Utawala bora na Uwajibikaji!
Hivi ni vitu gani? Nani hawajibiki? Je utawala siyo bora? Nani ni mtawala? Mtawala ndiye hawajibiki? Au anayetawaliwa hawajibiki? Kipi kinaathirika zaidi ikiwa mtawala na mtawaliwa hawawajibiki katika nafasi zao?
Tunaona sawa ila tunatazama tofauti.Ndiyo,mitazamo tofauti katika kuijenga jamii yetu.
Itakuwa kheri kama mitazamo yote itakuwa chanya na yenye afya kwa maslahi mapana ya taifa.
Hivyo katika kutumia uhuru wa kujieleza na kutoa maoni leo kijana wenu nimechanganua kwa ufupi kabisa wapi tuboreshe kuijenga jamii yetu
ELIMU: Sekta nyeti kabisa iliyoibeba taswira ya jamii. Mitaala bora huchochea uwajibikaji na uweledi katika utendaji na utawala. Mitaala iliyopo inahitaji maboresho makubwa sana kuweza kufikia dhamira ya dhati kuwa na jamii imara na yenye misingi thabiti. Elimu yetu ina nadharia ya kumuwezesha kijana kujiajiri lakini uhalisia unasimama kwenye kuajiriwa. Aina hii ya elimu inamnyima mwananchi nafasi ya kuhoji na kuchanganua mambo yanayoendelea katika nchi yake kwa sababu ya uelewa mdogo na kutokujua haki na wajibu wake katika kujenga nchi.
Elimu haisimami tu mashuleni na vyuoni pia hata elimu ya jamii. Jamii iliyoelimika inaepushwa na mambo kadha wa kadha kama vitendo vya kihalifu, uvunjaji wa sheria,uonevu, ukandamizwaji na udhalilishwaji.
Tuongeze majukwaa ya kutoa elimu,ujuzi na maarifa ili tuache kuendelea kutoa nafasi za teuzi kwa wazee waliofeli na tuwe tayari kutoa nafasi kwa vijana ili waje na akili mpya inaliyojaa ari ya mafanikio na ubunifu.
Tungekuwa na elimu yenye yenye mtaala wetu unaoakisi tamaduni na mila zetu tusingefika huku ambapo kila msomi anawaza ataitiaje serikali hasara, vijana wanasoma wakiwa hawajui nini hatima yao mbele huku serikali ikiendelea kuwapa vipaumbele wasomi wa zamani. Mtu alishastaafu eneo moja anarudishwa kufanya kazi eneo lingine. Huku kubebana ndiko kunasababisha tunashindwa kwenda sawa na kasi ya dunia kwa kufungia mawazo na ubunifu mpya kabatini.
Unahitajika mdahalo zaidi ili kutoa nafasi kwa wananchi na wadau wa elimu kueleza changamoto za mtaala wetu na kipi cha kufanya kuboresha hali ya elimu nchini iendane na dira ya nchi yetu.
UONGOZI NA SIASA: Ni nini dira ya nchi hii? Kila kiongozi anayeingia madarakani anakuwa na vipaumbele na sera zake. Hatuna mkakati wa muda mrefu kuboresha hali ya kiuchumi na kijamii. Hii yote inasababishwa na KATIBA.
Ndiyo, katiba iliyobeba maono ya tangu 1977 haiwezi kuwa sawa na hali inayoendelea hivi sasa. Tunahitaji mapitio na maboresho ya katiba hii ili kuweza kuwa na jamii yenye VIONGOZI BORA NA WANAOWAJIBIKA. Siasa imeiharibu jamii yetu. Kila mmoja yupo kuangalia maslahi yake. Imefika mahali hakuna wa kumuamini baina ya chama tawala wala wapinzani na wakosoaji. Hii yote inasababishwa na elimu duni ya wananchi na ukiritimba.
Rasiliamali za nchi zinatumiwa vibaya kwa maslahi ya watu wachache huku wanaohoji wakinyoshewa mtutu wa bunduki au wakinyamazishwa na RUSHWA. Hakuna tena ulinzi katika rasilimali za nchi kila mmoja anakula pale anapoona panamtosha. Ufisadi katika mali za nchi umekuwa wazi na hakuna anayehoji wala kuwajibishwa.
Mfano ulio hai na wa hivi karibuni ni ripoti ya mkaguzi wa serikali. Hakuna mradi wa serikali uliozalisha faida kwa nchi na hakuna kiongozi aliyewajibishwa kutokana na hasara kubwa zilizotokea bali wanahamishwa vigogo kutoka sehemu walizoharibu kupelekwa sehemu zingine.
Katiba inamlinda mtawala. Ni vigumu kumuwajibisha kiongozi anayetenda kinyume na sheria za nchi na asiyewajibika ilhali yuko ndani ya misingi ya katiba.
Kumekuwa na mfululizo wa malalamiko kutoka waajiriwa, wafanyabiashara, wawekezaji,wakulima kuhusu hali ya kiuchumi na mfumuko wa bei, mrundikano wa kodi na usumbufu kutoka kwa watendaji wa serikali lakini serikali imeshindwa kutatua matatizo hayo. Hii yote inasababishwa na kutokuwajibika na viongozi katika nafasi zao hivyo kutoa mianya ya RUSHWA na UKWEPAJI KODI ambao unaurudisha nyuma zaidi uchumi wa nchi.
Bahati mbaya sana tumeingiza siasa katika kila nyanja za kijamii. Siku hizi viongozi wa dini wanahubiri siasa, wasomi wameingia kwenye siasa wanachambua mambo kwa kuzingatia hisia na kada kuliko uhalisia, katika mashirika ya umma ndiyo kumechafuka zaidi kila mteule na muajiriwa ameshachagua upande.
Bunge letu linajadili hoja kwa majibu mepesi. Ni aibu kusikia jambo ambalo limeleta mkanganyiko katika jamii halafu majibu yanayotolewa na wahusika serikalini ni mepesi na wanatoa kwa kuhusisha sheria ambayo nayo ina mapungufu na mwanya wa upigaji.
Tukiamua kuibadili katiba na tukaweka mzani wa siasa sawa bila kuhusisha nguvu dola kama jeshi la polisi tutakuwa na viongozi wanaowajibika na wanaotekeleza sera na dira ya nchi kwa maslahi ya taifa na watu wake.
HABARI NA MAWASILIANO: Zamani tuliamini kalamu ya mwandishi ni nguvu mojawapo katika kubadilisha jamii. Kalamu ilikuwa na nguvu ya kumuwajibisha kiongozi na kuionuesha serikali wapi imepuyanga na wapi imeenda sawa, kipi cha kufanya na kipi ni cha kukiacha maana hatuwezi kulibeba kila jambo lisilo na msingi kwa taifa.
Taaluma imeingiliwa na siasa. Ukandamizwaji uliolandana na utekaji, utesaji na mauaji ya waandishi wa habari ukaitia hofu tasnia. Waandishi wamechagua upande na kuanza kufata kila kinachosemwa na wakuu wa nchi.
Waandishi wamekandamizwa nao wameamua kuwakandamiza wakosoaji. Kalamu imeamua kufuata mkumbo wa kukosa maadili na kuanza kutumika kuchafua wanaharakati walioamua kuifumbua macho jamii. Wamewapa watu majina mabaya na kuanzisha kampeni kedekede kuhakikisha jambo la mtawala linafanikiwa. Inatia hasira na kuhuzunisha ila unaweza kuwaelewa maana kila mmoja amechagua maslahi binafsi bila kuzingatia nini kinafanyika.
Majukwaa ya uchambuzi yamepotea na yaliyopo yanapangiwa hoja za kujadili. Mitandao ya kijamii inatumika kusambaza habari zisizo na mantiki kwa jamii.
Kwa mfano ulio hai wameibuka watu wanaojiita CHAWA WA MAMA. ndiyo, ni watu wazima ila wameamua kujiita chawa. Wameichukua tasnia ya habari, mitandao ya kijamii kwa bajeti za watu binafsi walio serikalini na kuhakikisha kila anayesimama kuisema serikali inapokosea anashambuliwa ipasavyo kuhakikisha kile anachosema hakisikiki.
Hatuwezi kuwa na kiongozi muwajibikaji ikiwa mtaani anaimbwa na kusifiwa hata katika mambo ambayo ni wajibu wake kutktleza.
Kiongozi hakosolewi wala kuelezwa uhalisia wa mambo atajuaje jamii inachohitaji.
Tuiweke tasnia huru kutoa taarifa kinachoendelea katika jamii na serikalini ili watu waweze kutoa maoni yao katika kuijenga Tanzania moja.

Upvote
1