Loh!! ubinadamu kazi kweli kweli!!kuna wengine kazi yao kukosoa na kuona ubaya wa watu wengine. Unajua ni umauti gani utakaokupata ndugu????au waongea tuu ilimradi una uwezo???tumia pumzi, akili, hekima na uwezo aliokupa Mwenyezi Mungu kumtukuza kwa kutenda meme siku zako zilizobakia na siyo kuangalia na kunyooshea vidole wengine..bora ungenyooshea walio hai na siyo wafu...waache wapumzike Mungu ndiye awahukumu kwani wewe hukuumba mtu hapa duniani ati!!! Hata maandiko yanasema hakuna mwenye haki hata mmoja yeye anayethubutu kunyooshea kidole maovu ya wenzie amejiangalia yeye??hawa ndo wale wambea waliozoea kusema mabaya ya wenzao pasi na kujua kuwa anajipalia makaa kinywani mwake..Hujui wewe utaondoka kwa njia gani hapa duniani hivyo tumuombee na tuwaombee wote Mwenyezi Mungu awarehemu na kuwapa pumziko la milele...Tujifunze kukosoa walio hai na siyo wafu jamani...Kama ulikuwa jasiri na wewe ni jasiri na mtakatifu saaana andaa darasa la kuwaonya vijana na watanzania na siyo kusemea marehemu wetu vibaya. Maandiko yanasema pia Ulimi ni sumu ya **** ukitumika vibaya hivyo ndugu tujiangalie sana sisi wenyewe (tutoe maboriti kwenye maisha yetu kabla ya kuangalia kibanzi kidogo kwenye macho ya wenzetu). Kumbuka hata Yesu alisema usishangae makahaba na watoza ushuru wakaingia mbinguni wakawaacha wale wanaojiita wameokoka..tujiangalie sana sana ndugu zangu yamkini Mungu anataka tuokolewe kwa kupitia vifo au matatizo ya wenzetu na siyo tuangamie...Tubuni sana kwa maana Ufalme wa Mungu Umekaribia...