Taifa la waliokata tamaa, Dawa yake ni nini?

Taifa la waliokata tamaa, Dawa yake ni nini?

Kosa ambalo tunafanya kama raia ni kuamini tunahitaji watu au kikundincha watu kuja kututuoa hapa tulipo bila kujua hiyo mentality ndio the very cause of our demise as a Nation and as THE PEOPLE.

Cha msingi turejee misingi. Tuanze na ujenzi wa familia imara yaani baba mama na watoto, huku ndipo tutaweza toa viongozi siku za baadae wataoweza kurithi na kuiendesha mifumo bora na sheria na miiko mizuri ya uongozi.

Tuachane na hizi mbaga za kutafuta mkombozi, sisi ndio wakombozi wa taifa letu hakuna mtu ataweza hiyo kazi pekee yake. Magufuri amekuja kutupaambania mnaona jinsi alivyoshambuliwa kila kona hadi leo hatuelewi nini kilitokea but tutajua nyuma yake watu wabaya na waovu walishirikiana kufanya madhara.

Ifike wakati tujitathimini sisi kwanza binafsi haya matatizo kuanzia gazi ya vitongoji, kata, wilaya hadi mkoa tunadeal nayo vipi kama jamii.

Sio barabara inaharibika tunasema "tunaomba serikali ije kutujengea barabara" Hapana, hii si sawa. Tunachotakiwa ni kumtuma muwakilishi akatusemee bungeni kuwa tunahitaji barabara, kama inawezekana kujengewa tuambiwe lini tutaipata kama haiwezekani atuletee majibu ili wanaichi tuweze kwanza kuhoji matumizi ya mapato ya halmashauri zetu na kama mapato ni kidogo then tuanze kuja na mikakati ya kukuza mapato kupitia shughuli za uchumi na kuhamasishana kuwa na vikao vya kujadili namna ya kupata mapato ya kulipia gharama za ujenzi wa barabara.

Tukifanya hivi ndani ya miaka 5 barabara zitajengwa nyingi sana. Na tutapunguza gharama za ukali wa maisha.
 
Dawa ni kuchukua fursa tu. Rahisi kupata cheap labour, tumia dini utawaokota kirahisi sana, ongea na mchina muungane kwenye betting utazikusanya sana. Fursa Huwa n nyingi sana
 
Ukitaka kujua viongozi weusi hawana akili panda ndege kwenda ulaya basi ukiwa kwenye Mwewe mtaambiwa mfunge mikanda utaangalia nje kwenu kwenye vumbi na harufu kali!

Mwewe ataenda spidi na kupaa , humo ndani Bata zitaendelea, utakula na kunywa na kusinzia, mara ghafla ukiwa unaota unakimbizwa na shetani kwenye sherehe ya kitchen party huko Buza kwa Mpalanger mara ghafla utaamshwa na kuambiwa ukae sawa na kufunga mkanda maana mnakaribia kutua ukicheki nje mf Amsterdam utaona Jiji zuri na safi na sasa utakumbuka jinsi kwenu mlivyo maskini , wachafu na wajinga!

Binafsi naamini Aircraft ni technology ya kipekee sana, mzungu akili mingi sana!

Mtu mweusi atabaki mjinga tu milele na milele kama viongozi wake weusi wataendeleza kizazi cha wajinga kwa kuongoza nchi kijinga!
We unaambiwa NIGERIA ilikuwa na mafuta mengi kuliko hata Dubai na pia Nigeria ipo blessed na madini kibao ila kila leo wanamivutano ya kitahira mpaka wananchi wake wanakuwa matapel wa dunia nzima kutwa migogoro ya kijinga mixer udini wa hizi dini zilikuja na melikebu mpaka sasa Dubai ni giant dhidi ya Nigeria kiuchumi.
 
Mpaka hapa tulipo kama nchi, tumetoka mbali sana!
Tumepitishwa jangwani sisi, kwenye miiba na mbigili tumepitishwa,

Tumepita kwenye machungu makali na kisha viongozi wetu badala ya kutengeneza vijana na watumishi waadirifu, wamejikuta wakitengeneza vijana wezi, watumishi wa umma mafisadi na Taifa la watu waliokata tamaa kabisa na kesho yao

Sababu moja wapo ni viongozi kuwa majizi na mafisadi huku wao wakiwahimiza waliochini yao wawe waadirifu mpaka kufa ili hali wakiwaona viongozi wao wanavyojichotea mabilioni ya mapesa na kutengeneza ufalume wao wa ki anasa hapa duniani

Hiyo imekuwa ni ambukizo baya sana kiasi ambacho hata wale viongozi tuliodhani wako sahihi katika kuliongoza Taifa letu bado wananchi na hasa watumishi wa umma, wamekuwa wakitupia lawama kwa viongozi hao na ukiangalia kwa undani, ni kuwa tu pengine imetokea kubanwa mianya ya ufujaji wa pesa za Wananchi

Tumeshuhudia aina mbalimbali ya viongozi na jinsi ambavyo viongozi hao wamekuwa wakiweka mikakati mbali mbali katika kulinasua Taifa letu ili kuondokana na umasikini uliopo

Lakini kila tulipopata kiongozi, sauti kubwa imekuwa ikisikka kuwa, HATOSHI NA HAFAI kwa kuwa huyu ni dhaifu, huyu ni mshamba na huyu ni hivi na vile!

Kama mtanzania, matamanio yako ni kupata kiongozi yupi na afanye nini ili pengine moyo wako utasema, This is the leader we will travel with to bring us the promised land


Kinachosikitisha zaidi, jamii pia ilishawakatia tamaa hata wapinzani, wakiwaona ni wale wale na hawatabadirisha chochote zaidi ya kujibadisha wao na maisha yao

Taifa la watu waliokata tamaa! Dawa yake nini?

Viongozi nao walishakata tamaa, hawana mawazo mapya, hawana uwezo wowote wa kuwatoa wananchi kwenye mtanzuko huu wa maisha duni na kukata tamaa, badala yake wamebaki kujisifia wasivyovianzisha wakati huohuo wakiviita ni miradi ya kukurupuka!
we ndio umekata tamaa, ukiona vipi kajitundike tu,siye tunadunda na kufurahia maisha ndani ya Taifa letu pendwa
 
Back
Top Bottom