Taifa letu limeoza kwa kukosa maadili na tutaona mengi sana

Taifa letu limeoza kwa kukosa maadili na tutaona mengi sana

Omusolopogasi

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2017
Posts
7,101
Reaction score
18,051
Wana JF,

Mwaka 2020 ulikuwa mwaka wa uchaguzi mkuu. Mambo yalifanywa na viongozi wetu yanaonyesha kwa kiasi kikubwa suala la maadili katika nchi yetu limepigwa teke. Taifa liimeoza kabisa. Uozo umeanzia kwenye kiini. Kuna mambo ambayo pengine hayatakushangaza iwapo yatafanywa na wakora mtaani. Lakini yanapofanywa na Rais wa nchi na wasaidizi wake, basi kuna tatizo kubwa la msingi. Taifa inabidi likae chini na kujiuliza ni wapi limekosea.

Kitendo cha Rais, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, TISS na wengine kuchapisha makaratasi feki ya kura na kumwekea Rais ambaye ni mgombea tiki pamoja na wagombea wake wa ubunge na kuyaingiza kwenye vituo vya kupigia kura kwa nguvu ya polisi kilinifikirisha na kunisononesha sana. Watu wenye maadili hawawezi kufikiria, achilia mbali kufanya kitu kama hicho. Taifa lenye maadili haliwezi hata kufikiria kitu kama hicho. Forgery ya kiwango cha "kitaifa" ikiongozwa na Ikulu na vyombo vyake ni jambo la kusikitisha sana.

Kama Rais na viongozi wakuu wa kitaifa walifanya hivyo Oktoba 2020, kwa nini sisi watu wa kawaida tusifanye haya mambo ya ajabu tunayoona kila siku? Kwa nini mimi na wewe tusifoji vyeti vya elimu? Kwa nini tusifoji majina ya watu na kuyatumia? Kwa nini tusitumie vyeti vya watu wengine kutafuta na kufanyia kazi? Kwa nini tunashangaa kuwa na vibaka, majambazi km Ikulu inaweza kuwaza na kutekeleza ujangili wa aina ya Oktoba 2020? Kwa nini unashangaa mtihani wa NECTA unapoliki? Kwa nini unashangaa mke anavyo choma nyuma na kuumua mumewe ndani? Yote haya yanaonyesha jamii yetu isivyokuwa na maadili kuanzia kileleni hadi bondeni.

Tumeona mamia ya watu ambao serikali imesema walibambikiziwa makosa na kusota mahabusu wakiachiwa. Kama serikali inaweza kufanya hivyo, kwa nini tunashangaa vibaka kuongezeka wakati watu wenye madaraka makubwa ya kuongoza nchi ni vibaka pia? Rais anatoka miongoni mwetu. Tukiwa jamii ya vibaka, Rais naye atakuwa kibaka tu kwa sababu hatuwezi kuleta Rais kutoka nchi nyingine asiyekuwa Mtanzania.

Jana nimesoma hapa habari ya mtihani wa mchujo wa kazi za TRA kuliki. Sikushngaa. Nilijua ni matokeo tu ya Taifa kuoza kuanzia kwenye kiini.

Taifa limekosa maadili kuanzia kwenye kiini kabisa. Taifa limeoza. Tafakari. Chukuwa hatua!

1628532430369.png
 
Back
Top Bottom