Taifa la washabikia uzinzi - Tanzania

Taifa la washabikia uzinzi - Tanzania

Nyangomboli

Umeongea kwa gadhabu sana lakini inaonekana kama hujui au ume-overlook lengo la hoja yenyewe. Unaweza kutuambia nidhamu ya Kanumba hadi aitwe kioo cha jamii ni ipi, kutembea na mtoto au kuigiza mambo ya ngono au kufa katika mazingira ya uzinzi? Kama si uzinzi aliokuwa anafanya unaweza kutuambia yule mtoto underage alikuwa anatafuta nini kwa Kanumba usiku wa manane. Hicho ndicho unakiita kioo cha jamii. Kama Kanumba ni kioo cha jamii basi ndio maana mleta hoja anasema tumekuwa taifa la kushabikia uzinzi na kuupaka marashi.

Kwa uelewa wangu, Kanumba amechangia taifa kuendeleza uvivu, badala ya kukaa na familia zetu hasa jioni kutafakari tujengeje taifa, kina mama wanawaza kungojea maigizo ya uongo na ngono zembe, amefanikiwa sana kuwafundisha kinamama jinsi ya kuwa cheat wanaume zao. Vile vile amechangia sana kurudisha nyuma maadili ya vijana wetu, hasa kitendo chake cha kutembea na mtoto mdogo, kimeniuma sana nikizingatia mtoto wangu wa kike amejifunza nini wakati kamuona hata rais kumbe anafurahia matendo hayo, nitaanzia wapi kumuonya, it is a pity indeed to the president and its cabinet.

feedback ndg yangu,
ni kweli kabisa, inauma sana kuona viongozi wakuu wa nchi wakishabikia upuuzi kisa eti ni marehemu. huyu jamaa kaharibu sana jamii yetu kwa mambo yake, juzi nilikua naangalia muvi yake moja ikanitia kichefu chefu sana, anapinga eti Mungu hayupo, si mafundisho ya shetani haya?

cha ajabu watu wanamshangilia na kumpa sifa za uongo kama hero of the nation, ametutia aibu sana. watanzania tuache unafiki let call a spade a spade and not the big spoon. ndio amekufa, lakini marehemu alikua mchafu, period.

cha msingi ni kuionya jamii yetu ya kitanzania kutoiga matendo ya marehemu hasa uzinzi
 
...acha fikra mgando ww, kwani we hujui ngono zembe ni hatari?, hujui kunywa pombe kupita kiasi ni hatari?, ni nani aliyetoa onyo kwa wasanii kujichubua na mamake up yaliyopitiliza alipokufa wacko?.....jifunze kubadili tabia mwnyw sio kila k2 tupoteze muda...tumeshachoka kuwa taifa la hamasa, tunahamasishwa kuvaa kondomu, kutovuta sigara, kunawa mikono kabla na baada ya kula, kuchmba mashmo ya vyoo, uzazi wa mpango...etc eee
 
Hatima ya lulu kupelekwa mahakama au la ni swala la kisheria zaid. Nalipo mikononi mwa Dpp na vinginevyo. Je? Akisema hana kesi ya kujbu jamii itaic vp
 
Mkuu mbona hueleweki?. Matendo ya mtu yaachwe yahukumiwe na mungu mwenyezi, sisi kama wanadamu hatupaswi kuhukumu mtu. Kwa kuwa Kanumba amefariki kutokana na ugomvi na mpenzi wake haitukatazi sisi mashabiki wake na tuliovutiwa na kazi yake wakati wa uhai wake kuomboleza.

Inawezekana ni kweli kabisa kuwa ni mzinzi lakini katika dunia ya leo na hasa Tanzania ni only 0.001% ya actively sexual people hawajawahi kuwa na wapenzi kabla ya ndoa. Wengi wetu siku hizi huanza na mahusiano kwanza then tukaamua kufunga ndoa, ni nani ajuaye kuwa Kanumba(if he could live longer) na Lulu wangekuja funga ndoa au la?. Unapoongea tunashabikia uzinzi unatakiwa na uhakika beyond reasonable doubt kuwa wewe hujawahi kufanya mapenzi nje ya ndo a chance of 0.0001.

Tusiangalie vibanzi vilivyo machoni mwa wenzetu bila kutoa boriti zilizo machoni mwetu. Sidhani kama kumzika Kanumba ni kushabikia uzinzi huo ni upotoshaji wa hali ya juu sana.
Kwa kifupi nilivyokuelewa hutaki tuseme kafa kwa uzinzi kwa vile karibu wote tumepitia uzinzi, poor analysis, ni sawa na kusema utamruhusu mtoto wako wa kike say aendeleze uzinzi kwa vile wewe na mke wako mlikutana kwenye uzinzi. Ni hatari sana kuwa na jamii yenye mawazo kama yako, kinachotakiwa tukemee tabia hii hata kama imefanywa na kipenzi chenu Kinumba.
 
Vifo:stiv 2k kisu,J.mjema kisu,F.nely kisu,vivian&complex uzinzi na ulevi,max HIV,leo kanumba pombe&uzinzi,tubadilike!
 
kanywe maziwa mgando yatakusaidia ndugu yangu.

Naona tumbo linakusumbua!!
 
naunga mkono mtoa hoja sio kwamba anamuazibu anaongea ukweli

Mkuu umeaema ukweli wengi wanaishia kushabikia wana kwepa kusema ukweli hiv kitendo ikinichakushabikia kweli/huu ni kuweka pembeni maadiri ya dini zetu naamini hakuna kiongozi yeyote wa dini anaweza kushabikia ili bari atakemea watanzania tubadilike
 
unajua ni wanandoa wangapi wanakufa kwa kuchomana visu wao kwa wao?
Unajua ni ajali ngapi ambazo hazisababishwi na ulevi ambazo zinachukua maisha ya watu!! Na hasa vijana? Au kwavile huwajui, sio masupastaa!!!
 
ndiyo vifo vya macelebrity hivyo we unataka angekufaje? na kufia wapi?,kanisani?maisha na kazi zake vimetengeneza mwelekeo wa kifo chake..angalia vifo vya mastaa wa ulaya akina whitney Houston,2 Park na wengineo wamekufa kutokana na viashiria vya kazi na matendo yao.
 
Ingawa tumesikitishwa na kifo cha Steven Kanumba, kuna haja ya kuuangalia ukweli kama ulivyo. Pamoja na kupewa heshima kubwa kuliko hata aliyostahiki kutokana na wakati wa kifo chake, sasa basi turejeeni kwenye mambo muhimu. Tumefanikiwa kuuonyesha ulimwengu kipaumbele chetu hasa kujali sana usanii kuliko uchapakazi. Najua wengi hawatapenda mawazo haya. Ukweli ni kwamba nimeshangaa kuona Kanumba akishabikiwa na viongozi kuliko hata marehemu makamu wa rais Omar Juma. Kunani? Je hii ni sawa? Sikuona rais kwa wakati tofauti na mkewe, na vigogo wengine wakimiminika kwenda kwenye msiba wa Omar Juma kwa spidi kama hii. Hakika Tanzania ni nchi ya wasanii.
Bwana alitoa Bwana amechukua. Maisha yanaendelea. Turejee kwenye kupambana na ufisadi, usanii, uvivu na urongo basi. Au siyo?
 
Huu ujumbe anatakiwa apewe mkulu.
Kwa yeye utafikili amechanjiwa na misiba.
 
It is a pity kuwa nchi nzima na Rais wetu, PM, etc wanashabikia uzinzi. Huyu Marehemu (RIP) alikuwa katika matendo yasiyo mpendeza Mungu, lakini hayo yote Tanzania hawayaoni. Huyu alikuwa anafanya uzinzi, basi najua mtanipiga madongo, potelea mbali.
Michael Jackson pamoja na shutuma za kuwadhalilisha watoto, kifo chake kiliombolezwa na maelfu ya watu duniani kote! Jililie nafsi yako na siyo ya mwenzako!
 
It is a pity kuwa nchi nzima na Rais wetu, PM, etc wanashabikia uzinzi. Huyu Marehemu (RIP) alikuwa katika matendo yasiyo mpendeza Mungu, lakini hayo yote Tanzania hawayaoni. Huyu alikuwa anafanya uzinzi, basi najua mtanipiga madongo, potelea mbali.

Ni uzinzi ama uasherati? Maana Mzinzi ni yule aliyeoa tu
 
Hiki ni kipimo kizuri sana cha akili za watanzania. Perfect unawajua nini kilicho muhimu kwao. Ndio maana magazeti ya udaku yameshawajua wapi pa kuwalia pesa kiulani. Tena hamna cha ngazi za juu wala fisadi wala mkulima wala dni wengi wamekua washabiki wa upuuzi.
 
Hivi Tanzania nzima mnzinzi ni Kanumba peke yake.Mnaelewa maana ya neno Uzinzi na Uasherati??Mngekuwa mnaelewa maana yake
sidhani mngediriki kumshupalia Kanumba.

Mbona hata jf lipo jukwaa la uzinzi na uasherati linafurahiwa tu....au mmemchukia tu Kanumba..
 
Hivi Tanzania nzima mnzinzi ni Kanumba peke yake.Mnaelewa maana ya neno Uzinzi na Uasherati??Mngekuwa mnaelewa maana yake sidhani mngediriki kumshupalia Kanumba. Mbona hata jf lipo jukwaa la uzinzi na uasherati linafurahiwa tu....au mmemchukia tu Kanumba..
hapo sasa!
 
Back
Top Bottom