Taifa la ISRAEL halitambui Ukristo; na hata Yesu wanamuona ni "MHAINI".

The Dictator

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
4,475
Reaction score
12,281
images (15).jpeg

Ninapoelezea jambo hili linalohusu 'nchi hii', sio 'taifa lile la Mungu wa Biblia'; nitagusia katika vipengele mbalimbali ili kuona haswa huu mzizi ulianzia wapi

KIHISTORIA:

Wayahudi wengi (ikiwa ni pamoja na viongozi wa dini ya Kiyahudi) hawakumkubali Yesu kama Masihi (Masiha) kwa sababu:

Yesu hakutimiza matarajio yao ya kisiasa ya Masihi waliokuwa nayo wakati huo. Walimtarajia Masihi wa kijeshi au mfalme ambaye angewaokoa kutoka kwa utawala wa Kirumi katika enzi zile za kaisari. Badala yake masihi huyu alipokuja;
Mafundisho ya Yesu yalikuwa tofauti na ya viongozi wa Kiyahudi (kama Mafarisayo na Masadukayo), akiwakemea kuwa ni wanafki.

Mpaka leo hii Wayahudi (Jews) wanaendelea kusubiri ujio wa Masihi waliyeahidiwa kuwa angukuja. Masihi atakayefanya mabadiliko ya wazi duniani (kama amani ya kimataifa, hekalu kujengwa tena, nk).

••••> Hivyo, Wayahudi wengi wa sasa bado hawamtambui Yesu kama Masihi au Mwana wa Mungu—wanamchukulia kama mwalimu wa Kiyahudi au nabii aliyetofautiana na imani ya Kiyahudi.

UKRISTO: MGOGORO WA KIHISTORIA

Katika historia ya Ulaya na dunia kwa ujumla; Wakristo (hasa wakati wa Dola ya Kirumi hadi karne ya kati) waliwalaumu Wayahudi kwa “kumuua Yesu” (kulingana na mafundisho fulani ya Kikristo).

Hii ilisababisha karne nyingi za chuki dhidi ya Wayahudi (antisemitism)—ikiwemo mateso, mauaji, na kuwindwa kwao.

Kwa hiyo, baadhi ya Wayahudi walikuza hofu au hata msimamo mkali dhidi ya Ukristo kama mfumo uliowatesa.

Kwa hiyo, si kwamba Israeli ya sasa "inachukia Wakristo" kwa sababu ya Yesu pekee, bali kuna historia ndefu ya migogoro ya kidini.

KISHERIA NA KIJAMII KATIKA ISRAEL YA LEO

Israel hii ya leo iliyoundwa kisiasa; 14 Mei 1948, ni taifa la Kiyahudi, lakini pia lina wakristo (karibu 2%)—hasa Waarabu Wakristo.

Ukristo huruhusiwa kisheria nchini Israel, na makanisa yapo.

Ingawa, kuna mashinikizo makubwa ya kijamii kutoka kwa jamii za Kiyahudi ya madhehebu ya Orthodox dhidi ya watu wanaookoka kuwa Wakristo (wanaoitwa Messianic Jews).

•••> Katika baadhi ya maeneo, vikundi vya Kiyahudi wenye msimamo mkali huona Ukristo kama "uhaini wa kidini au WAHAINI" kwa kuwa inaamini Yesu ni Masihi.
 
Dume la mbegu apo Mashariki ya katii ni moja tuu,wengine wachumba tu.. Makobaz yanapelekwaa motoo hataree
1000041077.jpg
 
Mpaka leo hii Wayahudi (Jews) wanaendelea kusubiri ujio wa Masihi waliyeahidiwa kuwa angukuja. Masihi atakayefanya mabadiliko ya wazi duniani (kama amani ya kimataifa, hekalu kujengwa tena, nk).

••••> Hivyo, Wayahudi wengi wa sasa bado hawamtambui Yesu kama Masihi au Mwana wa Mungu—wanamchukulia kama mwalimu wa Kiyahudi au nabii aliyetofautiana na imani ya Kiyahudi.
Wakawachochea Waroma kumuua Masihi, na Mungu akawakataa na wakapata kipondo cha uhakika kutoka kwa Waroma mwaka wa 70AD na hekalu lao kuvunjwavunjwa na kuchomwa moto bila kusalia jiwe juu ya jiwe. Na hadi leo hawana amani kama taifa. Wakome!

Kinachofanya Wayahudi wasiondolewe kama taifa ni duniani ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu, kwamba japo walimkataa Yesu bado ahadi ya Mungu kwa Abrahamu ya kuwafanya taifa iko palepale. La sivyo wangekuwa hawapo tena duniani kama taifa. Ndio maana Hitler alishindwa, na waarabu wanashindwa, na hakuna mtu atakaefanikiwa kuwamaliza Israel duniani, kwa nuclear au bunduki. Si kwa sababu wao ni taifa teule Mungu anawapendelea,la hasha. Ni kwa sababu ya ahadi ya Mungu kwa babu yao Ibrahimu
 
Chanzo chako ni kipi mkuu, kwa haraka haraka Israel kuna madhehrbu ya kawaida kama ilivyo nchi nyengine mfano Tanzania, marekani n.k wao wana uhuru wa kuabudu pia ukristo ni imani isiyo ya kulazimisha mtu kila mtu ana chaguo lake, lakini pia kizazi hiki so kile cha musa, kuna mabadiliko makubwa hivyo tuache kuongea vitu visivyo na msingi vya vijiweni au tusivyo vielewa kwa kina.

Kwa haraka haraka hujui unaongea nini ?
 
View attachment 3375940

Ninapoelezea jambo hili linalohusu 'nchi hii', sio 'taifa lile la Mungu wa Biblia'; nitagusia katika vipengele mbalimbali ili kuona haswa huu mzizi ulianzia wapi

KIHISTORIA:

Wayahudi wengi (ikiwa ni pamoja na viongozi wa dini ya Kiyahudi) hawakumkubali Yesu kama Masihi (Masiha) kwa sababu:

Yesu hakutimiza matarajio yao ya kisiasa ya Masihi waliokuwa nayo wakati huo. Walimtarajia Masihi wa kijeshi au mfalme ambaye angewaokoa kutoka kwa utawala wa Kirumi katika enzi zile za kaisari. Badala yake masihi huyu alipokuja;
Mafundisho ya Yesu yalikuwa tofauti na ya viongozi wa Kiyahudi (kama Mafarisayo na Masadukayo), akiwakemea kuwa ni wanafki.

Mpaka leo hii Wayahudi (Jews) wanaendelea kusubiri ujio wa Masihi waliyeahidiwa kuwa angukuja. Masihi atakayefanya mabadiliko ya wazi duniani (kama amani ya kimataifa, hekalu kujengwa tena, nk).

••••> Hivyo, Wayahudi wengi wa sasa bado hawamtambui Yesu kama Masihi au Mwana wa Mungu—wanamchukulia kama mwalimu wa Kiyahudi au nabii aliyetofautiana na imani ya Kiyahudi.

UKRISTO: MGOGORO WA KIHISTORIA

Katika historia ya Ulaya na dunia kwa ujumla; Wakristo (hasa wakati wa Dola ya Kirumi hadi karne ya kati) waliwalaumu Wayahudi kwa “kumuua Yesu” (kulingana na mafundisho fulani ya Kikristo).

Hii ilisababisha karne nyingi za chuki dhidi ya Wayahudi (antisemitism)—ikiwemo mateso, mauaji, na kuwindwa kwao.

Kwa hiyo, baadhi ya Wayahudi walikuza hofu au hata msimamo mkali dhidi ya Ukristo kama mfumo uliowatesa.

Kwa hiyo, si kwamba Israeli ya sasa "inachukia Wakristo" kwa sababu ya Yesu pekee, bali kuna historia ndefu ya migogoro ya kidini.

KISHERIA NA KIJAMII KATIKA ISRAEL YA LEO

Israel hii ya leo iliyoundwa kisiasa; 14 Mei 1948, ni taifa la Kiyahudi, lakini pia lina wakristo (karibu 2%)—hasa Waarabu Wakristo.

Ukristo huruhusiwa kisheria nchini Israel, na makanisa yapo.

Ingawa, kuna mashinikizo makubwa ya kijamii kutoka kwa jamii za Kiyahudi ya madhehebu ya Orthodox dhidi ya watu wanaookoka kuwa Wakristo (wanaoitwa Messianic Jews).

•••> Katika baadhi ya maeneo, vikundi vya Kiyahudi wenye msimamo mkali huona Ukristo kama "uhaini wa kidini au WAHAINI" kwa kuwa inaamini Yesu ni Masihi.
View attachment 3375940

Ninapoelezea jambo hili linalohusu 'nchi hii', sio 'taifa lile la Mungu wa Biblia'; nitagusia katika vipengele mbalimbali ili kuona haswa huu mzizi ulianzia wapi

KIHISTORIA:

Wayahudi wengi (ikiwa ni pamoja na viongozi wa dini ya Kiyahudi) hawakumkubali Yesu kama Masihi (Masiha) kwa sababu:

Yesu hakutimiza matarajio yao ya kisiasa ya Masihi waliokuwa nayo wakati huo. Walimtarajia Masihi wa kijeshi au mfalme ambaye angewaokoa kutoka kwa utawala wa Kirumi katika enzi zile za kaisari. Badala yake masihi huyu alipokuja;
Mafundisho ya Yesu yalikuwa tofauti na ya viongozi wa Kiyahudi (kama Mafarisayo na Masadukayo), akiwakemea kuwa ni wanafki.

Mpaka leo hii Wayahudi (Jews) wanaendelea kusubiri ujio wa Masihi waliyeahidiwa kuwa angukuja. Masihi atakayefanya mabadiliko ya wazi duniani (kama amani ya kimataifa, hekalu kujengwa tena, nk).

••••> Hivyo, Wayahudi wengi wa sasa bado hawamtambui Yesu kama Masihi au Mwana wa Mungu—wanamchukulia kama mwalimu wa Kiyahudi au nabii aliyetofautiana na imani ya Kiyahudi.

UKRISTO: MGOGORO WA KIHISTORIA

Katika historia ya Ulaya na dunia kwa ujumla; Wakristo (hasa wakati wa Dola ya Kirumi hadi karne ya kati) waliwalaumu Wayahudi kwa “kumuua Yesu” (kulingana na mafundisho fulani ya Kikristo).

Hii ilisababisha karne nyingi za chuki dhidi ya Wayahudi (antisemitism)—ikiwemo mateso, mauaji, na kuwindwa kwao.

Kwa hiyo, baadhi ya Wayahudi walikuza hofu au hata msimamo mkali dhidi ya Ukristo kama mfumo uliowatesa.

Kwa hiyo, si kwamba Israeli ya sasa "inachukia Wakristo" kwa sababu ya Yesu pekee, bali kuna historia ndefu ya migogoro ya kidini.

KISHERIA NA KIJAMII KATIKA ISRAEL YA LEO

Israel hii ya leo iliyoundwa kisiasa; 14 Mei 1948, ni taifa la Kiyahudi, lakini pia lina wakristo (karibu 2%)—hasa Waarabu Wakristo.

Ukristo huruhusiwa kisheria nchini Israel, na makanisa yapo.

Ingawa, kuna mashinikizo makubwa ya kijamii kutoka kwa jamii za Kiyahudi ya madhehebu ya Orthodox dhidi ya watu wanaookoka kuwa Wakristo (wanaoitwa Messianic Jews).

•••> Katika baadhi ya maeneo, vikundi vya Kiyahudi wenye msimamo mkali huona Ukristo kama "uhaini wa kidini au WAHAINI" kwa kuwa inaamini Yesu ni Masihi.
Yesu amezaliwa bila baba.

Mungu akampa miujiza ili kuthibitisha kwa Wayahudi kuwa yeye ni Mtume.

Wayahudi juu ya huu miujiza mkubwa kabisa wa kuzaliwa bila baba wakamkana.

Hawakuishia hapo bali walisema maneno kuhusu mama yake mimi sina ujasiri wa kuyaandika.

Siwezi kurejea matusi sembuse matusi aliyotukanwa Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Wayahudi wanaamini kuwa walimuua Yesu na Wakristo wanaamini hivyo.

Allah kwenye Qur'an anasema kuwa hawakumuua wala hawakumsulubu.

Allah alimnyanyua mbinguni Mtume wake.
Mwenyezi Mungu akawalani Wayahudi.
 
daaaah, watu wangu wana angamia kwa kukosa maarifa kama uliweza kumuamini mtu aliyekuja na kitabu na story za kiyahudi zilizo kuwepo katne kibao eti kimetoka mbinguni sina cha kukudai kwa uwezo wako wa akili.

Hebu tuache kumuhusisha na kulitaja jina lake hovyo pia.

Uhalali wa watumishi wa mungu sio wa kulazimisha au wakijizima data na kujifanya huoni kwamba huwenda fikra zako zikatokea kweli au flani akawa mungu wa kweli mambo hayako hivyo.

Ni kweli yesu alitukanwa na hakuwa muslam, kama unavyo sema na walimkataa baadhi na baadhi walimkubali pia lakini habari za yesu za kweli zinapatikana kwenye kitabu cha zamani pekee cha kiyahudi na sio kitabu kingine baada yake ambacho kiasili hakitoki kwenye eneo yesu alilo liishi.

Niseme tu ukweli hakuna mungu anayeitwa allah na kitabu cha Quran ni copy ya biblia ninaweza kuthibitisha hilo lakini kama umejizima data na kulazimisha kuwa Allah yupo na Quran ndio katabu cha kweli sina cha kukudai pole sana
 
Sisi walokokole na wakatoliki wa kimara king'ong'o hatuwezi kukubali
 
Wayahudi ndio Wakristo. Wakristo wametoka ndani ya Uyahudi. Na Yesu alikuja kwasababu hiyo yaani kuwabadilisha Wayahudi pamoja nawewe kuwa wakristo. Ila kwasababu ya ugumu wa mioyo yenu mlimkataa nayeye akaamua kugeukia watu wa mataifa mengine.
 
Chanzo chako ni kipi mkuu, kwa haraka haraka Israel kuna madhehrbu ya kawaida kama ilivyo nchi nyengine mfano Tanzania, marekani n.k wao wana uhuru wa kuabudu pia ukristo ni imani isiyo ya kulazimisha mtu kila mtu ana chaguo lake, lakini pia kizazi hiki so kile cha musa, kuna mabadiliko makubwa hivyo tuache kuongea vitu visivyo na msingi vya vijiweni au tusivyo vielewa kwa kina.

Kwa haraka haraka hujui unaongea nini ?
Sasa wewe ndio hujui unaongelea nini, japo unamsema mwezio. Mgawanyo wa dini nchini Israel uko hivi;
  • Total population of Israel: ~9.8 million
  • Jewish population: ~7.2 million
  • Percentage Jewish: ~73–74%
  • Muslims: ~18% of the population
  • Christians: ~2%
  • Druze: ~1.6%
  • Others/Unclassified (including non-religious): ~4–5%
Hivyo basi, ni sawa kusema karibu taifa lote la Israel hawamtambui Yesu, ukifikiria asilimia 2% tu ya watu wa Israel ndio Wakristo. Jews hawamtabui Yesu kuwa ndie alikuwa Masihi, ni kweli alivyosema
 
Sawa sawa mkuu sikulifuatilia hilo kwasababu nazani halina msingi wowote ndio maana sikulipa kupaumbele kwa sasa asante kwa data.
 
Sasa wewe ndio hujui unaongelea nini, japo unamsema mwezio. Mgawanyo wa dini nchini Israel uko hivi;
  • Total population of Israel: ~9.8 million
  • Jewish population: ~7.2 million
  • Percentage Jewish: ~73–74%
  • Muslims: ~18% of the population
  • Christians: ~2%
  • Druze: ~1.6%
  • Others/Unclassified (including non-religious): ~4–5%
Hivyo basi, ni sawa kusema karibu taifa lote la Israel hawamtambui Yesu, ukifikiria asilimia 2% tu ya watu wa Israel ndio Wakristo. Jews hawamtabui Yesu kuwa ndie alikuwa Masihi, ni kweli alivyosema
Wengine wapo-kupinga tu. Tumewazoea hata hivyo
 
daaaah, watu wangu wana angamia kwa kukosa maarifa kama uliweza kumuamini mtu aliyekuja na kitabu na story za kiyahudi zilizo kuwepo katne kibao eti kimetoka mbinguni sina cha kukudai kwa uwezo wako wa akili.

Hebu tuache kumuhusisha na kulitaja jina lake hovyo pia.

Uhalali wa watumishi wa mungu sio wa kulazimisha au wakijizima data na kujifanya huoni kwamba huwenda fikra zako zikatokea kweli au flani akawa mungu wa kweli mambo hayako hivyo.

Ni kweli yesu alitukanwa na hakuwa muslam, kama unavyo sema na walimkataa baadhi na baadhi walimkubali pia lakini habari za yesu za kweli zinapatikana kwenye kitabu cha zamani pekee cha kiyahudi na sio kitabu kingine baada yake ambacho kiasili hakitoki kwenye eneo yesu alilo liishi.

Niseme tu ukweli hakuna mungu anayeitwa allah na kitabu cha Quran ni copy ya biblia ninaweza kuthibitisha hilo lakini kama umejizima data na kulazimisha kuwa Allah yupo na Quran ndio katabu cha kweli sina cha kukudai pole sana
Genius...
Ninachoweza kusema ni kuwa unazungumza vitu ambavyo huvijui.
 
Back
Top Bottom