Taifa la washabikia uzinzi - Tanzania

Loh!! ubinadamu kazi kweli kweli!!kuna wengine kazi yao kukosoa na kuona ubaya wa watu wengine. Unajua ni umauti gani utakaokupata ndugu????au waongea tuu ilimradi una uwezo???tumia pumzi, akili, hekima na uwezo aliokupa Mwenyezi Mungu kumtukuza kwa kutenda meme siku zako zilizobakia na siyo kuangalia na kunyooshea vidole wengine..bora ungenyooshea walio hai na siyo wafu...waache wapumzike Mungu ndiye awahukumu kwani wewe hukuumba mtu hapa duniani ati!!! Hata maandiko yanasema hakuna mwenye haki hata mmoja yeye anayethubutu kunyooshea kidole maovu ya wenzie amejiangalia yeye??hawa ndo wale wambea waliozoea kusema mabaya ya wenzao pasi na kujua kuwa anajipalia makaa kinywani mwake..Hujui wewe utaondoka kwa njia gani hapa duniani hivyo tumuombee na tuwaombee wote Mwenyezi Mungu awarehemu na kuwapa pumziko la milele...Tujifunze kukosoa walio hai na siyo wafu jamani...Kama ulikuwa jasiri na wewe ni jasiri na mtakatifu saaana andaa darasa la kuwaonya vijana na watanzania na siyo kusemea marehemu wetu vibaya. Maandiko yanasema pia Ulimi ni sumu ya **** ukitumika vibaya hivyo ndugu tujiangalie sana sisi wenyewe (tutoe maboriti kwenye maisha yetu kabla ya kuangalia kibanzi kidogo kwenye macho ya wenzetu). Kumbuka hata Yesu alisema usishangae makahaba na watoza ushuru wakaingia mbinguni wakawaacha wale wanaojiita wameokoka..tujiangalie sana sana ndugu zangu yamkini Mungu anataka tuokolewe kwa kupitia vifo au matatizo ya wenzetu na siyo tuangamie...Tubuni sana kwa maana Ufalme wa Mungu Umekaribia...
 
Usukumani kanumba kuliliwa ni sawa kabisa. Aliyekufa ni wa asili yao hivyo ni mmoja wa wasukuma amepotea.
 
Yesu akisha kubaki pekee na yule mwanamke mzinzi, alimwambia aende na amani kwa vile dhambi yake ilisamehewa, LAKINI alimwambia asiende kutenda tena uzinzi. Vivyo hivyo wale waliomshutumu yule mama hawakupaswa kuendelea kutenda dhambi ile waliomshutumu yule mama.
Tanzania bila maadili ya kimaandiko inawezekana.
 
That being the
case,Lulu aachiwe huru mapema iwezekanavyo.
Mkuu hii tafakuri makini kama watu hawamuoni kanumba kama mfano mbaya kimaadili. Basi sioni kwa nini Lulu ashikiliwe kwa mauaji ya Kanumba.
Yule aliyesema usiue ndiye aliyesema usizini.
Kosa la Kanumba na la Lulu mbele za Mungu yote ni dhambi.
 
mkuuu nakuunga mkono! kanumba alikuwa kwenye uzinzi na hakuna anayezungumzia hilo! tumsifu kwenye kazi zake ila ukweli utabaki pale pale
 
It is a pity kuwa nchi nzima na Rais wetu, PM, etc wanashabikia uzinzi. Huyu Marehemu (RIP) alikuwa katika matendo yasiyo mpendeza Mungu, lakini hayo yote Tanzania hawayaoni. Huyu alikuwa anafanya uzinzi, basi najua mtanipiga madongo, potelea mbali.

hongera wewe ambae hujawah kuzini toka uzaliwe, na mungu akupe mema mengi dunian na akhera
 
Uzinzi au ubaya wake haufanyi watu wakae kimya na kusema mwacha aende maana alikua mtu mbaya. Hapa watu wanalia kwa mema aliyoyafanya na kuifanyia nchi ya Tanzania kwa ujumla. Mabaya mangapi umefanya na Mwenyezi Mungu kakupa uhai mbaka leo? Unataka kusema wewe siku ukirudi mavumbini nduguzo wasilie eti kisa ulifanya ubaya siku fulani na ukaonekaka au watu wakajua.. Wewe ni mzinzi sembuse na kwenye msiba wako watu watalia, kama umewahi kuzini sema mapema kwamba jamani mimi ni mzinzi hivyo basi kwenye msiba wangu msinililie maana nimewahi kufanya ubaya, otherwise PIGA KIMYA mzazi.
 

Wazinzi wa JF hawadili na under 18...
Huyo alikuwa mbakaji.
Na kama leo akifufuka ana kesi ya kujibu kwa kukaharibu katoto ambako tulimkabidhi akafundishe sanaa, ila ye akaenda kukafunza ngono...
 
mtoa mada umekurupuka.wacha wenye moyo wa kuomboleza waomboleze.
 
It is a pity kuwa nchi nzima na Rais wetu, PM, etc wanashabikia uzinzi. Huyu Marehemu (RIP) alikuwa katika matendo yasiyo mpendeza Mungu, lakini hayo yote Tanzania hawayaoni. Huyu alikuwa anafanya uzinzi, basi najua mtanipiga madongo, potelea mbali.

Kama nimeelewa vizuri kilichotokea ni Kifo cha S. Kanumba na Watanzania uliowataja walikuwa wakiomboleza kifo hicho hapa jambo kuu lilikuwa ni 'KIFO' regadless kimetokana na uzinzi au ajali ya gari au maradhi. matendo ya marehemu na tuliobakia ni kazi ya MUNGU kuhukumu, sisi kama binadamu tuna haki ya kuomboleza kwa kifo cha yeyeto anayetuhusu ndio kibinaadamu . RIP Steve
 
Mkuu hii tafakuri makini kama watu hawamuoni kanumba kama mfano mbaya kimaadili. Basi sioni kwa nini Lulu ashikiliwe kwa mauaji ya Kanumba.
Yule aliyesema usiue ndiye aliyesema usizini.
Kosa la Kanumba na la Lulu mbele za Mungu yote ni dhambi.

afadhali umesema hayo maneno mekundu MBELE ZA MUNGU wote ni wadhambi. sisi kama binadamu tufanye yanayotupasa na sio kuanza kuwahukumu wenzetu kwa matendo yao kwani hakuna aliye msafi. Cha msingi hapa Steve amekufa wanaompenda wana haki ya kumlili na kuomboleza kifo chake, na Lulu kahusishwa na kifo chake ana haki ya kusimama mbele ya vyombo vya sheria kwa mujibu wa sheria za nchi yetu ajibu tuhuma. haya mengine ya umalaya uzinzi n.k. yatabaki kuwa yalikuwa ni sehemu ya maisha yao kazi ya kuwahukumu ni ya MUNGU na kwa kuwa wote wametenda dhambi basi uzinzi wa kanumba hamuondolei LULU kosa la kuua (kama lipo). Ila kwangu mimi naona bora tu haka katoto LULU kakapumzike kwanza gerezani huenda kakipata nafasi ya kurudi uraiani katatulia na kubadilisha life style yake, at her age alikuwa ni bad news na msanii ambaye alikuwa ni mfano mbaya kwa watoto wa kike wanaomtazama
 
Muanzisha mada nina wasisi na jinsi ulivyo lelewa.Kama kanumba alikuwa mzinzi sio sabbu ya kusherekea kifo chake bana.Kama Jirani yako kafa kwa ukimwi au kugongwa na gari akiwa amelewa hutaenda kwenye huo msiba? Alafu kama umeoa,siku ya kwanza ku do uli do ukiwa kwenye ndoa?
 
MAMC point noted,Jamii yetu inaelekea kubaya sana ni kama issue ya Semunge wananchi na viongozi wote walikua wanakimbizana kwenda kwa babu kabla ya kufanya research mpaka waziri anahaidi kutengeneza barabara kwa excuse ni kivutio cha Utalii.Mbona sijaona wanaotetea haki za watoto hata kwenda kumfariji LULU? maana bado hajadhibitika kuwa na hatiaKanumba amefanya nini cha muhimu kinachostahili hiyo publicity mpaka serikali kutoa hiyo 10m kama rambi rambi?
 
One thing is clear to me in this thread. Wengi wa pro-Kanumba ni females while the majority of anti-Kanumba ni males,why?

NB uchunguzi imezingatia IDs tu,i stand to be corrected.
 
It is a pity kuwa nchi nzima na Rais wetu, PM, etc wanashabikia uzinzi. Huyu Marehemu (RIP) alikuwa katika matendo yasiyo mpendeza Mungu, lakini hayo yote Tanzania hawayaoni. Huyu alikuwa anafanya uzinzi, basi najua mtanipiga madongo, potelea mbali.

Iko ivi, kanumba ni mtu wakawaida tu tofaut nikazi yake, sasa ktk misiba iliyoudhuriw nawatu weng ni mitatu tu Mwl nyerere+Sokoine moringe+S kanumba, sasa basi sk hakumpigia mtu cm aje kwnye msiba nimatakwa ya mtu mmoja mmoja, hivyo ni sis wenyew, pia hakuna alie msafi hapa,
 
Mia ya mia...

hivi ni mema yepi aliyoiletea s.k tz? Tz imepata misaada ya dola ml ngapi kutokana na sk kuitambulisha tz kimataifa? Kila 1 anajijengea sifa kutokana na mchango wake katika jamii na sifa hiyo ndo ataondoka nayo hapa kwenye sayari dunia. Sk ameithibitishia tz na kizazi chake kwamba tasnia ya filamu tz imegubikwa na uzinzi kwenda mbele! Kwanza angalia hata film zao hata maadili hazina - tunaojiheshimu tunaogopa kuziangalia na watoto. Ukiondoa akina muhogo mchungu the rest ni wavamizi tu wenye lengo la kuwadhililisha mabinti ambao nao kwa kukosa malezi kwa wazazi wao they hav become easy target to immoral people like the late s.k and the like
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…