King Suleiman
JF-Expert Member
- Dec 27, 2010
- 496
- 328
Nyangomboli
Umeongea kwa gadhabu sana lakini inaonekana kama hujui au ume-overlook lengo la hoja yenyewe. Unaweza kutuambia nidhamu ya Kanumba hadi aitwe kioo cha jamii ni ipi, kutembea na mtoto au kuigiza mambo ya ngono au kufa katika mazingira ya uzinzi? Kama si uzinzi aliokuwa anafanya unaweza kutuambia yule mtoto underage alikuwa anatafuta nini kwa Kanumba usiku wa manane. Hicho ndicho unakiita kioo cha jamii. Kama Kanumba ni kioo cha jamii basi ndio maana mleta hoja anasema tumekuwa taifa la kushabikia uzinzi na kuupaka marashi.
Kwa uelewa wangu, Kanumba amechangia taifa kuendeleza uvivu, badala ya kukaa na familia zetu hasa jioni kutafakari tujengeje taifa, kina mama wanawaza kungojea maigizo ya uongo na ngono zembe, amefanikiwa sana kuwafundisha kinamama jinsi ya kuwa cheat wanaume zao. Vile vile amechangia sana kurudisha nyuma maadili ya vijana wetu, hasa kitendo chake cha kutembea na mtoto mdogo, kimeniuma sana nikizingatia mtoto wangu wa kike amejifunza nini wakati kamuona hata rais kumbe anafurahia matendo hayo, nitaanzia wapi kumuonya, it is a pity indeed to the president and its cabinet.
feedback ndg yangu,
ni kweli kabisa, inauma sana kuona viongozi wakuu wa nchi wakishabikia upuuzi kisa eti ni marehemu. huyu jamaa kaharibu sana jamii yetu kwa mambo yake, juzi nilikua naangalia muvi yake moja ikanitia kichefu chefu sana, anapinga eti Mungu hayupo, si mafundisho ya shetani haya?
cha ajabu watu wanamshangilia na kumpa sifa za uongo kama hero of the nation, ametutia aibu sana. watanzania tuache unafiki let call a spade a spade and not the big spoon. ndio amekufa, lakini marehemu alikua mchafu, period.
cha msingi ni kuionya jamii yetu ya kitanzania kutoiga matendo ya marehemu hasa uzinzi