruhusu chanjo itatugharimu Tsh104Trilioni kwa idadi ya watu wetu nchi nzima. Hii ni fedha nyingi sana kwa nchi changa kama sisi".
Ngetti amefafanua kuwa fedha hizo zitatakiwa kukopwa kutoka Benki ya Dunia kwa udhamini wa ADB na itachukua miaka zaidi ya kumi kuzirejesha kwa riba ya asilimia 7.2.
Aidha, Ngetti amehoji, "kama nia njema kwa nini wazungu wamekimbilia kutafuta chanjo badala ya tiba kamili? Walijua kwa tiba utahitaji dozi chache sawa na idadi ya walioambukizwa ambao kwa sasa ni milioni 100 lakini kinga utacheza namba ya watu duniani".
"Jambo la pekee kama Taifa tunalotakiwa kufanya ni kufuata masharti ya kujikinga huku tulifanya kazi kwa bidii, huu ni upepo unaovuma na kupita, tusiondoshwe kwenye reli".
Ngetti amemaliza kwa kusema, "Magufuli si kichaa, wala hana historia ya ukichaa, anatutakia mema tusimvunje moyo. Lakini pia wataalamu wetu nao wakeshe maabara kukuna vichwa aidha kuchunguza chanjo hizo au kugundua za kwetu kama Waganda wanavyofanya"
My Take: Kwa vita hii tutashuhudia na kusikia mengi. Vita hii ya Magu na wanasayansi itaibua makubwa. Subiri tuone!