Yaani katika mambo yote ambayo wengine tunapigia kelele wao wanalilia hawapati nafasi ya kuzungumza Bungeni na kuwa Spika anawapendelea watu fulani fulani!?
Kwani walishawahi kuomba kuchangia hoja Bungeni wakanyimwa? Mbona siku ya Richmond Lowassa alikuwa wa kwanza kuchangia, alisema nini? Dr. Msabaha na Karamagi nao walipewa nafasi ya kuchangia.
Hoja ya kudai kwamba Spika huwa anapanga watu wake, sioni kama ina mantiki kwa kuwa hakuna Mbunge ambaye hunyimwa kuchangia hoja ama hotuba, na kwa bahati mbaya zaidi Spika huwa yuko very transparent kwamba Mbunge yeyote ambaye alishachangia hawezi kupewa nafasi ya kuchangia mara kwa mara, na hivyo top priority hupewa wale ambao huomba kuchangia huku akiwa hajawahi kuchangia. Nina hakika siku Rostam akiomba kuchangia ataitwa awe wa kwanza kwa kuwa hajawahi kuchangia.
Tatizo ni kwamba mafisadi wanaona aibu kusimama kuchangia hoja yoyote, watasema nini mbele ya runinga ambayo inatazamwa na Tanzania nzima mpaka na wapiga kura wao? Nani yuko tayari kujionyesha kwamba yeye ana-side na mafisadi. Hizo hoja za Hamis Mngeja type hakuna Mbunge hata mmoja anaweza kusimama kuongea pale Bungeni, maana nchi nzima inawaona.