Taifa au CCM- Kadi au Katiba?

Taifa au CCM- Kadi au Katiba?

Yaani katika mambo yote ambayo wengine tunapigia kelele wao wanalilia hawapati nafasi ya kuzungumza Bungeni na kuwa Spika anawapendelea watu fulani fulani!?

Kwani walishawahi kuomba kuchangia hoja Bungeni wakanyimwa? Mbona siku ya Richmond Lowassa alikuwa wa kwanza kuchangia, alisema nini? Dr. Msabaha na Karamagi nao walipewa nafasi ya kuchangia.

Hoja ya kudai kwamba Spika huwa anapanga watu wake, sioni kama ina mantiki kwa kuwa hakuna Mbunge ambaye hunyimwa kuchangia hoja ama hotuba, na kwa bahati mbaya zaidi Spika huwa yuko very transparent kwamba Mbunge yeyote ambaye alishachangia hawezi kupewa nafasi ya kuchangia mara kwa mara, na hivyo top priority hupewa wale ambao huomba kuchangia huku akiwa hajawahi kuchangia. Nina hakika siku Rostam akiomba kuchangia ataitwa awe wa kwanza kwa kuwa hajawahi kuchangia.

Tatizo ni kwamba mafisadi wanaona aibu kusimama kuchangia hoja yoyote, watasema nini mbele ya runinga ambayo inatazamwa na Tanzania nzima mpaka na wapiga kura wao? Nani yuko tayari kujionyesha kwamba yeye ana-side na mafisadi. Hizo hoja za Hamis Mngeja type hakuna Mbunge hata mmoja anaweza kusimama kuongea pale Bungeni, maana nchi nzima inawaona.
 
hili li chama la hovyo kweli wao ccm wanachoelewa ni kuvaa manguo yao ya kijani tu na sio utaifa wetu na zaidi ya yote nachukizwa sana na hawa vibaraka wa akina EL, RA na chenge yani ccm inaendeshwa na remote ya rostam na lowassa ni upumbavu sana kuwaona wazee kama kingunge wakimpigia magoti lowasa na rostam huuu ni wehu na sasa wanaingilia bunge huu ni ubakaji wa demokrasia.
 
Yaani kwenye chama kuna watu wana Elimu zao lakini wanashindwa kuitumia na wanajikuta wananyamazishwa na vijitu visivyo kuwa na elimu na kujikuta wanafuata mkumbo na kubaki midomo yao mabubu hawa nao ni wajinga.
 
Sasa najiuliza kwanini Sitta hakukataa kuomba msamaha? kwanini Sitta hakukubali kunyang'anywa kadi ya CCM na awe amestaafu siasa kwa heshima? lol! nafasi moja ya ukombozi imepotea hapa.

Jibu la swali lako lipo hapa

Na. M. M. Mwanakijiji
Alichofanya Spika Sitta ni kile vitani kinaitwa "strategic retreat" yaani kurudi nyuma kimkakati ili kujipanga upya. Kama nilivyoandika wiki iliyopita hii ni vita na siyo mapambano. Unaweza ukapoteza pambano moja au mawili lakini mwisho wa siku utashinda vita.

MM.
Kama kawaida I salute you. Mimi umenigusa sana kwenye hii decision aliyoifanya SItta. Ndugu wengi wanamawazo kuwa Sitta alitakiwa kuachia kadi, mimi naungana na wewe moja kwa moja kwamba kwa jinsi mambo yalivyo na yanavyo kwenda that was not the best option. Nataka kuamini kama ulivyosema alipoomba msamaha ni "strategic retreat" .

Otherwis makala yako ni nzuri sana kwa kuwa at times ninakuwa down thinking mapambano ni magumu mafisadi wanaelekea kutushinda lakini when we read this kind of staff unapata moyo tena then tunasonga mbele.
 
Napata uchungu sana ,kwa mtindo huu Demokrasia imeshindwa Tanzania na sasa ili kuwe na uwiano sawa na mgawanyo sawa wa raslimali ni bora kurejea katika mbinu kongwe ya uanamapindui ili sasa tuanzie hapo.Ndiyo maana naendelea kuwaheshimu akina Fidel Castro,Che Guevara,Col.Muamar Gaddaffi,Evo Morales wa Bolivia,Hugo Chavez wa Carcas Venezuela na hata Yoweri Museven.....hawa ni ma-role model wangu kwa kusema kweli. Si mapinduzi yote ni haramu,hwa jamaa wote walifanya mapinduzi ambayo ukifutilia kwa makini uchumi katika nchi zao ulianza kuwa stable,sasa naona CCM watanifanya nibadili muelekeo wangu wa kisiasa.

Siwezi kuvumilia kuona watanzania wakiendelea kuwa maskini huku CCM wakiendelea ku-play Delay tactics zao ili wabakie madarakani huku majirani zetu wakiendelea kutukejeli kila siku,Ni Lazima Heshima ya Mtanzania irudi! Roho inaniuma sana,yaani hata fikra mbadala CCM wanazikemea,hwa ndiyo wanotulazimisha wengine kutumia njia haramu,potelea mbali.Taifa gani ambalo wananchi wake ni maskini,wanakufa kwa maradhi,huku tunakosa mbinu mbadala za kukuza uchumi kwa sababu ya wapuuzi wachache? Hili silo taifa walilopigania babu zetu kama akina Mkwawa,Mirambo,Mangi sina,kimweri au akina Jk Nyerere,Bibi Titi,mzee kizota na wengineo,Mungu awalaze Pema Peponi.Leo hii viongozi wetu wmegeuka kuwa mawakala wa unyonyaji,wanatumiwa na wahindi,wachina na wazungu mliowakataa kututawala.

CCM ILAANIWE! MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Mr Zkuimi,

Katiba wanatunga wenyewe afu wanashindwa kuifuata.

Hayo ni maneno ya kweli wanatakiwa kujirudi na kjitama upya kama kweli ndicho wanachokifanya na kina lingana na katiba walio itunga??

Hata Irani yao ya CCM inapaswa kuandikwa upya haiwezekani hata kidogo ati yenyewe hutekeleza yote wayasemayo kwenye kampeni zao, Irani gani hufanya kila kitu?? Utasikia ati haya yote yalikuwa kwenye Irani ya CCM! "useless" kila kipindi cha miaka 5 yalikuwa kwenye Irani ya CCM jamani we're not fulls by the way, Nakama ni kweli basi takribani ni miaka zaidi ya miaka 15 basi CCM ingekuwa ishatuletea maendeleo ila mpaka sasa ni siasa zao ndio zatawala na unafki, kwanini wasikubali kuwa kipindi hiki twafanya hili kwa kiwango hiki na twahamia kwingine nasio kurudia kila siku pale pale, CCM wanaogopa kuwepo kwa maendeleo wata kosa sera za kuweka kwenye iyo wanayoita Irani yao
 
Sasa inajipambanua CCM ni nini, Maaskofu hamasisheni sasa kuipinga CCM kwani ndiye Mama wa Mafisadi. Hauwezi kumdhibiti mtoto bila kwanza kumwangamiza mama, atazaa wengine.
 
CCM should be told, NEVER AGAIN! what they are doing now is to defend their evil regime, but freedom is coming tommorow! people are now eyes and their ears open, because they know much/and are still knowing about EPA, RICHMOND, SONGAS, MEREMETA, BoT scams just to name a few, you cant fool people all the time, this is a solid truth that stands.

Our president administration is a comedy like! he is not really doing what should be done but he is just trying to show Tanzanians that he is there to combat corruption which is not true. He is leading a regime that is filled with evil men. JK ascended from CCM his cleanlines is questionable, how he managed to get at the state house is also on blackets that is why if he condems his fellow on the same boat defenetely when the boat breaks he is the one to be drowned because he shares the same interest.

But the message is, our poverty striken population is now looking at CCM and they are not differentiating CCM and MAFISADI, they define all the two synonymously, WARAKA WA KATOLIKI, WALAKA WA WA-LUTHERI, ISLAM, WALAKA wa KILA MTU BINAFSI (Because everyone is now preparing his/her own 'walaka' shows the loss of confidence with those on power. Tanzanians are now snached their land on the umbrella of investors, their anger one day will break out! what a disaster, we can not wait until the valuable peace of our our nation is lost, rather CCM should be disciplined by Tanzanians!

We cant allow them to continue fooling millions, we are now awake!

Freedom is coming tommorow.
 
Thanks kaka lakini tunapotoka pale tunapojifisadi na kuacha kualign every issue with presidential affairs. Mule ndani ya ccm kuna mihimili yote yaani serikali, bunge na mahakama kwani wajumbe wa kamati kuu wanatoka katika mihimili hiyo na ndo maana sitta anaingia kamati kuu kwa nafasi yake ya spika na si vinginevyo.
Kama unadhani sitta ndo mzalendo saaaana basi awe wa kwanza kufungua kesi ya rushwa dhidi ya matokeo ya uchaguzi wa rais w mwaka 2005.
For your good information miongoni mwa wenye uozo mkubwa wa ufisadi, sitta ni kinara na ingekuwa afya kwake na kwa nyie supporters wake kuangalia ways to settle issues siyo kukilaumu chama cha mapinduzi.
Tell him to declare interest on kagoda and richmond saga then let's talk of ccm card. Msitufanye hatuoni tunajua yanayoendelea ila tu tumekaa kimya.
Mbona unajichanganya, sema kikwete (rais anahusikaje) halafu mtenganishe na sitta (spika), kisha ichambue richmond, kagoda, buzwagi na mengine then kamuulize zitto kilichomnyamazisha ni nini na ni ipi kauli ya kamati ya madini
 
Kwanza tuombe wabunge wetu kama ubavu huo wanao wazuie mtu aliyechaguliwa nao kuwa SPIKA kuwa mjumbe wa vikao vya juu vya CHAMA kilichomteua kugombea nafasi hiyo. Spika wetu wa sasa kwa wadhifa huo ni mjumbe wa CC ya CCM. Ataachaje kujadiliwa huko?
Nafasi ya SPIKA kama ilivyo ya JAJI MKUU inapaswa kuwa above party politics vinginevyo tunachokijadili hapa ni ndoto tu.
 
Kaazi kwelikweli. Nini msingi wa mamlaka yetu ya nchi. Hakika tumelewa madaraka mpaka tunalifananisha bunge na kikundi cha uchekeshaji Komedy!!!! Inamana kuwasemea wananchi bunge limegeuka kichekesho kwa serikali. Tuwaambie wananchi tuliowapa madaraka wamelewa, wanawacheka kwa kuwa wananunulika kwa wali, kanga, na masahani ya pilau.
 
hvi jamani Sitta huwa anapita humu.. naomba Mungu akipita asome hii article ya Mwkjj itampa nguvu sana.. Sitta tuko nyuma yako usikate tamaa, kwangu mimi naona hicho kikao ni gas imewekwa kwenye tank sasa washa gari tuanze safari kwa speed na standard ya kuogopewa na ao wapuuzi na wize wa mchana kweupe
 
Kuna watu huwa mnamwaga sifa hapa kwamba Kikwete ni mwana mapinduzi ana heshimu na kusikiliza maoni ya watu na ndiyo maana uhuru wa watu kujieleza umejaa ? Mimi nasema uhuru huu umejaa kwa kuwa ni muda wake they can no longer silence the mass .Lakino JK si mkweli na hapendi kuambiwa ukweli na kwa JK CCM kwanza Tanzania na haki za Nchi baadaye .Majuzi ameshutumiwa kwa kutoa go ahead Mbunge ambaye ni Mganda kule Bigaramulo na yeye ana injinia muda Tume kutangaza CCM wameshinda ni Tarime pekee alishdwa mara zote pamoja na majeshi yake kutumika .
Duh wewe una hasira!Unaweza kumeza moto kwa hilo donge lililopo mdomoni!Punguza kidogo najua wewe ni wale mnaopigana kule unyanchorini jamani polepole!
 
Nafikiri nakubaliana nawe WildCard. Inabidi mbadilishe Katiba yenu (Ya Jamhuri ya Muungano wa Tz.) na kuwe na utaratibu mwengine wa kupatikana Spika. Kwa sasa Bw. Sitta aliomba pale akiwa ni Mteule wa CCM aliyetakiwa kugombea nafasi hiyo. Kwa maana nyengine Uspika wake ana ubia na CCM. sasa kwa nini CCM isimuweke kiti moto?
 
Chama kina encourage usanii iwe kigezo cha kuongoza nchi.kazi kwelikweli
 
Nafikiri nakubaliana nawe WildCard. Inabidi mbadilishe Katiba yenu (Ya Jamhuri ya Muungano wa Tz.) na kuwe na utaratibu mwengine wa kupatikana Spika. Kwa sasa Bw. Sitta aliomba pale akiwa ni Mteule wa CCM aliyetakiwa kugombea nafasi hiyo. Kwa maana nyengine Uspika wake ana ubia na CCM. sasa kwa nini CCM isimuweke kiti moto?
Mkuu,
Mbona unasema Katiba yenu badala ya yetu?
 
Kwa maoni yangu naona kama CCM haikumpongeza Spika kwa kuwa mstari wa mbele kupiga vita rushwa basi inadhihirisha kuwa kama chama hakiungi mkono vita dhidi ya rushwa. Yaani hapa ni pande mbili tu ama unapiga vita ama unatetea na kukumbatia rushwa. Na ushahidi wa vigogo kuongoza kwenye rushwa uko wazi mno. Inatia uchungu mno kufahamu sasa Chama chetu kilivyo. Hapana, tunahitaji kuamka sasa na kusema sasa basi. Tuwapuuze wapuuzi na kuwaunga mkono wazalendo.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Bunge lina watu wenu wengi, na Rais anatoka chama chenu; vunjeni Bunge mrudi kwa wananchi sasa! Kama Bunge halichezi ngoma mnayoipiga au kuitikia mlio wa sauti zetu, rudini kwa wananchi mtafute madaraka upya.

Makala hii inaweza kutumika na gazeti lolote lile bila ya kubadilisha mtunzi.

Kama mnafikiri mambo hayaendi vizuri, na mnafikiri mna hoja, Bunge lina watu wenu wengi, na Rais anatoka chama chenu; vunjeni Bunge mrudi kwa wananchi sasa! Kama Bunge halichezi ngoma mnayoipiga au kuitikia mlio wa sauti zetu, rudini kwa wananchi mtafute madaraka upya.

THUBUTU, KWANI UBAVU WANAO HIVI SASA????

MBELE UFISADI, NYUMA ZOMBE, KULIA EU NA WENGINEO KUHUSU DAFTARI LA WAPIGA KURA, KUSHOTO MAWAZIRI KUZOMEWA BINGENI, JUU RICHMOND, CHINI BUZWAGI, LOLIONDO ETC ,KATIKATI WALIMU NA WAZEE WA JUMUIYA ILIYOVUNJIKA.SUPPLIMENTARY: KUNYIMA WANAFUNZI MIKOPO YA VYUO, WANANCHI WA KAWAIDA MAISHA AFADHALI YA JANA, MADERVA WA MABASI. HAMNA MTAJI KABISA KAMA NI KUCHEZA BAO WAMETAKATA.

TUACHE KUJADILI UDHAIFU WAO, BADALA TUTUMIE UDHAIFU HUO KUJENGA NA KUIMARISHA LENGO LA UHURU
 
Jana nimezungumza na baadhi ya wahariri na nimewaambia wazi kuwa wao ndio wanawapa nguvu hawa mafisadi!

Kama CCM walimjadili Sitta na wakajadili mambo hayo sirini na kuwa ilikuwa ni moto moto kwanini katika tamko lao hawakusema hasa nini kilichosemwa kwa nani na kwa nini? Katiba ya CCM inatoa maelekezo kabisa ya nini cha kufanya kuhusu mwanachama yeyote yule na adhabu gani zinaweza kutolewa, ni nani aliyekuja na wazo la kumvua tu uanachama?

Sasa waandishi wanapoandika in detail kitu ambacho CCM haisemi hadharani wanawapa nguvu. Hata bila kwenda in detail Chiligati angeweza kusema "CCM imekaa chini na kuangalia mmoja wa wanachama wake na kumuonya; baadhi ya wajumbe walitaka mwanachama huyo avuliwe uanachama lakini mwanachama huyo aliomba radhi na hivyo Kamati imeundwa kufuatilia x,y". Lakini hili hawakulifanya!

Sasa waandishi wanapoandika vitu in detail ambavyo CCM yenyewe hata kuviacknowledge haijafanya hivyo ina maana CCM inatumia vyombo vya habari kupitisha habari rasmi ambayo yenyewe haina ujasiri wa kuziweka hadharani.
 
Back
Top Bottom