Nafahamu na kila mmoja wetu humu anafahamu namna ulivyo na chuki binafsi kwa mh Rais wetu mama Samia suluhu Hassani,kwa bahati mbaya kwako ni kuwa unapuuzwa na wengi kwa kuwa watu wanafahamu kuwa huwa unaandika kwa chuki na hasira tu kwa mh Rais.
Watanzania wanatambua juhudi kubwa zinazofanywa na mh Rais wetu katika kuboresha maisha ya watanzania,amefanya haya kwa wakulima kwa kutoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini katika mbolea na hivyo kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni, mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu, Rais samia amewafuta machozi wakulima baada ya kufanya juhudi kubwa katika kuhakikisha kuwa wanapata soko la uhakika kwa mazao yao ,tofauti na ilivyokuwa awali walipo kuwa wanapangiwa Bei na mahali pa kuiza,.
Rais Samia na serikali yake ameboresha huduma za kijamii na kusogeza karibu kabisa ya watanzania, Amejenga zahanati, vituo vya Afya kila Kona ya nchi, Amejenga vyumba vya madarasa zaidi ya elfu 20 na hivyo kupelekea wanafunzi wote wanaofaulu kuanza masomo kwa pamoja,ameongeza mapato mpaka kufikia Trioni mbili kwa Mwezi pasipo kukimbizana Wala kufungiana biashara mitaani. Elimu bure Hadi kidato Cha sita
Ametoa maelfu ya ajira kwa vijana Mitaani, uwekezaji uneongezeka Sana kutokana na Imani kubwa Waliyonayo wawekezaji kwa Taifa letu kunakotokana na juhudi kubwa za mh Rais kuimarisha mahusiano yetu na mataifa mbalimbali tofauti na ilivyokuwa awali, jiulize kwanini Rais wa marekani aliamua kuitembelea Tanzania Kati ya makumi ya nchi Barani Afrika?
Demokrasia na utawala Bora ni imara Sana kwa Sasa na ndio maana unaona hata ripoti ya CAG ikiwa huru,Rais Samia ameendelea kuchukua hatua za kinidhamu kwa wezi na wabadhirifu wa Mali za umma,lakini pia uchunguzi unaendelea kwa wengine wote na hatua za kisheria zitaendelea kuchukuliwa.
Rais wetu Ni imara,Jasiri , shupavu na madhubuti Sana kiuongozi na ndio maana tumefika hapa tulipo na tunaendelea kusonga mbele kwa Kasi ya upepo na kupata mafanikio katika kila secta na kila eneo, ndio sababu ya Kuendelea kuaminika na kuungwa mkono na mamillion ya watanzania